Kwa mwenye ufahamu kuhusu hili naombeni msaada wenu

Remotex

Member
Oct 3, 2020
29
75
Habarini wanajukwaa la Elimu... kwa heshima na taadhima ninajambo naomba msaada kwenu...

Nilimaliza elimu yangu ya sekondari (O'Level) mwaka 2002 Shule flani ya ufundi hapa nchini tuseme miaka 18 iliyopita... skubahatika kuchaguliwa kuendelea na masomo, kwa maana sikufanya vizuri... na baada ya hapo nilirudi kijijini kupambana na shughuli za kilimo.

Baada ya kujitathimini kwa muda mrefu, Bado najihisi nina uwezo flani wa kimasomo kusoma masomo ya ufundi katika chuo cha ufundi huko Dar chuo cha Dar es Salaam Institute of Technology (DIT) kwa Course ya Biomedical Equipment Engineering (BEE). Ili niweze kuwakomboa ndugu na jamaa huku kijijini kwa huduma za kiafya.

Baada ya kufwatilia vigezo vya kujiunga nimegundua kuwa skusoma "Biology" sababu ilikuwa ni shule ya ufundi. Je hicho kinaweza kuwa kikwazo cha kutochaguliwa... Si kwa sasa ni mwakani 2021 Mungu akipenda na nitajisomesha mwenyewe.

Matokeo yangu ni kama ilivyo hapa chini.
1. Basic Mathematics-B - Pass
2. English - C - Pass
3. Geography - C - Pass
4. Eng/Science - D - Pass
5. Chemistry - D - Pass
6. Kiswahili - D - Pass
7.Geography - D - Pass
8. Building Construction - D - Pass

Kwa mwenye ufahamu kuhusu hili naombeni msaada wenu...
"PAMOJA TULIJENGE TAIFA LETU"
Ahsanteni naomba kuwasilisha.
 
Remotex

Member
Oct 3, 2020
29
75
Nipo nje ya mada

hiyo BBE huwezi komboa familia yako
Ni kweli umejistukia kuwa uko nje ya MADA
sasa kwann unapoteza muda wa kuandika maoni yako kama unajua umetoka nje ya MADA? kitu kama hujui bora ukae kimya

Issue ya familia yangu haihusiani na nlichomba kusaidiwa maoni...
 
Remotex

Member
Oct 3, 2020
29
75
Mkuu hayo ni macourse gani? Atajiajiri vipi potelea mbali kuajiriwa?
Jamani someni MADA kwa umakini, wengi humu najua mmenizidi Elimu kwa kiwango kikubwa... mimi sijaomba ushauri wa kujiajiri wala kuajiriwa, mimi nilichouliza kwenye swali langu la msingi ni kwamba. Je, naweza kukidhi vigezo vya kupata nafasi ya kusoma hiyo course sababu sjasoma BIOLOGY baaaasi... mimi nlishajiajiri na shamba miaka 17 iliyopita... nataka kuisaidia jamii na wala si familia yangu binafsi
 
Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
12,591
2,000
Mkuu hayo ni macourse gani? Atajiajiri vipi potelea mbali kuajiriwa?

Mwenzangu labda anataka ajiajiri afungue office yake ya ku repair vyombo vya maabara 😂😂🤣🤣🤣🤣, mtoa mada fanya throughly research kabla huja apply, usije pats dead end! Hivi hio course inahusu nini?🤣🤣🤣😊😊😊😊☺️☺️☺️
 
Hazchem plate

JF-Expert Member
Feb 25, 2011
9,924
2,000
Mwenzangu labda anataka ajiajiri afungue office yake ya ku repair vyombo vya maabara , mtoa mada fanya throughly research kabla huja apply, usije pats dead end! Hivi hio course inahusu nini?

inaonekana kukaa mtaani hakujamfunza
 
Remotex

Member
Oct 3, 2020
29
75
Mwenzangu labda anataka ajiajiri afungue office yake ya ku repair vyombo vya maabara , mtoa mada fanya throughly research kabla huja apply, usije pats dead end! Hivi hio course inahusu nini?
Mbona umeshajijibu hapo mwenyewe? fixing and repairing vifaa tiba, Je kipi kinachoshindikana hata kama ni kufungua workshop? watu wanavunjika viungo mbalimbali je siwezi kutoa huduma ya kuwatengenezea miguu bandia? mikono bandia? na kadhalika... Mbona hamnijibu mnazunguka zunguka tuuuuuuuu kama mtu hujui nyamaza
 
Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
12,591
2,000
Mbona umeshajijibu hapo mwenyewe? fixing and repairing vifaa tiba, Je kipi kinachoshindikana hata kama ni kufungua workshop? watu wanavunjika viungo mbalimbali je siwezi kutoa huduma ya kuwatengenezea miguu bandia? mikono bandia? na kadhalika... Mbona hamnijibu mnazunguka zunguka tuuuuuuuu kama mtu hujui nyamaza

Umeambiwa sasa hivi hawana hiyo mikono na miguu bandia???
 
Remotex

Member
Oct 3, 2020
29
75
Umeambiwa sasa hivi hawana hiyo mikono na miguu bandia???
Mchawi ni nani? Mchawi ni mtu yeyote anayetumia mbinu zozote zile iwe mchana au usiku kurudisha maendeleo ya mtu nyuma.

Yani wewe uko against tu... Rebecca jaribu kuwa optimistic kidogo, hatuwezi kuwa na maendeleo kwa watu kama nyie msiopenda maendeleo.

