Kwa nguvu hii ya CHADEMA, Mwalimu Nyerere leo angekuwa HAI, angeendelea kukumbatia KADI ya CCM? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nguvu hii ya CHADEMA, Mwalimu Nyerere leo angekuwa HAI, angeendelea kukumbatia KADI ya CCM?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Yericko Nyerere, Sep 8, 2012.

 1. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #1
  Sep 8, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,249
  Likes Received: 3,836
  Trophy Points: 280
  Nguvu ya mabadiliko inayoongozwa na chama kilicho moyoni mwa wazalendo wa kweli wa nchi hii inanipa hofu kuamini kama mzee wangu Mwalimu Julius K. Nyerere LEO hii angekuwa hai angeendelea kumiliki kadi ya kisiasa ya kijani yenye alama ya JEMBE na NYUNDO.

  Alama hizo muhimu katika historia na siasa za nchi hii, zilikuwa ni uashirio wa mambo makuu mawili, JEMBE= Mkulima, NYUNDO=Mfanyakazi. Lakini leo ni kinyume kabisa tena kabisa, JEMBE = Vyombo vya Dola, NYUNDO = Risasi/mabomu.

  Hali ya kisiasa ndani ya ccm imekuwa ya mikingamo, huku wimbi la ufisadi nchini likishamiri kila uchao, hata wale wahafidhina wa chama wamegeuka kuwa wakwasi wa chama hiki mufilisi. Sasa hivi dhana ya kuitwa chama cha siasa imetoweka na sasa kinajieleza bila kuuliza kuwa ni GENGE la walanguzi wa raslimali za umma.

  Kupitia chama hiki, watu wanafanya jambo lolote watakalo, hata wakiitaka roho yako leo hii wanapata tu. Wameweza kupakia twiga kwenye ndege, wameweza kuza madini, wamehongwa suti, wamehonga vyeo nyumba ndogo, wamejiuzia migodi, wamejipa tenda.

  Yani ukiwa ccm hakuna unalolishindwa, wanafikiria kama kuna japo hata uwezekano wa kuitoa roho ya Mtume s.w au Yesu Kristu ilimradi kuondoa dhana ya dhambi kwako.

  Nikiangalia utawala wa Mwalimu Nyerere najiona mimi nimkosaji mkubwa ninaestahili adhabu mbele ya ghadhabu ya mungu, kwanini haya yanatokea huku watanzania tukiacha hawa mumiani waendelee kuliangamiza taifa?

  Rais wa kwanza Mwl. Nyerere pamoja na kutokuwepo rasilimali nyingi wakati huo alijenga kiwanda karibia kila mkoa. Alijenga nyumba za serikali ambazo wezi Mkapa na Magufuli wamekuja kuuza, alijenga bandari Dar, Tanga, Mtwara, Mwanza, ALIONGOZA SERIKALI YENYE NIDHAMU AMBAYO RUSHWA ILIKUWA NI MWIKO. Alileta umoja wa kitaifa kwa kuongoza serikali bila kujali dini wala. Wakati wake elimu ilikuwa inatolewa bure tena kwa ubora wa hali ya juu. Wakati wake shule zilikuwa na vifaa na waalimu. Wakati wa Kikwete elimu katika shule za msingi na sekondari imekuwa na mzaha tu. Si hayo tu bali mwalimu alijenga nidhamu ya chama, kiasi kwamba kila mtanzania alijivunia kuitwa mwanaccm.

  Ikumbukwe kuwa enzi hizo taifa lilikuwa likitegemea pamba, mkonge na tumbaku tu kujipatia fedha za kigeni, lakini kwa hekima za viongozi wa enzi hizo chini ya Mwalimu, waliwahudumia watanzia bila mawaa.

  Hivi leo mwalimu angekuwepo, angeendelea kukumbatia kadi ya ccm?
   
 2. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #2
  Sep 8, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  "Nimeangalia huku na kule......chama ambacho kinaweza kushika dola ni chadema"
   
 3. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #3
  Sep 8, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Angekuwa ameshahama ccm kwa sababu cc
  m si Baba yake wala si mama yake.
   
 4. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #4
  Sep 8, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,249
  Likes Received: 3,836
  Trophy Points: 280
  Heheee saaaaafiiiiii sana, naikumbuka vema kauli hiyo ya mtakatifu Jk Nyerere
   
 5. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #5
  Sep 8, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Wewe ndio unayejua sababu mzee wako.
   
 6. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #6
  Sep 8, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Mkuu Nyerere ni mtakatifu?
   
 7. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #7
  Sep 8, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,249
  Likes Received: 3,836
  Trophy Points: 280
  Mkuu Rirtz, hapa hazungumziwi kama mzazi wangu, bali anazungumziwa kama mwanasiasa na kiongozi mashuhuri wa watanzania
   
 8. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #8
  Sep 8, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mwenye heri.
   
 9. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #9
  Sep 8, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Nimekupata mkuu...mjadala mwema takuwa msomaji tu.
   
 10. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #10
  Sep 8, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  siku hizi
  JEMBE = kuchimba kaburi
  NYUNDO = kutengeneza jeneza
   
 11. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #11
  Sep 8, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,249
  Likes Received: 3,836
  Trophy Points: 280
  Naubariki mchakato unaoendelea wakumtawaza kuwa MTAKATIFU, kwasasa ni MWENYE HERI
   
 12. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #12
  Sep 8, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,249
  Likes Received: 3,836
  Trophy Points: 280
  Hahaaa itakuwa ajabu wewe usome tu bila kuchangia chochote? basi kumbe sasa magamba karibu unayavua, Pipooooooz ............!
   
 13. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #13
  Sep 8, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,249
  Likes Received: 3,836
  Trophy Points: 280
  Heheee sawasawa kabisa mkuu
   
 14. Chilisosi

  Chilisosi JF-Expert Member

  #14
  Sep 8, 2012
  Joined: Oct 19, 2008
  Messages: 3,055
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Ritz umekua sana siku hizi,
  anaona unajibu hoja kama mtu mzima vile, sio kama zamani ulikuwa unatoka povu
   
 15. Chilisosi

  Chilisosi JF-Expert Member

  #15
  Sep 8, 2012
  Joined: Oct 19, 2008
  Messages: 3,055
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mie binafsi nashindwa kuelewa ,
  Ikiwa nyerere alijenga viwanda enzi zile za umasikini
  Inakuwaje vinakufa leo wakati wasomi ni wengi na tuna utajiri mkubwa?
   
 16. Jakubumba

  Jakubumba JF-Expert Member

  #16
  Sep 8, 2012
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 1,627
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
 17. RGforever

  RGforever JF-Expert Member

  #17
  Sep 8, 2012
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 6,187
  Likes Received: 1,908
  Trophy Points: 280
  Siku hizi MMEPOA KWELI!
   
 18. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #18
  Sep 8, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,249
  Likes Received: 3,836
  Trophy Points: 280
  Asante sana mkuu, unazidi kudhihirisha uthabiti wa mwalimu tofauti na makapi yaliyopo sasa hivi ndani ya ccm
   
 19. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #19
  Sep 8, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,249
  Likes Received: 3,836
  Trophy Points: 280
  Sio kupoa, wameishiwa propaganda huku chama chao kinawaangusha
   
 20. Chilisosi

  Chilisosi JF-Expert Member

  #20
  Sep 9, 2012
  Joined: Oct 19, 2008
  Messages: 3,055
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  umeona eeh!
  jamaa wamekuwa wapole sana wameanza kukubali matokeo kabla ya mechi
   
Loading...