Kwa mwenye uelewa kuhusu nafasi ya Cardinal Pengo kwenye ukatoliki

Pamoja na kwamba sikubaliani nae katika mabo Fulani Fulani nitabaki kumuheshimu kama mpakawa mafuta, successor of the apostles maana ndio maaan halisi ya askofu.

Mzee "mpakwa mafuta"?Nani kampaka?.....Labda uniambie kuna mwanadamu mmoja baadhi ya wanadamu hapa duniani wanamwita "Papa" ndio kampaka mafuta kwa utashi wake mwenyewe wa kibinadamu,mungu hajahusika hapo na hajatuma mtu...labda mtupatie ushahidi..

Pengo na wengine in those lines,ni wanadamu ,anaheshimiwa kadri yeye anavyoheshimu wengine,Thats it sir!
 
Tena unaweza kumwondelea ukardinali akapewa mwingine. Na huyu akistaafu lazima arudi kigoma tu.
 
Mzee "mpakwa mafuta"?Nani kampaka?.....Labda uniambie kuna mwanadamu mmoja baadhi ya wanadamu hapa duniani wanamwita "Papa" ndio kampaka mafuta kwa utashi wake mwenyewe wa kibinadamu,mungu hajahusika hapo na hajatuma mtu...labda mtupatie ushahidi..

Pengo na wengine in those lines,ni wanadamu ,anaheshimiwa kadri yeye anavyoheshimu wengine,Thats it sir!
Unawakumbuka wanafunzi wa Yesu? walifundisha na kuwapa mikoba wengine na wengine na wengine, hadi unawaona maaskofu wa kanisa Leo Hii, inaitwa apostolic succession.
 
Ukisikia rais wa baraza la maaskofu katoliki Tanzania huyo ndiye mwenye mamlaka na wakatoliki wa tanzania

Pengo yeye ni kardinali hiki ni cheo anachopewa na papa na kinampa uwezo wa kuiwakilisha nchi kumchagua papa au yeye mwenyewe kuwa papa kama hajatimiza umri wa miaka 80

Katika baraza la maaskofu katoliki pengo ni mjumbe tu kama walivyo maaskofu wengine wa katoliki
 
Acha stori za kijiweni, msamiati wa upako kanisa katoliki haupo, maaskofu wote hapa Tanzania akiwemo huyo pengo wapo chini ya balozi wa papa,

Hapa imetolewa elimu nzuri sana wewe umeamua kukalia elimu ya kijiweni, jielimishe kupitia michango ya wadau utaelewa, ingekuwa pengo ndio bosi wao ungesikia kateua askofu Fulani, kamhamisha yule, kamshusha cheo askofu Fulani, kumbuka hata kwenye sherehe za kumsimika askofu wa jimbo fulani anaweza asipangwe kwenda kumsimika, na shughuli ikafanywa na mwakilishi wa papa au atateuliwa askofu yeyote wa jimbo kuu au hata wa jimbo la kawaida

Mara nyingi hawa wawakilishi wa papa wanakuwa na cheo cha kiuaskofu au kadinari
Hongera sana kwa kutoa elimu nzuri ili wasioelewa wapata elimu,Nasisitiza uko sawa kabisa.
 
Pengo ni Askofu sawa na maaskofu wengine, yeye mamlaka yake ya Uaskofu yanaishia jimbo kuu la Darisalama tu.
Katika kanisa katoliki maaskofu wote huwa wanateuliwa na Papa(balozi wa papa nchini kupeleke barua ya siri wa mapadri na wakati mwingine hata walei wa mahalia na kupendekeza majina matatu ya mapadri wenye sifa kama tabia njema,elimu,imani ya kanisa na nk na majina hayo yanapelekwa kwenye cenodi kujadiliwa na jina moja litakalopita hapo linaenda kwa papa tiyari kwa kutangazwa.
 