Huduma za afya zingekuwa zinatosha serikali isingekuwa inajenga vituo vya afya kila kukicha, na kila chuo inapoweka course jua kunauhitaji... issue ya kujiajiri au kuajiriwa n la mtu binafsi... nmesema tangu mwanzo kama huwezi kunipa ushauri kaa kimya wapo wanaoweza... kuandika andika humu hakukukufanyi wewe kuwa bora kuliko wengine
 
KISIWAGA

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
2,259
2,000
Mkuu sasa unaanzaje kurudi darasani na huo utitiri wa mindevu humo kidevuni kwako au ndio spana za ugumu wa maisha zimekupiga uchizi & upofu
 
Remotex

Member
Oct 3, 2020
29
75
Mkuu sasa unaanzaje kurudi darasani na huo utitiri wa mindevu humo kidevuni kwako au ndio spana za ugumu wa maisha zimekupiga uchizi & upofu
Kisiwaga unafeli wapi?

Mimi sisomi kwa ajili ya kutafuta maisha mkuu ili niajiriwe... nataka kusoma ili nisaidie jamii na niongeze kiwango changu cha elimu... hata historia ya marehemu iwe ndefu ndefu kidogo...
 
Sir_Mimi

JF-Expert Member
Jun 21, 2013
6,711
2,000
Jamani someni MADA kwa umakini, wengi humu najua mmenizidi Elimu kwa kiwango kikubwa... mimi sijaomba ushauri wa kujiajiri wala kuajiriwa, mimi nilichouliza kwenye swali langu la msingi ni kwamba. Je, naweza kukidhi vigezo vya kupata nafasi ya kusoma hiyo course sababu sjasoma BIOLOGY baaaasi... mimi nlishajiajiri na shamba miaka 17 iliyopita... nataka kuisaidia jamii na wala si familia yangu binafsi

Mkuu Remotex

Nikutie moyo,humu aliyekuzidi elimu ni yule mwenye maisha zaidi yako hata STD 7 kama amesogea kimaisha bado si size yako,kibongo bongo elimu za kwenye makaratasi hazimsaidii tena mtu zaidi ya knowledge ila kuigeuza iwe pesa haiwezi.usione watu wanaunga unga humu kwamba wanajua meeengi ukaogopa unakuta kwa siku haingizi hata mia amebaki kuzunguka na bahasha tu kuomba ajira bora wewe upo shamba unaweza kujisomesha.

Nikupongeze kwa kutaka kurudi shule,nakushauri ingia google tafuta website au email yao waandikie haya maswali nadhani yanajibika kirahisi kama unakutana na mtu aliye kitengo pale.
 
Sir_Mimi

JF-Expert Member
Jun 21, 2013
6,711
2,000
Umeambiwa sasa hivi hawana hiyo mikono na miguu bandia???
.......................Ulishapata mtu mwenye tatizo au ndugu akahitaji iwe ni mguu au mkono wa bandia?

Pale CCBRT japokuwa pana mkono wa beberu ila mguu wa bandia bila 800K hujapewa,na hiyo ni pamoja na uandike barua kuomba msaada yenye muhuri wa serikali za mitaa kwamba wewe ni maskini hivyo wakusaidie kama sivyo kiungo kinafika 1mill na zaidi sasa kama mtu ameona ana wito wa kusaidia jamii inayomzunguka kwanini asifanye aseme ila “kwa sababu serikali yenyewe inavyo basi wataendaga kununua huko ngoja mi niachane navyo”!

Ni wangapi na uchumi huu wenye uwezo wa kutoa 800K hata kama ni lak3 ili kununua kiungo cha bandia?nadhani wazo la mdau ni zuri msimkatishe tamaa.
 
Remotex

Member
Oct 3, 2020
29
75
Mkuu Remotex

Nikutie moyo,humu aliyekuzidi elimu ni yule mwenye maisha zaidi yako hata STD 7 kama amesogea kimaisha bado si size yako,kibongo bongo elimu za kwenye makaratasi hazimsaidii tena mtu zaidi ya knowledge ila kuigeuza iwe pesa haiwezi.usione watu wanaunga unga humu kwamba wanajua meeengi ukaogopa unakuta kwa siku haingizi hata mia amebaki kuzunguka na bahasha tu kuomba ajira bora wewe upo shamba unaweza kujisomesha.

Nikupongeze kwa kutaka kurudi shule,nakushauri ingia google tafuta website au email yao waandikie haya maswali nadhani yanajibika kirahisi kama unakutana na mtu aliye kitengo pale.
Nashukuru kwa ushauri wako kiongoz... sababu najihisi bado nauwezo wa kukaa darasani... Hesabu bado nazikumbuka vizuri tu, ni kama mtu alieshajua kuendesha baiskeli hata ipite miaka mingapi bila kuendesha ukimpa ataendesha tu... na pia Lugha hainipigi chenga... I can cope with any environment at any particular circumstances
 
mtoto mdogo sana

JF-Expert Member
Apr 16, 2020
306
1,000
Hoja ya msingi:

Mtoa mada hapo juu, lengo lake sio ishauri wala maoni ya wachangiaji.

Ana majibu yake na mlengo wa maamuzi ambao amekwisha kujiwekea na anangoja kura za kutosha kutoka kwa wachangiaji ili ajiridhishe.

Hii ni kutokana na namna anavyoelekeza namna inavyotakiwa ajibiwe na anaamini kuwa kuna usahihi alionao ambao hakuna mtu anayeweza kuuelewa.

Aidha niwe upande wa mtoa mada

Aina ya uhandisi unayohitaji kusimea haihitaji alama za somo la Biolojia hivyo ili kujiridhisha zaidi, tafuta kitabu cha mwongozo na maelezo ya kozi zinazotolewa na chuo husika uangalie iwapo unakidhi.

Uwe na siku njema
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom