Kwa nilichokiona na kukisikia leo nathibitisha rasmi kuwa Tanzania hatuna 'Critical Journalists' bali tuna 'PR and Round Table Journalists' tu

Ukiona anayehojiwa au Kuulizwa Maswali anayajibu kwa Furaha, hatetemeki, anatingisha Miguu yake kama yupo Sebuleni Kwake na Familia yake, hatokwi na Jasho, hapandwi na Hasira mpaka anadiriki kuomba maswali ya Nyongeza huku akiishia Kuwakaribisha Chakula ili mvimbiwe vizuri kwa Uroho wenu jua waliopo ( wanaomuhoji ) ni bure kabisa na anayehojiwa nae ameshawadharau halafu anawamudu pia hawamtishi.

Nimesikitika sana tu kwa nilichokiona.
Mkuu mbona hili linajukana kabisa!! Halafu mkutano ulivyoandaliwa siyo kwa kitaalam kabisa. Mkutano kama huu unakuwa na follow up questions, na rais angejibu eg maswali matatu, matatu. Hili la kuuliza maswali yote kwa pamoja halafu rais ndiyo ajibu kuna kitu kinakwepwa. Kuhusu hili la ''waandishi'' wa Tanzania hilo wala lisikusumbue. Wenyewe walikwenda kulilia maslahi yao na kusifu ili wafikiriwe kwenye safari za nje. Kama huyo sijui Balile, huyo jamaa anachojua ni tumbo lake tu.
 
Ukiona anayehojiwa au Kuulizwa Maswali anayajibu kwa Furaha, hatetemeki, anatingisha Miguu yake kama yupo Sebuleni Kwake na Familia yake, hatokwi na Jasho, hapandwi na Hasira mpaka anadiriki kuomba maswali ya Nyongeza huku akiishia Kuwakaribisha Chakula ili mvimbiwe vizuri kwa Uroho wenu jua waliopo ( wanaomuhoji ) ni bure kabisa na anayehojiwa nae ameshawadharau halafu anawamudu pia hawamtishi.

Nimesikitika sana tu kwa nilichokiona.
Wote wanavizia uteuzi, njaa kitu mbaya
 
Ungekuwepo ungeuliza nini?

Sent from my TECNO-C9 using JamiiForums mobile app
Ningeuliza hivi:
Tangu awamu ya sita imeingia madarakani chini ya uongozi wako, tumeshuhudia ukisisitiza juu ya umuhimu wa kuchukua hatua juu ya ugonjwa wa COVID, na hata hapa leo umetuambia juu ya hilo na uwepo wa wagonjwa wa COVID nchini na mipango ya serikali kuleta chanjo. Pia, umekuwa ukisisitiza Watanzania kuchukua hatua za kujilinda ikiwemo kupunguza misongamano isiyo ya lazima. Lakini, hivi karibuni tumeshuhudia ukimpigia simu mwanamuziki aliekua anatumbuiza usiku kwenye tamasha la muziki, na ukisema unatamani ungekwepo pale huku ukipongeza tamasha hilo. Je, kwa kitendo hicho huoni kuwa unachanganya wananchi kama kiongozi namba moja wa Serikali?
Au unadhani kuwa tamasha lile na matamasha ya aina ile ni moja ya misongamano muhimu isiyokwepeka?Huoni kama kwa hatua ile ume-endorse muendelezo wa mikusanyiko ya muziki katika kipindi hiki ambacho unatusisitiza tuepuke misongamano isiyo ya lazima?
Kipi ni kipi?
 
UNGEKUWA WEWE UNGEULIZA NINI CRITICALLY .....TUSAIDIE....naona huna hoja sema mimi ningeuliza 1,2,3,4...etc
 
Ukiona anayehojiwa au Kuulizwa Maswali anayajibu kwa Furaha, hatetemeki, anatingisha Miguu yake kama yupo Sebuleni Kwake na Familia yake, hatokwi na Jasho, hapandwi na Hasira mpaka anadiriki kuomba maswali ya Nyongeza huku akiishia Kuwakaribisha Chakula ili mvimbiwe vizuri kwa Uroho wenu jua waliopo ( wanaomuhoji ) ni bure kabisa na anayehojiwa nae ameshawadharau halafu anawamudu pia hawamtishi.

Nimesikitika sana tu kwa nilichokiona.
watu wanalinda maslahi, huwezi ona Hawa watu ikipita leo na kesho wataanza kujadili mambo mengineyo kadha wa kadha wakati leo wamepata nafasi Ila wakajiona Kama wapo primary ndo wanajifunza jinsi ya kuuliza maswali
 
Waandishi unawaonea tu,

Tanzania hatuna hata Maprofesa,

Yaani hakuna profesa Tanzania nzima aliyegundua namna Bora na ya haraka ya kupika Ugali tu.

Huko Kigoma unaambiwa Kuna Ugali unapikwa Kwa siku saba.
 
Ningeuliza hivi:
Tangu awamu ya sita imeingia madarakani chini ya uongozi wako, tumeshuhudia ukisisitiza juu ya umuhimu wa kuchukua hatua juu ya ugonjwa wa COVID, na hata hapa leo umetuambia juu ya hilo na uwepo wa wagonjwa wa COVID nchini na mipango ya serikali kuleta chanjo. Pia, umekuwa ukisisitiza Watanzania kuchukua hatua za kujilinda ikiwemo kupunguza misongamano isiyo ya lazima. Lakini, hivi karibuni tumeshuhudia ukimpigia simu mwanamuziki aliekua anatumbuiza usiku kwenye tamasha la muziki, na ukisema unatamani ungekwepo pale huku ukipongeza tamasha hilo. Je, kwa kitendo hichi huoni kuwa unachanganya wananchi kama kiongozi namba moja wa Serikali?
Au unadhani kuwa tamasha lile na matamasha ya aina ile ni moja ya misongamano muhimu isiyokwepeka?Huoni kama kwa hatua ile ume-endorse muendelezo wa mikusanyiko ya muziki katika kipindi hiki ambacho unatusisitiza tuepuke misongamano isiyo ya lazima?
Kipi ni kipi?
Swali la pili ambalo ningeuliza:
Pia, tangu umeingia madarakani umekua ukisisitiza suluhu na maelewano kati ya makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoa haki kwa makundi yote ya Watanzania. Moja ya haki ya msingi kabisa kwa Watanzania, ambayo ni haki ya kikatiba ni demokrasia ikiwa ni pamoja na kushiriki shughuli za kisiasa za vyama vyao vya siasa, na wanasiasa wa vyama vyote kufanya mikutano ya hadhara na shughuli za kisiasa kwa kadri ya sheria za nchi. Je, tamko lako la kuzuia mihadhara ya kisiasa kwa sasa huoni kuwa linavunja haki ya msingi ya kikatiba kwa wananchi wa Tanzania?
Je, haki ya wananchi na wanasiasa kushiriki na kufanya mikutano ya kisiasa ni takwa la kisheria au ni takwa la rais aliye madarakani?
 
Usifkiri hawana uwezo wa kuuliza..ukute itikadi inabana...hivo lazima waende taratibu..ingawa mama yetu hana noma kabisa...na asiyempenda huyo ni mchawi..
 
Back
Top Bottom