Unachanganya sana haya makitu. Elewa kwamba daraja la juu kabisa ni kuwa Askofu, hata Papa ni Askofu na kwa utaratibu wa sasa ni lazima atimize majukumu yake akiwa Vatican.
Kardinali huteuliwa na Papa peke yake na wajibu wake mkuu ni katika kumchagua mwandamizi wa papa na kumshauri katika kuliongoza kanisa lote.
Kwa mantiki hiyo kardinali siyo mkuu wa maaskofu na wala siyo mkuu wa kanisa katoliki katka nchi mahalia.
 
We IQ fupi sana! Yani unahukumu uelewa wangu kisa hukubaliani na Mimi? Kwa taarifa yako tu, Mimi ni mkatoliki hard to core, naifaham vizuri church hierarchy, kanisa siyo sum of national churches!! Kila jimbo lina autonomy we takataka, Pengo hawezi na hana mamlaka yeyote nje ya jimbo lake la dar es salaam, Pengo akiongea hawakilishi Tanzania, anawakilisha Dar! Kuna bwege mwingine kama wewe kaanzisha thread eti makao makuu ya kanisa Tanzania yaamishiwe Dodoma! Nonsense kabisa, ndo akili kama zako. Yani mnadhani pale st Joseph ndo makao makuu ya kanisa Tanzania? Muundo wa kanisa siyo national churches, hatuna individual national church, kuna had padri ni cardinal kwa taarifa yako, umegusa pabaya. Eti nikuPM? Nikupm mbumbumbu wa mwisho.shiit
Hard core kwenye ukatoliki unamtukana mwenziyo kiasi hicho!
Mada ilikuwa nzuri sana ni namna tu ya kupeana maarifa na kuongezeana ujuzi basi.
Uelewe hapa duniani hadi kifo chako hautafaulu kuelewa mambo yote.
Na hata unachokielewa, saazingine waweza kuwa unakielewa tofauti na mtu anayekielewa sawasawa akakupinga.
Sasa unapokutana na mbishi ama anayejua zaidi yako, 'usizalalile' hadi kutokwa povu, mpe nafasi ya kujenga hoja.
Unaweza kukuta una-repent kuwa ulipotoshwa katika kuelimishwa ama haukuelewa wakati ukifundishwa, hayo yote yapo!
Sasa mitusi yanasaidia nini kwenye mjadala na mtu usiyefahamiana naye?
Forum nzuri sana hii, tujifunzeni kuvumiliana.
 
Habar wakuu! mimi ni muumini wa dhehebu la katoliki, kumekuwa na simtofaham baina ya sisi wakatoliki kuhusu nafas ya pengo katika baraza la maaskofu tanzania! jana nilikuwa nabishana na jamaa mmoja mwenye itikad tofaut na ukristo kwa kusema ivyo nadhan mtakuwa mmenipata jamaa ni itikadi gan! kwa uwelewa wangu nafaham kama pengo ni askofu wa jimbo kuu katoliki la Dar ila kwenye balaza la askofu tanzania sifaham nafas yake na jamaa yeye anasema pengo ndio kiongozi mkuu wa wakatoliki tanzania sasa kwa mwenye uelewa juu ya hili tunaomba atufafanulie najua wapo baadhi ya wakatoliki wenye uwelewa mdogo kama mimi, ivyo kwa faida ya wengine , kiongozi mkuu wa wakatoliki tanzania ni yupi? ni kweli Pengo au kuna mwingine? na kama kuna mkubwa zaidi ya Cardinal Pengo uyo nae atakuwa Cardinal au atakuwa na cheo gan?

Wewe ni mkatoliki kweli?
 
JE, KUNA TOFAUTI GANI KATI YA KADINALI NA ASKOFU?

'Canon Laws' ambazo ibara zake hutajwa hivi, Can. 381 na kadhalika zinatosha kumwelewesha yeyote muundo wa Kanisa Katoliki. Zinataja mamlaka ya askofu, askofu-mkuu, kardinali, rais wa baraza la maaskofu na zaidi.

