Kwa nilichokishuhudia VETA, nashauri mfumo wa elimu ufanyiwe marekebisho makubwa level ya sekondari

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,532
44,644
Watu Wengi wamechoka Sana baada ya kumaliza Chuo na kukosa ajira na Wengi hawana ujuzi wowote wanajuta kwanini wasingepitia hata veta toka siku nyingi.

Pia wako vijana waliomaliza form four wamefeli Serikali imeanza vizuri Sana kuhakikisha wanapewa ujuzi.

Serikali tunaomba Sana mbadilishe mfumo huu wa elimu.baadhi ya secondary zinadilishwe ziwe vyuo vya Ufundi stadi.kila kata kiwepo kituo Cha angalau karakana moja aidha mashine kubwa au taasisi za Serikali zinazodili na uzalishaji kwa mashine itasaidia watoto wa mitaa husika kujifunza Ufundi Zaidi.

Tunapoteza watu wazuri kwa sababu mifumo haijawekwa sawa sioni faida ya form five na form six kwa karne Kama ya Sasa.
 
Kwani kujenga vyo vya ufundi ni shilingi ngapi?
Tunafeli wapi kujenga vyo vipya vya ufundi vilivyo vizuri.
tuache kukimbilia kusoma madegree yasio na maana wala tija.
 
Wasomi wapo wengi sana ni wakati wa Serikali kudeal na pia kuwekeza kwenye fani ambazo huitaji kuajiriwa .. unaweza kufanya mwenyewe mfano ufundi tuboreshe Veta na vyuo vya ufundi ikibidi hata tutoe na mikopo kuwa shawishi watu kwenda kusomea ufundi huyu fundi ni vyepesi kukulipa mkopo kwa maana akimaliza tu anaweza kujiajiri na kuanza kutengeneza pesa kuliko huyu uhasibu, Doctor, Engineer ambae mpk apate ajira ambazo hazipo.

Kipindi tunaitaji wasomi tuliwekeza nguvu kubwa mpaka kila mtanzania akaamini degree ndo kila kitu hii ikapelekea kupatikana mpk Degree za Chupi na watu kuanza kufoji vyeti imefikia hatua tofauti ya msomi na darasa la saba kuwa ni cheti tu.

Hatuwezi kuendelea kwa kutengeneza taifa la white collar jobs sasa ni wakati wa kutengeneza blue collar jobs pia kudhibiti idadi ya wanaoenda vyuo waende wale wenye sifa kweli kweli mfano hata kwa mwaka tukizalisha wasomi laki 2 mwenye weledi inatosha kuliko kuzalisha wasomi laki 8 ambao hawana tija zaidi ya mavyeti tu swala la ajira lingepungua sana

Waende vyuo wachache wengi waende Veta na vyuo vya ufundi na wapate mikopo kabisa kama hawa wanaoenda vyuo

Mfano mdogo tu Ufundi wa simu kwa maana ya hardware na software Tanzania

Watumiaji wa simu za mkononi ni milioni 40 na watumiaji wa internet ni milioni 23 kwa maana ya smartphone .. hapa tu kwenye ufundi simu nina hakika tungezalisha ajira nying sana na tungepata walipaji wa mikopo HESLB wengi tu kuliko kumkopesha mtu ambae hajui akimaliza chuo kazi anapata wapi .
 
Tatizo sio kuondoa form five na six wengi hseaelewi kuwa kusoma ni uwekezaji kama ulivyo uwekezaji mwingine .Unadsoma ili iwe nini mwisho? mfano mhindi akiwa na biashara mfano hospitali anapeleka mtoto kusoma PCB aje kuwa doctor hospitali yake au anayotarajia kuwekeza au anampeleka kusoma business administaration aje kuendeshabiashara ya familia au anayotarajia kuanzisha au kumwanzishia

Nini usome unatakiwa ku discuss na wazazi pia kueleza your future plans and their expectations and yours for your education si vizuri kusoma kama mwehu tu

mitoto mingi miswahili hai discuss na wazazi linajijazia tu kama bwege ohh nimeamua nisome hiki.
 
Watu Wengi wamechoka Sana baada ya kumaliza Chuo na kukosa ajira na Wengi hawana ujuzi wowote wanajuta kwanini wasingepitia hata veta toka siku nyingi....

..wazo lako ni zuri sana. Naliunga mkono kwa 200%.

..ila nashauri TUSIKURUPUKE ktk utekelezaji wa mapendekezo yako.

..this time tuangalie sana suala QUALITY badala ya quantity.

..tusiingize kabisa SIASA ktk uanzishwaji wa vyuo vya Veta na utoaji wa elimu ya ufundi.

