Kwa namna wabunge wanavyolalamika kuna haja ya kuiangalia kwa makini Ilani ya CCM, yawezekana imejaa janja janja

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,773
141,638
Awali ya yote nimshukuru mbunge wa Mbeya ambaye pia ni naibu Spika kwa kutufumbua macho kwamba kuna maeneo fulani ilani inasema tofauti na uhalisia unaosemwa na serikali.

Natoa rai kwa wananchi tulioichagua CCM kwa kishindo kikuu tuipitie kwa makini Ilani ya uchaguzi hasa katika maeneo yanayotuhusu ili kujiridhisha na utekelezaji wake.

Kazi Iendelee!
 
Awali ya yote nimshukuru mbunge wa Mbeya ambaye pia ni naibu Spika kwa kutufumbua macho kwamba kuna maeneo fulani ilani inasema tofauti na uhalisia unaosemwa na serikali...
Joni hiyo inaitwa akili kumkichwa,ama zakuambiwa changanya na zakwako.
 
Jamaa kwenye kampeni alikuwa anaenda anaahidi Tu "hii barabara itajengwa , manager tangaza kandarasi sasa hvi " anampigia simu Waziri wa ujenzi , anamuuliza kuna sh ngap hapo.

Waziri naye huku anajamba jamba anasema kuna Kias fulan Mzee , anasema haya idhinisha pesa fulan Kwa Ajit ya barabara ya mwilolewa kwenda mtobe km 150 , wananchi wewe.
 
Sasa mnajadili mini ikiwa mkuu wa kaya alishasema tangaza tenda! Hela zipo tens nyingi sana.Tumechezewa sana.

Ninyi hamtaki kumuunga mkono MAGU.
 
Wewe na CCM wenzio wote ni wanafiki!

Umesahau huyu mkurugenzi wa tume dhaifu ya uteuzi na sio uchaguzi alipomkandia Lissu na kuiponda ilani ya CHADEMA bila aibu akaanza kuisifia ilani ya CCM nanukuu

"Watanzania wa sasa wanataka maji, barabara na vituo vya afya sio brah brah"

Nani alimuambia watanzania wote wanahitaji vitu vyote hivyo? Vipi kuhusu haki zao na uhuru wao je ilani ya CCM vilujumuishwa hivi??

Inakuaje muamuzi anakua upande wa timu moja nini unategemea???
JamiiForums1397431097.jpeg
 
Awali ya yote nimshukuru mbunge wa Mbeya ambaye pia ni naibu Spika kwa kutufumbua macho kwamba kuna maeneo fulani ilani inasema tofauti na uhalisia unaosemwa na serikali...
Ina maana ww uliamini ile ni ilani au orodha ya mahitaji ya binadamu? Ile ilani ni uhuni kama uhuni mwingine. Nimeshasema sana hapa jukwaani kuwa hakuna uwezekano wa kuwa na ilani iliyoandikwa kila hitaji la wananchi, wakati uwezo wa kuhudumia kama hiyo ilani ilivyo ni chini ya 30%.

Na huo uhuni wa kujaza page nyingi ni ujinga wa jiwe ili aonekane ana uwezo wa kuongoza. Lakini kwa akili ya kawaida tu ile ilani ni utapeli kama utapeli mwingine. Hatimaye sasa utapeli ule uko wazi.
 
Awali ya yote nimshukuru mbunge wa Mbeya ambaye pia ni naibu Spika kwa kutufumbua macho kwamba kuna maeneo fulani ilani inasema tofauti na uhalisia unaosemwa na serikali...
Unaweza kudanganya watu wote kwa muda fulani.lakini huwezi kuwadanganya watu wote kwa muda wote.KWELI MACCM NI WAKOLONI WEUSI TANZANIA.
 
Wameshaona hii Ilani haitafanikiwa maana mwenye Ilani hayupo. Matumaini yameenda na mwendazake.

Na sasa tunafanya kazi tukiwa ikulu mda wote.
 
Mmkuu hao wabunge wa CCM wanafiki tu!!! Ndiyo hao walikuwa wanaisifia serikali hata miezi mitatu hatujamaliza. Hawaniconvince kwa chochote!!! Eti leo wanajifanya mbogo!!!!
 
Back
Top Bottom