Sheria ya kanisa, Can. 381(1) na Can. 391(1), zinasema kwamba askofu jimboni, ndiye mkuu na mwenye madaraka jimboni.

Ibara hii inatokana agizo la mkutano wa maaskofu uitwao Vatican II, uliotoa hati iitwayo “ Lumen Gentium” ibara ya 27, isemayo kwamba, askofu jimboni ni mwakilishi wa Yesu na si mwakilishi wa Papa au chombo chochote.

Vilevile, hakuna andiko la kanisa linalotaja maneno “Makao makuu”. Badala yake jengo la kanisa liitwalo “ Cathedral ” ndilo lenye mamlaka ya uaskofu.

Kwa wale wanaopenda neno “Makao makuu”, basi afadhali waseme “ Cathedral ” ndiyo “Makao makuu” ya kanisa jimboni.

Pale Roma, “ Cathedral ” ni kanisa liitwalo “St. Lateran’s archbasilica”. Kumbe, makao “makuu ya Kanisa Katoliki duniani”, siyo anakoishi Papa yaani kule Castle Gandolfo au pale Vatican, bali ni hapo “St. Lateran archbasilica”.

Hata kanisa maarufu lililopo Vatican, yaani “St. Peter’s basilica”, lina hadhi ndogo iitwayo “Basilica”, wakati hili la “makao makuu” linaitwa “Arch-basilica”, hadhi kubwa kuliko makanisa yote Katoliki duniani.

Ibara ya 390 na 436(3) ya sheria za kanisa, zinamkataza askofu (bishop ) pamoja na askofu-mkuu ( arch-bishop ) wasiendeshe misa kwenye “ Cathedral ” bila ruhusa ya askofu mahalia, yaani askofu mwenye jimbo.

Hivyo, Polycarp Kardinali Pengo au askofu Tarcicius Ngalalekumtwa, hawawezi kuendesha misa kwenye “ Cathedral” ya Moshi, yaani kanisa kuu la jimbo la Moshi, bila kwanza kuruhusiwa rasmi na askofu wa Moshi Isaac Aman.

Pia, kwa kutumia sheria, Can. 763, askofu wa jimbo, mfano pale hapa Moshi, amepewa mamlaka na Papa kumpiga marufuku askofu yeyote duniani asihutubie lolote jimboni kwake ikihitajika kufanya hivyo. Yaani zikiwepo sababu za msingi kufanya hivyo.

Mwaka 2004, Joachim Kardinali Meisner, alitumia ibara hii kumkataza askofu Jacques Gaillot asiingie jimboni Cologne, kwani alikwishachokwa kuigawa nchi kwa kauli zake alizoziita “ni maoni yake binafsi”.

Nimechagua ibara hizi chache kuonyesha mamlaka ya askofu, uone kwamba, hakuna askofu hata mmoja nchini aliye juu ya mwingine. Kila mmoja ana mamlaka kamili katika jimbo lake, na ndiye mchungaji wa waumini walio katika jimbo lake.

SASA TUONE UKARDINAL NI NINI?

Mkatoliki akitaka utumishi wake utambulike rasmi kikanisa, lazima atasajiliwa au kusimikwa kwenye kundi linalotambulika. Mara nyingi huwa ni jimboni au kwenye jumuiya ziitwazo “ religious”.

Zamani kila aliyesimikwa hivyo aliitwa “kardinali”. Lakini kuanzia karne ya tisa, neno “kardinali” lilibaki kutumika tu kwa walioitwa na Papa wakahamia na kusimikwa upya Roma.
Padri aliyehamishiwa Roma, huko alisimikwa kwenye kanisa lililoitwa “ titular church”. Hiyo ikawa aina ya kwanza ya makardinali, wakijulikana kama “ cardinal-Priest ”.

