Kwa niliyoyaona wodi ya wazazi, simtii mimba tena mke wangu

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
19,454
25,372
Aisee wakuu muwe mna waheshimu sana mama zenu kwa kweli ,kwa niliyoyaona wodi ya wazazi aiseee nimeathirika kisaikolojia sitamani tena kumtia mimba mke wangu nahisi kama atakufa kwa kweli.

Roho ilikuwa juu juu kipindi mke wangu anaenda kujifungua ,nilivyoingia wodi ya wazazi ndio kabisa nikaishiwa nguvu kwa kuwaonea huruma.

Jamani jamani wanawake wanateseka sana wakiwa wanajifungua yani nilihisi mke wangu hatoki akiwa hai lazima afe.

Kwa kweli hata nikipita mtaani minions mwanamke ana ujauzito natamani kulia kwa kumuonea huruma ,Sitamani kabisa kumpa mke wangu mimba kama kungekuwa na uwezekano wa kufunga kizazi kwa mwanaume ningeenda walai
Maana wanawake wanapitia mateso makubwa sana.

Ushauri wenu wakuu niondokane na hii hali .
 
Kafunge uzazi ,wanaume wanafunga pia vasectomy utakuwa Na amani
 
Wakuu msaada wenu tafadhari nimekuwa muoga sana wa hii kitu na kila nikiona mwanamke ana mimba taswira ya kifo naiona kabisa juu yake,

Nifanyaje ili niondokane na hii hali?
 
Sheria za kitabibu (hypocrates oath) na sheria za uuguzi (kwa mujibu wa frolence nightingale) ,
Mtumishi yeyote wa afya haruhusiwi kutoa siri za wagonjwa(yale ayaonayo n kuyasikia wakati wa kutoa huduma au matibabu ya mgonjwa),
Mume wa mama mjamzito haruhusiwi kuingia katika chumba cha kujifungulia (delivery) room,

Nimesikitika sana kuona unakosa maadii kijana hapa jukwaani hili ni kosa kisheria pia ni uzalilishaji wa wanawake na kada nzima ya afya,

MODS FUTENI HUU UZI UNAWEZA KULETA MADHARA MAKIBWA.
 
Wakuu msaada wenu tafadhari nimekuwa muoga sana wa hii kitu na kila nikiona mwanamke ana mimba taswira ya kifo naiona kabisa juu yake,

Nifanyaje ili niondokane na hii hali?
lakin ss wanawake hyo taswira inakuja tu pale kwenye uchungu basi tukishashusha tunasahau kabisa ,, Mungu kwa hilo n moja ya maajabu yake kwetu ,,yan ile siku unataman kurudisha siku nyuma ,,unaapa na kuapa sitakaa nirudie tena ,, kaburi huwa tunalichungulia laki sasa tukisha zaa tu ile furaha tunasahu halaf baada ya muda tunataka kuongeza ..wakat ww ukiwaza kufunga kizaz ikifika mwenzio anahamu na mtt usijeshangaa ana mimba
 
sasa cha kuogopa n nn,

Kama utamuwahisha mapema hospitali na hakuwa na complication wakati wa mimba yake tegemea kupata mtoto na mke,

ila its only logical kama wewe unatafuta kwa jasho na yeye azae kwa uchungu.

usiwe mbahili tu kumhudumia mkeo, na wewe kazi yako n kukoswakoswa na bodaboda/magari wakati ukitafuta mahitaj ya familia
 
Kwanza nilisahau kukupa hongera kwa kupata ongezeko katika familia...
Na maumivu yote anayopitia mwanamke pale atakapomuona mwanae tu, anasahau kila kitu. Mtoto akifika umri fulani yeye mwenyewe atakuomba mtafute mwingine. Nadhani hua wanamisi kulea vitoto vichanga sijui!!!
 
lakin ss wanawake hyo taswira inakuja tu pale kwenye uchungu basi tukishashusha tunasahau kabisa ,, Mungu kwa hilo n moja ya maajabu yake kwetu ,,yan ile siku unataman kurudisha siku nyuma ,,unaapa na kuapa sitakaa nirudie tena ,, kaburi huwa tunalichungulia laki sasa tukisha zaa tu ile furaha tunasahu halaf baada ya muda tunataka kuongeza ..wakat ww ukiwaza kufunga kizaz ikifika mwenzio anahamu na mtt usijeshangaa ana mimba
Duh!

Ila ndivyo inavyokuwaga mwenye tatizo huwa hajionei huruma bali watu wake wa karibu hususani mpenzi ndio hupata mfadhaiko mkubwa.
 
Back
Top Bottom