Kwa nchi kama Tanzania mtu wa kijijini akifa kwa coronavirus kama hajaenda hospitali serikali inajuaje?

Ikulumaliyawananch

JF-Expert Member
Mar 14, 2018
339
533
Hizi takwimu za serikali ni maigizo. Hivi Tanzania kuna utaratibu wa kufanya autopsy kwa kila mtu anaye kufa ukoje?

Hili baraa la coronavirus litauwa wengi Africa na wengi hawata ripotiwa. Kwasababu hatuna utaratibu wa kila anaye kufa kufanyiwa uchunguzi wa kujuwa chazo cha kifo chake. Watu wanafikiri kwamba nchi za uraya na Marekani watu wengi wamekufa kuliko mabara mengine.

lakini ukweli ni kwamba nchi za uraya na marekani zina utaratibu mzuri wa kufanya autopsy kwa kila anaye kufa, nakuweka tarifa hadharani bila kuficha. Yaani nchi za Ulaya hakuna anaye zikwa bila madakitari kutoa report ya kilicho sababisha kifo chake. Nchi kama China wanajulikana kwa kupika takwimu na kuficha ukweli hivyo kuna uwezekano China ina watu wengi waliokufa kuliko nchi nyingine yoyote ila hawakuripotiwa.

Kumbuka China walianza kupambana na ugojwa huu tangu mwishoni wa mwaka jana. Yaani baada ya hii coronavirus kuisha tunahitaji kufumua mifumo yote ya utawala ili tusuke upya. Huu ugojwa wa coronavirus umeonyesha jinsi viongozi wa Africa wasivyojali wananchi wao. Viongozi wengi wa Afrika kitu mhimu kwao sio uhai wa wananchi bali ni uhai wa utawala wao.

Ndio maana unaona Waafrika wanavyofanyiwa unyama huko China lakini hakuna hata kiongozi moja aliyempigia simu rais wa China kumweleza au hata kutoa kauli ya kukemea China kwa unyanyasaji wa kibaguzi wanaofanyiwa Waafrika wanoishi huko China. Pia Waafrika hasa Watanzania sasa tubadili mtazamo na tabia.

Katika nchi za Afrika hasa Tanzania kuna kasumba ya kuabudu watu wenye ngozi nyeupe. Yaani unakuta maofisini mtu mweupe anapewa kipaumbele kuliko mweusi, hii inaitwa self-hate. Kwa wafirika wote wenye akili tuanze kujipenda wenyewe tuache kasumba ya kufikiri watu weupe ni bora kuliko weusi.

Waafrika wote tuanze kupendana na kuinuwana. bila hivyo siku moja hawa watu weupe watakuja kutufuta kwenye uso wa bara na Africa na wataleta watu wao kuja kukaria bara letu.
 
Inabidi ujue nchi zingine zinahesabu vipi kabla hujaanza kulialia kila kitu kama kawaida ya watanganyika walio wengi.

Aidha sio kila kifo kinachotokea sasa kinasababishwa na corona, naona wengi mnasahau hili.
 
Wakifa si wameshakufa..
Siku hizi binadamu tumekuwa kama kuku wenye mdondo ukifa popote SHAURI YAKO.

"baba unahonga hawara elfu kumi,
watoto wanakufa na njaa nyumbani"
 
hizi takwimu za serikali ni maigizo. Hivi Tanzania kuna utaratibu wa kufanya autopsy kwa kila mtu anaye kufa ukoje?

Hili baraa la coronavirus litauwa wengi Africa na wengi hawata ripotiwa. Kwasababu hatuna utaratibu wa kila anaye kufa kufanyiwa uchunguzi wa kujuwa chazo cha kifo chake. watu wanafikiri kwamba nchi za uraya na marekani watu wengi wamekufa kuliko mabara mengine.

lakini ukweli ni kwamba nchi za uraya na marekani zina utaratibu mzuri wa kufanya autopsy kwa kila anaye kufa, nakuweka tarifa hadharani bila kuficha. Yaani nchi za uraya hakuna anaye zikwa bila madakitari kutoa report ya kilicho sababisha kifo chake. Nchi kama china wanajulikana kwa kupika takwimu na kuficha ukweli hivyo kuna uwezekano china ina watu wengi waliokufa kuliko nchi nyingine yoyote ila hawakuripotiwa.

Kumbuka china walianza kupambana na ugojwa huu tangu mwishoni wa mwaka jana. Yaani baada ya hii coronavirus kuisha tunahitaji kufumuwa mifune yote ya utawala ili tusuke upya. Huu ugojwa wa coronavirus umeonyesha jinsi viongozi wa Africa wasivyo jari wananchi wao. Viongozi wengi wa afrika kitu mhimu kwao sio uhai wa wananchi bali ni uhai wa utawala wao.

Ndio maana unaona wafirika wanavyo fanyiwa unyama huko china lakini hakuna hata kiongozi moja aliyempigia simu raisi wa china kumweleza au hata kutoa kauli ya kukemea china kwa unyanyasaji wa kibaguzi wanao fanyiwa wafirika wano ishi huko china. Pia wafirika hasa watanzania sasa tubadili mtazamo na tabia.

Katika nchi za afrika hasa Tanzania kuna kasumba ya kuabudu watu wenye ngozi nyeupe. yaani unakuta maofisini mtu mweupe anapewa kipaumbele kuliko mweusi, hii inaitwa selfhaters . kwa wafirika wote wenye akili tuanze kujipenda wenyewe tuache kasumba ya kufikiri watu weupe ni bora kuliko weusi.

Wafrika wote tuanze kupendana na kuinuwana. bila hivyo siku moja hawa watu weupe watakuja kutufuta kwenye uso wa bara na Africa na wataleta watu wao kuja kukaria bara letu.
Hoja yako haitofautiani na ya wanaodai Serikali inapika takwimu za hali ya COVID-19, katika taarifa zake, lakini hao hao hawajitokezi kusema mgonjwa fulani wanayemjua hajatajwa.

Je, unajua au umesikia waliokufa huko vijijini na wamezikwa bila Serikali kujua? Kumbuka maisha ya vijijini kwa leo siyo yale ya kabla na mara tu baada ya uhuru. Isitoshe vijijini hakuna watu wasiyojua mambo ya kisasa. Hakika huko tahadhari za kujikinga na maambukizi ni kubwa mno kuliko mijini. Isitoshe mgeni akiingia anajulikana siku hiyo hiyo. Wasomi na wataalamu mbalimbali wanazikwa huko.

Punguza au/na acha kuishi kwa dhana. Jikinge maambukizi, wewe na familia yako, kwa kuzingatia ushauri unaotolewa mara kwa mara. Hayo ya kiutawala waachie wawakilishi (Rais na viongozi wake, Wabunge, Madiwani, Wenyeviti wa Serikali za Mitaa na wajumbe wake). Hao wanahusika na jamii, kwa ujumla, kuihamasisha na kuisimamia katika utekelezaji wa ushauri wa kitaalamu.
 
Back
Top Bottom