Baadaye mashemasi nao wakawa wanahamishiwa Roma, huko wakapewa vituo vilivyoitwa “ deaconia ”. Ikawa aina ya pili ya makardinali waitwao “ Cardinal-Deacon ”.

Kazi za Papa zilipoongezeka, akahitaji msaada wa maaskofu kutoka majimbo jirani yaliyoitwa “ Suburbicarian Diocese”. Hali ya maaskofu hawa kuwa karibu na kuhitajiwa Roma, kukawafanya waitwe “ Cardinal-Bishop ”.

Hizi ndizo aina tatu za makardinali. Zipo hadi leo, yaani “ Cardinal-Deacon ”, “ Cardinal-Priest ” na “ Cardinal-Bishop ”.

Kuanzia mwaka 1150, Papa alianza kuwaita makardinali kwenye vikao vya kumshauri, ambavyo hadi leo vinaitwa “ Consistory” .

Mwaka 1179, haki ya kumchagua Papa mpya, ikaacha kuwa ya wanajimbo wengine wa Roma, bali ikabaki kwa “makardinali” tu kwenye mkutano unaoitwa “ Conclave ”. Mwaka 1975, Papa Paul VI alifupisha umri wa kardinali kuhudhuria “ Conclave ”, yaani chini ya miaka 80.

Tumeona kwamba, kitendo cha kupewa ukardinali na Papa, ni uhamisho wa kwenda Roma. Uhamisho huo unamfanya awe mwanajimbo wa Roma, ambaye kama haishi Roma, basi kokote aliko duniani anafanya umisionari.

Ile aina ya “ Cardinal-Bishops ” bado hupewa lile kanisa liitwalo “ Suburbicarian Diocese”. Siku hizi “ Cardinal-Deacons ” hupewa hata yale makanisa, “ titular church”.

Ile aina ya “ Cardinal-Priest ”, wengi hawaishi Roma kwa sababu ya umisionari wao mbali na Roma. Mmojawapo ni Polycarp Kardinali Pengo, anayeongoza Jimbo la Dar es Salaam, lililo kilomita 6043 kutoka Roma.

Je, mtu anapewa ukardinali baada ya kufikia ngazi ipi ya utumishi? Teodolfo Kardinali Mertel, alipewa ukardinali Machi 15, 1858 akiwa hajapata hata ushemasi. Machi 20, 1556 Reginald Kardinali Pole alikuwa ameshakuwa kardinali kwa miaka 20 na ameshashiriki “ Conclave ” tatu akiwa hajawa padri.

Kuanzia Februari 2, mwaka 1983, Papa John Paul II aliwapa ukardinali mapadri saba, waliobaki na upadri wao bila kuwa maaskofu.

Watano kati yao wameshafariki ambao ni Henri Kardinali de Lubac, Avery Kardinali Dulles, Aloys Kardinali Grillmeier, Joseph Kardinali Congar, Leo Kardinali Scheffczyk. Wawili kati yao wako hai, yaani Roberto Kardinali Tucci na Albert Kardinali Vanhoye.

Papa Benedict XVI, naye ana mapadri wanne aliowapa ukardinali bila kuwa maaskofu. Watatu wamekwishafariki, ambao ni Domenico Kardinali Bartolucci, Urbano Kardinali Navarrete, Umberto Kardinali Bett. Aliye hai ni Josef Kardinali Becker.

“ Roman Curia ” ni jopo linalomsaidia Papa kuendesha kanisa lote duniani. Karibu timu yote “Roman Curia” huripoti shughuli zake kwa “ Secretariet of State”.

Hivyo, “ Secretariet of State ” ana majukumu mazito ndani na nje ya Kanisa, kwani Papa anaweza kusifiwa au kulaumiwa ndani na nje ya kanisa kwa sababu tu ya utendaji wa huyu “ Secretariet of State”.

Nafasi hii ya “ Secretariet of State ” sasa inashikwa na Pietro Kardinali Parolin, aliyeachiwa na Tarcisio Kardinali Bertone.
Wote Kardinali Bertone na huyu Parolin ni maaskofu. Lakini mwaka 1848, nafasi hii ilisimamiwa vizuri na Giacomo Kardinali Antonelli, ambaye alikuwa shemasi tu hadi kifo chake Novemba 06, 1876.

Papa anaweza kumpa mtu ukardinali kwa siri, yaani “ Cardinal in pectore” . Serikali ya China ilipomfunga askofu Ignatius Kung Pin-mei wa Shanghai, haigundua kwamba akiwa humo gerezani alipewa ukardinali kwa siri mnamo Juni 30, 1979.

Kardinali yeyote, kama alivyo Polycarp Pengo, siyo mwakilishi wa nchi kama Tanzania, kwani, hakuna jimbo wala parokia inayoitwa Tanzania.

Tumeona kwamba ukardinali ni kuwa mwanajimbo wa Roma au jirani na Roma (suburbcarian ). Hivyo, hata inavyoelekeza sheria ya kanisa, Can. 357(1), kardinali ni mwakilishi wa parokia yake pale Roma yaani “titular chuch”, ambayo ya Polycarp Pengo pale inaitwa Nostra Signora de La Salette.

Lakini ibara hiyo 357(1), bado inamdhibiti kardinali kwamba, hata hiyo parokia yake pale Roma, haruhusiwi kuiingilia kiutawala, kiuendeshaji au kinidhamu.

Hivyo, eneo pekee duniani ambako Polycarp Pengo ana mamlaka ya uchungaji, utawala, uendeshaji au nidhamu, ni ndani ya mipaka ya Dar es Salaam tu (rejea, Can. 381(1).

Wakati mabaraza ya maaskofu yanashamiri duniani, baadhi ya maaskofu waliitaadharisha Vatican kwamba, ama baraza zima au rais wa baraza hilo, ataweza kujikuta anaingilia ukuu wao jimboni na kugeuka kuwa mkuu nchini.

Hivyo, Papa aliiweka ibara ya 455(4) makusudi kulinda huo ukuu wa askofu wa jimboni, ili asiingiliwe kwa namna yoyote na baraza zima au rais wa baraza la maaskofu.

Hivyo, ibara hii inatosha kukuthibitishia kwamba, rais wa baraza la maaskofu, si kiongozi wa Kanisa Katoliki nchini, wala si mkuu wa maaskofu nchini.

Hivyo, Rais wa TEC, Askofu Tarcicius Ngalalekumtwa, naye eneo pekee la ukuu wake, ni mipaka ya Jimbo la Iringa tu. Nafadi yake kama Rais wa TEC inaheshimiwa na maaskofu wote pale tu anapotoa tamko kwa niaba yao. Yaani anaposimama kwa niaba ya kauli ya maaskofu wote, au anapotoa taarifa fulani kwa kuzingatia mipaka yake halali kiuongozi.

Mkutano wa makardinali wote duniani na Papa yaani “ consistory”, hauna mamlaka ya kutoa tamko kisha liitwe kuwa ni la Kanisa Katoliki duniani. Huo ni mkutano wa askofu wa Roma na wanajimbo wake.

Wakati mkutano wa maaskofu wote duniani na Papa, ndicho chombo kikuu kupita vyote kiitwacho “ magisterium”, chenye mamlaka ya kuamua lolote ndani ya Kanisa Katoliki.

Ibara ya 1121 ya Katekism ya Kanisa Katoliki inasema, askofu haachi kuwa askofu hadi kifo chake, hata akijiuzulu madaraka.

Lakini ukardinali ni tofauti. Padri Louis Billot alikuwa kardinali kwa miaka 16 ,alipojiuzulu ukardinali Septemba 21, 1927, akaacha kuwa kardinali.

Hivyo, uaskofu ni nafasi ya juu zaidi na nyeti zaidi ndani ya Kanisa Katoliki, kuuzidi ukardinali.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom