Kwa mwenye uelewa kuhusu nafasi ya Cardinal Pengo kwenye ukatoliki

cleokippo

JF-Expert Member
Dec 21, 2014
985
500
Habar wakuu! mimi ni muumini wa dhehebu la katoliki, kumekuwa na simtofaham baina ya sisi wakatoliki kuhusu nafas ya pengo katika baraza la maaskofu tanzania! jana nilikuwa nabishana na jamaa mmoja mwenye itikad tofaut na ukristo kwa kusema ivyo nadhan mtakuwa mmenipata jamaa ni itikadi gan! kwa uwelewa wangu nafaham kama pengo ni askofu wa jimbo kuu katoliki la Dar ila kwenye balaza la askofu tanzania sifaham nafas yake na jamaa yeye anasema pengo ndio kiongozi mkuu wa wakatoliki tanzania sasa kwa mwenye uelewa juu ya hili tunaomba atufafanulie najua wapo baadhi ya wakatoliki wenye uwelewa mdogo kama mimi, ivyo kwa faida ya wengine , kiongozi mkuu wa wakatoliki tanzania ni yupi? ni kweli Pengo au kuna mwingine? na kama kuna mkubwa zaidi ya Cardinal Pengo uyo nae atakuwa Cardinal au atakuwa na cheo gan?
 

bugzbunny

JF-Expert Member
Mar 9, 2013
647
500
Pengo ni askofu mkuu wa dar es salaam tu! Akienda jumbo LA morogoro ni mualikwa tu Luna askofu mkuu wake. Ukadinali manaake ni anaweza kuingia kwenye conclave kumchagua papa, etc na ukardinali Ata padri anaweza kupewa .pengo anawakilisha jumbo katoliki LA dar es salaam tu.!
 

cleokippo

JF-Expert Member
Dec 21, 2014
985
500
bugzbunny; asante ndugu yangu yaan apo kidogo nimekupata fresh maana jamaa alikuwa anasema kwakuwa yeye ni cardinal bas ndio kiongozi mkibwa wa kikatoliki tanzania
 

cleokippo

JF-Expert Member
Dec 21, 2014
985
500
ningeiona iyo post nadhan ingekuwa poa sana shangan sababu ingenisaidia sana kuujua ukweli juu ya hili
 

Grahnman

JF-Expert Member
Oct 2, 2017
1,672
2,000
Pengo ni Askofu kama walivyo maaskofu wengine Tanzania na mkubwa wao ni Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Tanzania na huchaguliwa na wao wenyewe.......yeye Pengo ni mwakilishi wa kwenda kumchagua Papa na cheo chake anaweza kuwa nacho hata Padri yeyote......kwa hiyo Pengo sio mkuu wa Kanisa Katoliki Tanzania
 

chihe

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
255
500
Mfumo wa kanisa katoliki hauna askofu Mkuu WA Nchi Bali kila askofu WA Jimbo ana mamlaka kamili ya Jimbo lake hivyo anawajibika moja kwa moja kwa papa. Kanisa katoliki lina baraza la maaskofu hivyo wana mwenyekiti na katibu WA baraza la maaskofu hao ndio wasemaji WA baraza hilo la maaskofu kwa Nchi husika. Cheo cha ukardinari ni cheo cha uwakirishi tu WA Nchi kuingia baraza la papa kuchagua papa. Zipo Nchi zina makardinar zaidi ya wawili. Pia kardinar anaweza kuwa hata padre na Huko nyuma mashemasi walikuwa wanateuliwa kuwa makardinar.. Hivyo ndugu zangu pengo Sio Mkuu WA kanisa katoliki Tanzania mfumo huo haupo ktk kanisa katoliki.
 

mizambwa

JF-Expert Member
Oct 8, 2008
4,431
2,000
Pengo ni askofu mkuu wa dar es salaam tu! Akienda jumbo LA morogoro ni mualikwa tu Luna askofu mkuu wake. Ukadinali manaake ni anaweza kuingia kwenye conclave kumchagua papa, etc na ukardinali Ata padri anaweza kupewa .pengo anawakilisha jumbo katoliki LA dar es salaam tu.!
Mkuu uelewa wako ni mdogo, we siyo mkatoliki, nakushauri tafuta muumin mkatoliki mwenye kuelewa. Au kiongoz yeyote wa kanisa mkatoliki jiran yako

