Kwa ndugu zangu wasambaa na wazigua, Lushoto jamani kuzuri ehhhh

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
Lushoto Kuzuri jamani
Muandishi: Othman Michuzi | Tarehe: Saturday, October 09, 2010

nikitabaruku katika mashamba ya mwenyeji huku Lushoto

benki pekee iliopo katika mji wa Lushoto

hii ndio stendi kuu ya mabasi Lushoto

abiria wakiwa katika daladala zinazopiga ruti za kuingia vijijini,kutokea Lushoto Mjini.

kina mama wafanyao biashara za matunda wakiwa katika sehemu yao ya kazi.



huu ni uchakuchuaji dhahiri
Muandishi: Othman Michuzi | Tarehe: Saturday, October 09, 2010

hii kitu nimekutana nayo jana nilipokuwa safarini kuelekea Lushoto Mkoani Tanga,yaani basi hili linakula vichwa kama daladala za jijji la Dar.huwezi amini hawa abiria walisimama kutokea Chalinze mpaka Lushoto na wazee wa feva walikuwa wakisikamisha basi hilo na kukagua na kushuka kwa kusema "haya nawatakieni safari njema" hivi hii imekaa vyema kweli wadau.
 
Dah, ungeoonyesha na milima ya kule kwetu jamani, umenikumbusha kukaya kwetu, itabidi niende kidogo ingawa sasa basi letu hilo Shambalai limepata ajali jana na kuua wasaambaa wawili
 
Angalia hizi nazo ni za LUSHOTO, hii ndo bara bara ya Lushoto, watu wanasema ni zaid ya Kitonga na ninakubaliana nao, kwenye hii barabara hakuna sheria bali kuna heshima kwani vinginevyo mnapelekana bondeni. IMG_0044.JPG
 
Sorry naona picha nyingine zimegoma ku-upload ni kubwa zaidi ya mb2 kwa picha
 
Angalia hizi nazo ni za LUSHOTO, hii ndo bara bara ya Lushoto, watu wanasema ni zaid ya Kitonga na ninakubaliana nao, kwenye hii barabara hakuna sheria bali kuna heshima kwani vinginevyo mnapelekana bondeni.View attachment 15085

hapo hakuna barabara, kitonga kuna barabara. hapo pakichongwa barabara hapawezi kuwa hatari kama kitonga. inaonekana wewe huijui kitonga
 
lushoto ukweni kwangu jamani ni pazuri ma mkwe yupo hapo na ba mkwe na mashemeji na mimi ntakuwa hapo soon kwenye makazi yangu mapya
 
hapo hakuna barabara, kitonga kuna barabara. hapo pakichongwa barabara hapawezi kuwa hatari kama kitonga. inaonekana wewe huijui kitonga

mimi nilisoma tosamaganga iringa, naijua kitonga sana, huwezi hata kidogo kuilinganisha na barabara inayotokea mombo kwenda soni, km huamini fanya safari moja ndo utajionea mwenyewe.
 
Du kweli akili yangu chafu,ngoja nikatubu.nilitegemea kuona picha za wadada wa kisambaa na kizigua
 
hapo hakuna barabara, kitonga kuna barabara. hapo pakichongwa barabara hapawezi kuwa hatari kama kitonga. inaonekana wewe huijui kitonga

Nimepita mara zaidi ya elfu moja barabara zote mbili (Kitonga; Moro-Iringa na Soni; Lushoto-Mombo). Hauwezi kuniambia Kitonga panatisha zaidi ya Lushoto. Ile barabara ni finyu na kwenye hanging cliffs; chini na juu. Makorongo marefu zaidi na hakuna hata space ya kukimbilia. Kitonga ina nafuu
 
Niliwahi kukwama maeneo haya mwaka 1997 nikienda mlalo, jiwe Liliporomoka kipindi ya mvua likabomoa eneo la barabara. Na eneo la magamba malori yakanasa kwenye matope ikabidi nilale lushoto. Nilitumia siku mbili kwa safari ya masaa 12 tu.
1461040435367.jpg
1461040450915.jpg
1461040462347.jpg
hizi ni picha za juzi barabara ya Mombo Lushoto kabla ya kufika Soni
 
Back
Top Bottom