..tuweke umakini mkubwa kwa kuanzisha idadi ya vyuo ambavyo tutavimudu kwa kuvipatia wakufunzi, miundombinu, na vifaa vyote vinavyohitajika ili kutuwezesha kutoa wahitimu waliowiva.

..zaidi napendekeza vyuo hivyo visambazwe nchi nzima kwa uwiano mzuri, hatua kwa hatua, bila upendeleo.

..Again, tulikosea kwenye mpango wa upe, tukakosea kwenye sekondari za kata, tukakosea kwenye elimu bure, naomba kwenye hili la uanzishwaji wa vyuo vya ufundi tufanye kitu sahihi.
 
Mkuu naona umechukua cheti chako cha VETA, hongera sn lakini ni hatua nzuri kuliko ungebaki na zero yako bila cheti
Hold kwanza hongera watu wanasomea ufundi wakijua wanaenda wapi mfano wanasoma kupika veta wakaange vitumbua u maandazi etc wauze kwenye hotel na restaurant mimi nina ndugu yangu kasoma Veta na nilimlipia usiku kucha hupika vitumbua na maandazi ana tenda huuza mahoteli ya kitalii ya kupeleka vitumbua na maandazi elfu moja vitumbua na elfu moja maandaza huwa anawauzia kwa mia tano wao wanauza zaidi ya elfu moja
 
Kwahiyo kukaa vitumbua kuna hitaji elimu ya VETA? pole sn
 
Watu Wengi wamechoka Sana baada ya kumaliza Chuo na kukosa ajira na Wengi hawana ujuzi wowote wanajuta kwanini wasingepitia hata veta toka siku nyingi...
Anza kwa kutowapeleka wanao secondary schools
badala yake wapeleke vyuo vya ufundi stadi.

Elimu ya sekondari ni kwa ajili ya kumuandaa kinadharia mtoto aweze kusoma high school na hatimaye chuo kikuu dunia nzima. vilevile kumuwezesha kusomea kazi mbali mbali ngazi ya kati ikiwemo ufundi mchundo ambao ni levo ya juu kidogo kuliko VETA.

Idadi ya vyuo vya VETA vilivyopo vinatosha sana kukidhi mahitaji ya nchi, Kuna maelfu ya waliosoma huko VETA hawana ajira na hawawezi kujiajiri kwa kiwango cha kutosha kwa sababu economy of scale katika taaluma waliisomea hairuhusu kila mhitimu kuanzisha biashara hiyo hiyo katika maeneo waliyopo kwa lugha rahisi hakuna wateja wa kutosha. Pia katika fani hiyo hiyo ya VETA kuna waliosomea vyuo vya technical college, na wengine university (mainjnia) wote hao wanalitazama soko hilo hilo. Tatu kila fani ina Bodi ambayo licha ya kusimamia maadili ya taaluma husika lakini kichinichini inatengeneza restrictions kuzuia wahitimu wengi wa fani husika wasiweze kuruhusiwa kufanya kazi kwa kuweka mazingira magumu ya usajili ambayo mara nyingi yanataka mtu mwenye degree ndiyo afanye kazi kubwa kubwa katika fani hiyo ya ufundi. Wahitimu wa VETA na vyuo vingine vya chini huzuiwa kusajiliwa hivyo hawawezi kufanya kazi kubwa vinginevyo ukubali kunyonywa kwa kufanya kazi hiyo kwa kutumia leseni ya mtu aliyesajiliwa na wewe kumlipa kwa kutumia jina lake.

Fuatilia vizuri wengi waliosomea vyuo vya VETA wanafanya shughuli zingine hususan bodaboda, mama/baba ntilie, umachinga na umalaya (sidharau kazi hizi). Hivyo hata kama vyuo lukuki vya ufundi vitajengwa ili kila familia iwe na mtoto aliyesoma huo ufundi bado tatizo la ajira litakuwa kubwa kwa sababu mwisho wa siku wengi wao hawataweza kufanya hicho walichosomea

Mkakati wa kupunguza tatizo la ajira hautaki unafiki, kuna mambo ya kufanywa katika short term na katika long term. Kilimo bado kina nafasi kubwa ya kupunguza tatizo la ajira lakini kama tutaacha wimbi ka kunyang"anya ardhi wananchi na kuwapa wanaoitwa wawekezaji.
 