Ningekupa namba yangu lkn natumia cm siwez kuingia PM
 

ebaeban

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
2,037
2,000
Kuna masinyori(balozi wa papa) hapa nchini yupo huyu nae ni mkubwa pia
Kadrinari- Hualikwa vatican kuchagua papa
- Huwapa daraja la uaskofu wale walioteuliwa na papa
Kadrinali siyo mkuu wa kanisa katoliki bali ni askofu-kwetu ndiye askofu mkuu jimbo la dar-es-sallam
 

cleokippo

JF-Expert Member
Dec 21, 2014
985
500
ebaeban! hata mm kwa uelewa wangu mdogo nilikuwa nafaham kwamba pengo ni askofu mkuu wa jimbo katoliki la Dar, sasa kuna mtu ndio alikuwa anang'ang'ania kuwa pengo ndio kiongozi mkuu wa wakatoliki tanzania na ndio kilichosababisha niandike uzi huu sababu mm ni mkatoliki sema tu sijui muundo wa uongozi wa juu wa kikatoliki apa tz nafaham tu kidunia kuwa papa ndio kiongoz wetu kidunia bas
 

bugzbunny

JF-Expert Member
Mar 9, 2013
647
500
We IQ fupi sana! Yani unahukumu uelewa wangu kisa hukubaliani na Mimi? Kwa taarifa yako tu, Mimi ni mkatoliki hard to core, naifaham vizuri church hierarchy, kanisa siyo sum of national churches!! Kila jimbo lina autonomy we takataka, Pengo hawezi na hana mamlaka yeyote nje ya jimbo lake la dar es salaam, Pengo akiongea hawakilishi Tanzania, anawakilisha Dar! Kuna bwege mwingine kama wewe kaanzisha thread eti makao makuu ya kanisa Tanzania yaamishiwe Dodoma! Nonsense kabisa, ndo akili kama zako. Yani mnadhani pale st Joseph ndo makao makuu ya kanisa Tanzania? Muundo wa kanisa siyo national churches, hatuna individual national church, kuna had padri ni cardinal kwa taarifa yako, umegusa pabaya. Eti nikuPM? Nikupm mbumbumbu wa mwisho.shiit
Mkuu uelewa wako ni mdogo, we siyo mkatoliki, nakushauri tafuta muumin mkatoliki mwenye kuelewa. Au kiongoz yeyote wa kanisa mkatoliki jiran yako

Ningekupa namba yangu lkn natumia cm siwez kuingia PM
 

Kungun

JF-Expert Member
Dec 9, 2016
208
250
Mkuu wa Kanisa Katolic ni mwenyekiti wa balaza la maaskofu wakatolic (TEC) na Pengo n mjumbe tuu kwasababu n askof nae. Lakin yeye n mwakilishi wa kanisa katolic kdunia yaaani kama kunamamb yanajadiliwa na kuhitaj maamuz baasi yey ndo kaz yake yaaani n kama wazr wa mamb ya nje wa kanisa katolic
 

jiwe la maji

JF-Expert Member
May 17, 2014
1,065
2,000
bugzbunny; asante ndugu yangu yaan apo kidogo nimekupata fresh maana jamaa alikuwa anasema kwakuwa yeye ni cardinal bas ndio kiongozi mkibwa wa kikatoliki tanzania
Ukardinali sio cheo cha kiutawala katika ukatoriki bali ni uteule tu wa kuweza kupata nafasi ya kuwa karibu na papa.

Kanisa katoriki ni Dora moja Duniani nzima rais wake ni Papa, kimamlaka ya kiutawa ukitoka kwa Papa unashuka kwa maaskofu wa majibo ambao nikama wakuu wa mikoa alafu chini ya majibo kuna parokia ambazo nikama wilaya alafu vigango kama kata na jumuia kama mitaa.

Chini ya Papa/rais, hakuna cheo cha kimamlaka ya kati kama vile makamo wa rais, waziri mkuu au mawaziri.

Mgawanyo wa kiutawala wa maeneo wa kanisa katoriki haufuati mgawanyiko wa maeneo ya kiserikali mfano Jimbo la rulenge la yule askofu mkatoriki ngangari kama Kakobe utawala wake unaanzia Ngara mpaka Chato.
 

Mbase1970

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
6,029
2,000
Pengo ni Askofu kama walivyo maaskofu wengine Tanzania na mkubwa wao ni Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Tanzania na huchaguliwa na wao wenyewe.......yeye Pengo ni mwakilishi wa kwenda kumchagua Papa na cheo chake anaweza kuwa nacho hata Padri yeyote......kwa hiyo Pengo sio mkuu wa Kanisa Katoliki Tanzania
Ijulikane tu kuanzia papa mpaka padre wa kawaida hawana tofauti maana wote ni mapadre. Hivyo padre yeyote anaweza kusema lolote lile ambalo linahusu jamii ambayo yeye kama kiongozi wa kiroho anao wajibu wa kukemea.

Uaskofu ni mgawanyiko tu wa kiutawala kati ya mapadre. Pengo ni kiongozi wa jimbo kuu la dar ambalo yeye ni Archbishop kuna maskofu hapo dar watakua chini yake kiutawala lakini pia hana mamlaka yeyote kwao kiutumishi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom