Kwa mwenye uelewa kuhusu chaja za laptops

Kisange

JF-Expert Member
Nov 21, 2015
368
315
Habari zenu wataalam.

Nilikua naomba kuuliza kwa wenye uelewa hapa.

Nilikua natumia pc yangu nilichomeka kwenye socket ghafla nikashangaa adapta inafuka moshi na inatoa maji fulani hivi yakunuka. Nikahisi tayari imeshaungua.

Kweli nilipojaribu nikagundua haifanyi tena kazi..

Hii adopta ni ya ACER ila nina adapta nyingine ya DELL ambayo imekatika PINi ya kuchomeka kwenye tundu.

Kwahiyo nilikua nauliza je nikikata waya wa PINI ile ya ile chaji ya ACER nikiunganisha kwenye hii adapta(chaja) ya dell je vipi itaweza kufanya kazi angalau hata kuwasha tu PC iakua afadhari maana kwa sasa pesa sina..

Hebu wajuzi mnisaidie..
 
Mods samahani naomba mnisaidie kuhamisha huu uzi jukwaa la Tech nimechanganya . Tafadhari
 
Kwenye adaptor ratings kuna mahali pameandikwa Volta, Amps

Sasa angalia hiyo adaptor iliyoungua linganisha na hiyo nyingine kama zinaendana au la! Kama zinaendana sawa! Kama haziendani labda Volts ni sawa lakini Amps zinatofautiana vile usitumie maana Amps ndo inaweza kuchaji betry japo kwa umeme live inaweza kuwasha laptop lakini haiwezi kuchaji betry!

Kingine ni pini za kuingia kwenye tundu la laptop kama zinaingiliana. Sikushauri ukate waya na kujiunganishia nyaya kienyeji utasababisha short inayoweza haribu laptop yako!
 
kissange,
weka namba yako ya simu hapa au nichek 0622100690 or 06882545 kama auna ujuzi wa hizo kitu unaweza uwa battery yako
 
No retreat no surrender,
Am not una uelewa na mambo ya umeme haswa pale unapoandika amp ndo zinachaj betr afu live inawasha pc ...maelezo yako yanafanya nione kuwa uelewa wako kwa hapo ni mdogo kwan kuna umeme usio na current mfano volt 6 afu current sifuri?? Sasa kama hamna unasemaje kuna wa kuwasha na wa kuchaj?
 
kissange, angalia original chaja ilkuwa inatoa volt ngap kama zinalingana hicho ndo cha muhim then after angalia inatoa amp s ngap tofaut ya kupungua au kuongezeka haina madhara sababu pc itatumia inavohitaj tu kuhusu battery kufa sio kweli kuna saket ipo ndan ya battery pack hapo inaitwa bms ndo kazi yake hiyo
 
Mkuu nashukuru nimefanikiwa. Imekubali vizuri tu inapiga kazi nafikiri nikirudi mjini ndo nitatafuta mpya maana huku nilipo adaptor ni elfu 45 nilizoea dar 20-25
 
No retreat no surrender,
Am not una uelewa na mambo ya umeme haswa pale unapoandika amp ndo zinachaj betr afu live inawasha pc ...maelezo yako yanafanya nione kuwa uelewa wako kwa hapo ni mdogo kwan kuna umeme usio na current mfano volt 6 afu current sifuri?? Sasa kama hamna unasemaje kuna wa kuwasha na wa kuchaj?
Ila nikushauri kitu zile adpata za hiyo bei ni nyingi ni fake jitahidi upate used japo ni ghari kidogo
 
Back
Top Bottom