Kwa NEC hii mpya, CCM inakwenda kufa - Dr. Slaa

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Kiongozi wa Upinzani Nchini Na Katibu Mkuu wa chama kikuu cha upinzani nchini-CHADEMA Dr Wilbroad Slaa amesema ameshangazwa na uamuzi wa CCM kupitisha majina ya watuhumia wakuu wa ufisadi nchini kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho ukiwemo ujumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa CCM-NEC.

Kiongozi huyo machachari nchini amesema hayo yote yamefanywa na CCM licha ya kelele za wananchi kote nchini kulaani ufisadi uliofanywa na watu hao na pia CCM kuizika kauli yake ya kujivua Gamba na kuwaondoa watuhumiwa wa ufisadi.

Hata hivyo Dr Slaa amesema hiyo ni furaha kubwa kwake na chama chake kwani kwa hali hiyo CCM imejizika yenyewe kwani wananchi kamwe hawawezi kukubali kuongozwa tena na chama kinachokumbatia ufisadi kwa viwango hivyo.

Source: Nipashe na Tanzania Daima.


 
Anachofanya Dr Slaa ni kuziba shimo la panya kwa mkate wa nyama.
 
Mimi nadhan Slaa amesukumwa na mihemko ya kisiasa tu. CCM na ujambazi , uhuni, ubakaji, udhulumaji na uchafu wao, bado ni MBUYU mzito kuukata. Huo ndio ukweli
 
JK hataki aonekane mbaya kwa akina Lowasa pia anaogopa kuonekana mbaya kwa jamii. Kwa hiyo anachofanya hapa, ni kuwaweka pamoja Nape na akina Lowasa, halafu ampe Ukatibu mkuu Nape ili Nape awashughulikie (japo hii itakuwa ngumu!) Ili isionekane ni yeye ndiye aliyewashughulikia!
 
Yaani kwa sasa ndani ya CCM mtindo ni UFISADI na USULTANI.

Huwezi amini Andrew Chenge, Mama Salma kikwete, Ridhwani Kikwete wamepita bila kupingwa!
 
Firauni hapendi kula uchafu,lakini anakula ndege anaekula uchafu...basi ccm kama firauni wangewezaje kuwafukuza wachafu (mafisadi)
 
Huyu mzee hana sera ingine zaidi ya ufisadi? analia sana.....aseme mengine...hawa ni watuhumiwa sio mafisadi.....tumechoshwa na sera zake za ufisadi ufisadi....
 
Huyu mzee hana sera ingine zaidi ya ufisadi? analia sana.....aseme mengine...hawa ni watuhumiwa sio mafisadi.....tumechoshwa na sera zake za ufisadi ufisadi....

siyo huyo mzee tu ata mimi nauchukia ufisadi kuliko kitu chochote dunia. kwahiyo anachofanya huyo mzee hakosei, ni watanzania wengi sana tunalia kila siku kuhusu ufisadi na hicho ndiyo pekee kitakacho iuwa CCM. wakiiba kura kama kawaida yao tuna wapiga mawe kama vibaka. tumeisha wachoka sana
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom