Kwa nguvu hii ya CHADEMA, Mwalimu Nyerere leo angekuwa HAI, angeendelea kukumbatia KADI ya CCM?

Mie binafsi nashindwa kuelewa ,
Ikiwa nyerere alijenga viwanda enzi zile za umasikini
Inakuwaje vinakufa leo wakati wasomi ni wengi na tuna utajiri mkubwa?
Hapo ndipo kila mtu anahitaji jibu makini, lakini wakujibu wapo bize na dili kharamu
 
siku hizi
JEMBE = kuchimba kaburi
NYUNDO = kutengeneza jeneza

Enzi za mwl mauaji ya raia yalitokea usukumani mzee ruksa aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani wa wakati huo aliiachia ofisi bila kuchelewa. Hivi sasa hali ni tofauti kabisa, wanaotakiwa kujiuzulu eti ndo wanaounda tume/kamati za kuchunguza mauaji.
 
sidhani kama nyerere angeendelea kukumbatia kadi ya hiki chama...angekaa pembeni kama walivyokaa pembeni viongozi waadilifu wa enzi hizo
 
Enzi za mwl mauaji ya raia yalitokea usukumani mzee ruksa aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani wa wakati huo aliiachia ofisi bila kuchelewa. Hivi sasa hali ni tofauti kabisa, wanaotakiwa kujiuzulu eti ndo wanaounda tume/kamati za kuchunguza mauaji.
Daaah inauma sana mkuu, yaani kama nakuona vile unavyokerwa na hali ya mambo ya nchi hii
 
Mie binafsi nashindwa kuelewa ,
Ikiwa nyerere alijenga viwanda enzi zile za umasikini
Inakuwaje vinakufa leo wakati wasomi ni wengi na tuna utajiri mkubwa?

siyo viwanda tu bali ni sekta zote
1. Elimu - Nyerere alijenga vyuo vya kila taaluma - maji, umeme, usafirishaji, kilimo, ualimu, uhasibu, biashara, misitu, nyuki, uvuvi, sanaa, ufundi nk . Hata ilipokuja mwamko wa kuwa na vyuo vikuuu wahuni hawakupata shida, kazi yao ilikuwa ni kuvibadilisha majina tu.
2. Usafiri - wakati wa mwl kila mkoa ulikuwa na kampuni ya usafirishaji wa mizigo na abiria, alijenga reli ya tazara, reli ya kati na tanga zilikuwa hai, wahuni wanachofanya hivi sasa badala ya kujenga reli mpya kusafirisha wakazi wa da slam wanatumia tu miundo mbinu ya mwl kama walivyofanya kwenye mavyuo.
3. Kilimo - Sio tu alisema kilimo ni uti wa mgongo bali alitekeleza kwa vitendo kwa kujenga chuo kikuu cha kilimo cha sokoinne pamoja na vyuo vingi vya diploma na certificate plus kiwanda cha kutengenezea zana za kilimo
4. Uongozi - kosa la uhaini adhabu yake ni kifo, mwl alipona majaribio ya kupinduliwa kwa kutumia nguvu mara kadhaa, lakini hakuna mhaini aliyeuawa, wote tunajua siasa za kiafrika zilikuwa ni kuua wapinzani wa aina yoyote, lakini mwl hakuua si wapinzani wa kawaida tu bali hata wahaini!!!! marais wa kiafrika akina mzee jomo kenyatta, iddi amini, mobutu sese seko, kamuzu banda, bokassa nk sera zao zilikuwa ni kuua wapinzani wa aina yoyote ile, cha ajabu miaka 27 baada ya mwl, watawala sasa wanaua wale wasiokubaliana na hoja zao
 
Mkuu Mrdash1 umefafanua vema kabisa, nadhani kama taifa huru, tunatakiwa kukaa na kutafakari wapi hasa tumeyumba na kuanguka kiasi hiki.
 
Kama sikosei mtazamo na msimamo wa Nyerere, mpaka anaaga dunia, ulikuwa ni kwamba kiongozi bora wa nchi hii Lazima atoke CCM pamoja na kukiri wazi kuwa CCM ilikuwa inanuka Rushwa.
 
Mkuu Tata, pamoja na hiyo kauli ya Mwalimu, unaamini kabisa kuwa angeendelea kuwepo ccm kweli? Nini kingembakisha huko zaidi?
 
Mkuu nadhani maovu na mabaya ya ccm ndo yangemfanya kuihama ccm na si nguv ya m4c
 
Kwani watu walijiunga CCM kwa sababu ya Nyerere? watanzania tusiwe mazuzu Nyerere hakuwa nabii, ni kumkufuru mungu kuona kila jambo Nyerere alilofanya alikuwa sahihi au aangeweza kulipatia ufumbuzi.Mwenyewe katika hotuba yake alishawahi kusema katika kipindi cha utawala wake kuna mambo ya msingi na ya kijinga aliyafanya.Labda kujiunga CDM ingekuwa sehemu ya mambo ya kijinga kuyafanya.
 
Alikuwa mwanamapinduzi hivyo angekuwa upande wa jeshi la ukombozi. Ishu ni ktk capacity gani, labda.
 
Kwani watu walijiunga CCM kwa sababu ya Nyerere? watanzania tusiwe mazuzu Nyerere hakuwa nabii, ni kumkufuru mungu kuona kila jambo Nyerere alilofanya alikuwa sahihi au aangeweza kulipatia ufumbuzi.Mwenyewe katika hotuba yake alishawahi kusema katika kipindi cha utawala wake kuna mambo ya msingi na ya kijinga aliyafanya.Labda kujiunga CDM ingekuwa sehemu ya mambo ya kijinga kuyafanya.

Rafiki, Nyerere alikuwa maarufu kuliko CCM. Ndio maana mpaka leo ktk baadhi ya vijiji kuna wananchi wanadhani Mwl. bado ni Rais. Nondo ya pili ni kumbuka jinsi alivyomnadi Mkapa 1995, CCM haikuwa na ubavu wa kumshinda Mrema (controversy) ila Mwl. akaweka uzito sio tu kuhakikisha kijana wake anapita ndani ya CCM bali hata kwa wananchi.

Of coz Mwl hakuwa sahihi ktk kila kitu, hata yeye mara nyingi alisema na kukiri hivyo.
 
Back
Top Bottom