Kwa mwenye taarifa za uhakika tujuzeni...

Yaani sasa napata picha ngoja tumsubiri mwanaki90 arejee but leornado nisubiri niku pm
 
MAISHA: Mume ajiua kwa risasi, amjeruhi mkewe

Mume ajiua kwa risasi, amjeruhi mkewe

INADAIWA kuwa, miaka kadhaa iliyopita, mume wa Vicky aliuawa kwa kupigwa risasi, na sasa mumewe mwingine KAJIUA kwa kujipiga risasi mjini Dodoma.

Mke wa marehemu, Vicky Kaombwe (34) naye kapigwa risasi, kalazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma iliyopo mjini humo.

Polisi wamesema, mume wa Vicky, Ofisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino yenye makao yake jirani na Ikulu ndogo ya Serikali, nje ya mjini wa Dodoma, Fredy Kaombwe (28), amejiua kwa kijipiga risasi kichwani.

Kuna taarifa zinazodai kuwa, Fredy hakujipiga risasi kichwani ila kifuani.

Kwa mujibu wa Polisi, Fredy alijiua muda mfupi baada ya kumkuta mkewe akiwa na mwanamume mwingine baa mjini Dodoma.

Inadaiwa kuwa, baada ya kumkuta mkewe hapo baa, Fred alimkimbiza mkewe na walifika hadi nyumbani kwao, mtaa wa Madole , Kigamboni,mjini Dodoma, wakati Vicky akiwa katika harakati za kufungua geti akapigwa risasi iliyomjeruhi sehemu za mbavu.

Kuna taarifa kwamba, hali ya Vicky si nzuri, bado yupo hospitali.

Tukio hilo limekuwa gumzo mjini Dodoma kutokana na mazingira ya kifo cha mume wa Vicky wa awali na huyu wa sasa.

hapo kwenye kijani
MKE YUKO SAFI SS NA ANAWEZA KUONGEA

Kwenye red
HUYU MWANAMKE ANAGUNDU AU NI MAZINGARA YA KUJIPATIA MALI WAUME ZAKE WOTE WANAKUFA YEYE ANASALIMIKA NI BINADAMU WA HALI GANI HUYU! VYOMBO VYA DOLA SHERIA INASEMAJE?
 
Walah ugali ulivyo mtamu hivi sijajiuwa kwa ajili ya mananke mi ningevua gamba halafu naweka gamba.
 
Nasikia mgoni alikuwa anajiexpress jamaa kwa hasira kamlima shaba mkewe na yeye akaamua kujilipua na shaba alimfuma guest house
jamaa atakua alikua anamheshimu sana mkewe sasa alivyoona hiyo picha kashidwa vumilia,mademu mbona hivyo jamani..
 
Kwa ninavyomjua Fredy, yale maamuzi aliyoyafanya hayakutokana na wivu peke yake, mana kama kujua mkewe hajatulia alishaambiwaga toka kitambo, alikuwa anajua ila alikuwa hajafumania kumkuta live na mwanaume.

Maamuzi aliyoyafanya yalichangiwa na hasira/wivu + pombe (alikuwa ameshapata kidogo kilaji) + discipline ya umilikaji silaha (hakuwa nayo).
Unajua umilikaji wa silaha unahitaji discipline, unapokutana na situation nzito kama ya kufumania mke na una silaha kibindoni au kwenye gari, kama huna discipline unachukua maamuzi kama hayo.

Niliyojifunza:
1. Sio kila mwanamke anafaa kuolewa kuwa mama watoto.
2. Umilikaji wa silaha unahitaji discipline ya hali ya juu. Kama huna hiyo discipline, sio lazima kumiliki silaha.
 
Nakubaliana na wewe 100%.
 
snipper umesema sawasawa kabisa. influence of alcohol na pia nidhamu ya bunduki. kuna watu these days wanakimbilia kumiliki bunduki kama ujiko vile, lkn uwezo wao kuzihifadhi, kujihimili wanapokumbwa na kadhia yoyote kiakili wanashindwa na kuishia kufanya mambo kama haya. vijana jihadharini sana na katabia haka ka kupenda kumiliki bunduki
 
asanteni hatimaye nimepata taarifa niliyokuwa nataka ripoti ya daktari na makachero hakuuwawa it was a personal insult..R.I.P MY FRIEND FREDY BUT JAMAA SIATAENDELEZA NI WAZO TU.....
 
asanteni hatimaye nimepata taarifa niliyokuwa nataka ripoti ya daktari na makachero hakuuwawa it was a personal insult..R.I.P MY FRIEND FREDY BUT JAMAA SIATAENDELEZA NI WAZO TU.....

Mkuu what do you mean "it was a personal insult"?
 
duh! ama kweli huyo mwanamke dhambi hii itamtafuna milele nimemsikitia sna mdogo wangu Fredy

Engozi za Katonda,

Dhambi ipi sasa? Ya kupigwa risasi mbili kifuani? Maana "story" inasema marehemu alimkuta BAA na mwanaume, then akaanza kumkimbiza, kufika getini boom!
 
Walah ugali ulivyo mtamu hivi sijajiuwa kwa ajili ya mananke mi ningevua gamba halafu naweka gamba.

We Kimichio, temea mate chini na umuombe Mungu akuepushe na huyo ibilisi! Akili inakuwa si ya kwako, labda kama hujapenda!!
 
Ni huzzuni sana kuona namna kijana mdogo kama huyu anapoteza maisha kwa sababu ya mapenzi yake kwa mkewe.Bila shaka kuna mtu alimtaarifu kuhusu mkewe kuwa na jamaa kwenye baa fulani huko Dodoma.Kwa taarifa za gazeti la habari leo,jamaa alimkuta mkewe na jamaa baa(sio guest house)!

Ni vyema tukajua namna ya ku handle family differences no matter how stressful and painful they are!At the end of the day,u need to thank God if you come to know that your partner is unfaithful !..You just need to handle it careful .The next step is to divorce, forgive and forget her !

Simfahamu huyu bwana..but RIP
 
Poleni wafiwa, Inasikitisha sana , Alikuwa bado kijana mdogo Sana. Hatuwezi kulaumu kwasababu hatuwezi kujua mazingira yalipelekea kuchukua maamuzi hayo.
 
buriani rafiki yangu fred.
kwa wanaume wenye uchu mjue tamaa huzaa dhambi na dhambi huzaa mauti.
huyu dada alikuwa na mume almaarufu kama deo wa ifad alipigwa risasi inasemekana na wabaya wake kazini,wakati huo fred alikuwa anatembea na mke wa deo.deo tulikuwa tunaishi nae mtaa wa nkuhungu na alikuwa anakunywa baa inaitwa suzy mwaka 2004baada ya kifo chake ikabidi fred achukue mzigo jumla.
simsemi vibaya ila inasikitisha na kutia machungu.
 
Mahusiano haya ni heri mkatengana tu kuliko kuishi kwa kuviziana. Ndoa za siku hizi watu wanaishi bila uaminifu wala kuheshimiana. Poleni wafiwa. R.I.P Freddy so sad. Na huyo mwanamama mmhh!
 
acha tu masters imemgharimu maisha, halafu alikuwa anamwamini mkewe sana.Nadhani hiyo miaka miwili alokuwa Korea mkewe alikuwa ana mtu pembeni na hata baada ya marehemu kurudi bado hakuacha uzinzi wake. Kweli mwnamke hata umpe nini haridhiki.

Onyo:tuweni makini na bastola hasa unapokuw na hasira. Jamani nalia mwenzenu ofisini hakukaliki...namuona rafiki yangu Fredy all the time.

Kuna theory inasema hata mke wa tajiri mkubwa duniani,unaweza kumpata kwa kipande cha hindi la kuchoma cha Tshs 100/=!
 
Mahusiano haya ni heri mkatengana tu kuliko kuishi kwa kuviziana. Ndoa za siku hizi watu wanaishi bila uaminifu wala kuheshimiana. Poleni wafiwa. R.I.P Freddy so sad. Na huyo mwanamama mmhh!

Nionapo story za namna hii zoezi la kuowa linanitatiza sana! Wacha niendelee kuwa namega bila kuowa.
 
Back
Top Bottom