Kwahiyo kukaa vitumbua kuna hitaji elimu ya VETA? pole sn
Ndio Veta hawafundishi tu kupika lakini kupika classic unakoweza kupata international certification
Chips kuku hata uswahilini wanaweza lakini Tanzania wameletwa wawekezaji wa Steers nk wanapika kuku chips kwa kiwango cha kimataifa.Mtu akivaa suti hawezi kula chips kuku uswahilini yuko tayari alipe elfu 20 kula chips paja steers kuliko uswahilini kwenye chips kuku elfu tatu mia tano

Hushangai kwa nini serikali ilete mwekezaji toka nje kuja kupika chips kuku?
 
Kwahiyo kukaa vitumbua kuna hitaji elimu ya VETA? pole sn
Hujui kitu kuna baba nitilie anaitwa AKO group search ana hadi website anapika vyakula Tanzania kwenye makampuni makubwa zaidi ya 45 na ni baba nitilie intenationally certified ana ISO ya quality assuarance ya kimataifa kuwa akikupa chajula kiko certified kiwe kitumbua or whatever .Issue sio tu kupika una cheti cha upishi kulisha public ukizingatia public health?
 
Ndio Veta hawafundishi tu kupika lakini kupika classic unakoweza kupata international certification
Chips kuku hata uswahilini wanaweza lakini Tanzania wameletwa wawekezaji wa Steers nk wanapika kuku chips kwa kiwango cha kimataifa.Mtu akivaa suti hawezi kula chips kuku uswahilini yuko tayari alipe elfu 20 kula chips paja steers kuliko uswahilini kwenye chips kuku elfu tatu mia tano

Hushangai kwa nini serikali ilete mwekezaji toka nje kuja kupika chips kuku?
Serikali hii hii ya hovyo nayo ni ya kuamini kitu
 
Kwahiyo kukaa vitumbua kuna hitaji elimu ya VETA? pole sn
kama unapika chakula kwa ajili yako na hawara yako haina shida pika lajini kulisha public unahitaji vyeti na certification kuwa unajua sheria pia za publuc heath na sheria zake pia kuwa ukichemka watu wakaugua kipindupindu utakoma.Tofautisha kujipikia chakula chako nyumbani na kulisha public
 
Hujui kitu kuna baba nitilie anaitwa AKO group search ana hadi website anapika vyakula Tanzania kwenye makampuni makubwa zaidi ya 45 na ni baba nitilie intenationally certified ana ISO ya quality assuarance ya kimataifa kuwa akikupa chajula kiko certified kiwe kitumbua or whatwver .Issue sio tu kupika
Watu wamesoma VETA kibao lakini wapo kitaa hana issue, tatizo la elimu ya Tanzania ni hizi field za mwezi mmoja badala ya mtu kukaa field kuanzia semester ya pili mwaka wa kwanza mpaka semester ya kwanza mwaka wa mwisho uone matokeo yake
 
kama unapika chakula kwa ajili yako na hawara yako haina shida pika lajini kulisha public unahitaji vyeti na certification kuwa unajua sheria pia za publuc heath na sheria zake pia kuwa ukichemka watu wakaugua kipindupindu utakoma.Tofautisha kujipikia chakula chako nyumbani na kulisha public
Hizo tenda labda kwenye hoteli za babu yako
 
Hold kwanza hongera watu wanasomea ufundi wakijua wanaenda wapi mfano wanasoma kupika veta wakaange vitumbua u maandazi etc wauze kwenye hotel na restaurant mimi nina ndugu yangu kasoma Veta na nilimlipia usiku kucha hupika vitumbua na maandazi ana tenda huuza mahoteli ya kitalii ya kupeleka vitumbua na maandazi elfu moja vitumbua na elfu moja maandaza huwa anawauzia kwa mia tano wao wanauza zaidi ya elfu moja
Duuh! Unasema ulimlipia kusoma kupika vitumbua na maandazi?
 
Watu Wengi wamechoka Sana baada ya kumaliza Chuo na kukosa ajira na Wengi hawana ujuzi wowote wanajuta kwanini wasingepitia hata veta toka siku nyingi.

Pia wako vijana waliomaliza form four wamefeli Serikali imeanza vizuri Sana kuhakikisha wanapewa ujuzi.

Serikali tunaomba Sana mbadilishe mfumo huu wa elimu.baadhi ya secondary zinadilishwe ziwe vyuo vya Ufundi stadi.kila kata kiwepo kituo Cha angalau karakana moja aidha mashine kubwa au taasisi za Serikali zinazodili na uzalishaji kwa mashine itasaidia watoto wa mitaa husika kujifunza Ufundi Zaidi.

Tunapoteza watu wazuri kwa sababu mifumo haijawekwa sawa sioni faida ya form five na form six kwa karne Kama ya Sasa.

Nimeona mijadala mingi kuhusu katiba ya nchi yetu ila cha kustaajabisha ni kwamba wananchi wengi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania hawaijui katiba yao na wengine ata kuwa nayo hawana, sio soft copy wala hard copy.

Ningependa kushauri wadau wa taaluma/elimu nchini na wizara husika ya elimu kueka elimu ya katiba kwenye masomo ya civics kwa O-level au vile wao wataona inafaa ili wananchi wapate kujua kilichoandikwa na kukielewa.

Tatizo linalojitokeza mbali na kutofundishwa kwa katiba yetu mashuleni, wananchi hawajajengewa hulka au tabia ya kujisomea vitabu mbalimbali, hivyo muamko wa wananchi kuitafuta katiba hiyo na kusoma unakuwa mdogo. Hali hii hupelekea watu kutoijua katiba yao hata kidogo na kutojua haki zao za kikatiba na kubaki kutengeza matatizo katika nchi. Mbali na hapo uzalendo hukosekana pia sio kwa makusudi lakini ni kutokana na mitaala yetu kutokidhi matwakwa kabisa. Hivyo mbali na kuomba taasisi husika na wadau kuekea mkazo suala la katiba kufundishwa mashuleni, waeke mkazo pia kwenye uwekezaji wa usomaji wa vitabu maana vitu viwili hivi ni muhimu kwa taifa letu.

Pia wizara ya elimu wafanyie kazi maagizo ya rais ilikuwa na mitaala yenye kujenga tija ya wanataaluma wetu. Elimu ya 5 na 6 haina mantiki tena na kutengeza matatizo mbalimbali ya watu kuwa na theoretical knowledge while lacking practical knowledge. Naona kama wanafunzi wajinga na diploma wakitoka o-level moja kwa moja kama nchi za wenzetu na ata ya ujirani, kenya zinavyofanya.

Wengi wetu hatujaajengewa hulka ya kusoma vitabu hali ambayo husababisha watu wengi kupoteza uwezo wa kusoma vitabu, na pia huchangia secta nyengine kudorora kama vile biashara ya magazetu sababu hanna wasomaji magazeti JMT, uandishi uchapishaji na uuzwaji wa vitabu, secta ya filamu na secta ya muziki. Mbali na hapo waandishi wa vitabu pia huadimika au kukosekana kabisa nchini kwani wanataaluma wetu hawafundishi kuhus uandishi wa kusoma vitabu.

Uandishi huo pia huzorotesha secta ya filamu na mziki nchini kwani secta hizo hutegemea sana uandishi bora wa tenzi na tamhilia na narratives zake, yani zile dialogue za kwenye tamthilia huwa hazina mvuto ata. Siwezi fafanua zaidi kwenye tamthilia mana sio mbobezi wa hiyo secta. Na tenzi za muziki wetu sio nzuri yani ni kupayuka tu na tenzi za ngono mana hawana chengine cha kuimba.

Naeka mkazo kwenye masomo mawili Kiswahili na English, yani masomo ya lugha ndo hutumika kujengea watu wetu uwezo wa kusoma na uandishi. Mfano toka form 1 usomaji wa vitabu,, na uchanganuzi (literature) ndo upewe kipaumbele pamoja na uandishi na sio kuanza form 3 au form 4. Wengi wa wanafunzi hawasomi hivo vitabu wakiwa form 3 au form 4 sababu walimu huwaandaa na mitihani ya taifa ya form 4 kwa kutumia summary zilizoandaliwa kutokana na mitihani iliyotangulia na huu ndo uhalisia wa mambo.

Mitaala hiyo iache kujikita na kufundisha vitenzi na nomino mana primary kwa miaka saba wanafunzi wanafundishwa hivo vitu. Elimu inatakiwa iwe endelevu ma sio repetition ya vitu inakuwa haileti mantiki. Hivyo basi vitu hivyo ambavyo vilifundishwa primary vikumbushikwe kwenye upembuzzi nadhani (literature) pamoja na ujuzi mwengine. Hii itajengea uwezo watu wetu wa kusoma ,kuandika,kuchambua na pia kuweza kuuza secta ya biashara ya magazeti pamoja na uandishi, uchapishaji na uuzaji wa vitabu mbali mbali na kutengeneza ajira kwa vijana wetu. Yani Ajira za uandishi na uchapishaji mana nchi za wenzetu zinafaidika sana na secta hiyo ya vitabu na magazeti kwa ujumla wake.

Pia napendekeza jina la nchi yetu lisikatishe maana watu wanakupa wagumu kuelewa huko baadae kuwa nchi ni Tanzania au ni Jamhuri ya muungano wa Tanzania, hivyo litumike lote kwenye kila kitu na itambulike kwa watu wote kuwa jina la nchi hii no JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
 
Back
Top Bottom