Kwa mwenendo wa Mwakyembe, Richmond tuna mashaka nayo

Mchumi90

JF-Expert Member
Mar 16, 2015
1,089
1,297
Wakuu,

Naomba nikiri kati ya mawaziri niliowaamini kwenye awamu hii ya tano ni huyu Mwakyembe. Kinachotokea sasa nabaki mdomo wazi, yeye ni mtu wa kuwaza tumbo lake tu (anauwezo wa kukataa hata jina lake huko tunakoenda).

Kwenye bunge la katiba alianza kuonesha haya mambo ya ajabu, alikuwa tayari kuwa bubu kwa kitabu alichokiandika mwenyewe kwa sababu alijua kwa kufanya hivo atakosa ulaji. Sakata la sasa la Bashite ndio kituko kingine, kila kitu kipo wazi kaja na kuanza kuikataa report ya Nape coz anajua akiongea ukweli huenda akatumbuliwa na kukosa kula.

Swali: Je hakuna uwezekano kwamba jamaa alitumwa kumchafua Lowassa kwenye Richmond kwa manufaa yake binafsi? Maana ni aina ya mtu ambaye yupo tayari kuongea uongo ili anufaishe tumbo laki.
 
"...Mheshimiw Spika, najua tatizo hapa ni Uwaziri Mkuu!" Waziri Mkuu mstaafu, Mheshimiwa Edward Ngoyai Lowassa alisikika akisema wakati akichangia Ripoti ya Kamati ya Madini na Nishati iliyokuwa inaongozwa na Mbunge wa Kyela; Mheshimiwa Harrison Mwakyembe!!

Bwana Lowassa au E.L kama wengine wanavyomwita, aliituhumu kamati hiyo kutomtendea haki huku akisema sababu ya kumchafua kote huko ni kwa ajili ya kiti cha Uwaziri Mkuu; akiwa na maana wabaya wake wanaitaka nafasi ya Uwaziri Mkuu!!

Hadi sasa haijafahamika ikiwa aliyekuwa anaimezea mate nafasi hiyo ni Bwana Harrison Mwakyembe ambae alionekana akiisoma ripoti hiyo kwa ushabiki wa wazi wazi au alimlenga Mheshimiwa Samuel Sitta ambae alionekana wazi kutumia kiti chake kushabikia Ripoti ya Harrison Mwakyembe!
 
Siku hizi CHADEMA mmekuwa na vigugumizi hasa ikitajwa skendo ya RICHMOMD na DOWANS kisa katajwa LOWASA, ila ESCROW mnaivalia kibwebwe hamna tofauti na yule ASIYEPENDA KITIMOTO LAKINI MCHUZI WAKE MNAKUNYWA SI UNAFIKI HUU. Ila katika maisha namuogopa sana mtu anayeipinga kauli yake ambayo ameitamka toka kinywani kwake mwenyewe, hivi si nyinyi kwa kipindi cha miaka nane mmemsakama jamaa ni fisadi na mkadiliki kusema ushahidi mnao, si nyie kupitia WABUNGE wenu mlikuwa mnafosi LOWASA ajiuzulu na ikiwezekana ashtakiwe sio nyinyi, si nyinyi kupitia gazeti la Kubenea MWANAHALISI mlikuwa mnaandika habari za kumponda Lowasa na mwenzake Rostam sie nyie. Alafu leo kwa KAULI ZENU KUANZIA VIONGOZI WENU MPAKA WANACHAMA WENU mnapigana na maneno yenu, hivi hamuoni nyinyi mshapoteza UAMINIFU KWA WATANZANIA sasa hivi ajenda ya ufisadi MMEIZIKA. Ila mkae mkijua mmewavunja mioyo yaywatu wengi ambao waliamini CHADEMA ni chama bora na kina watu waadilifu, kumbe wale wale.
 
Mwaki ni mtu anayeonesha kuwa anaroho mbaya sana.Anaonesha kuweka pesa mbele kuliko utu .
 
Wakuu,

Naomba nikiri kati ya mawaziri niliowaamini kwenye awamu hii ya tano ni huyu Mwakyembe. Kinachotokea sasa nabaki mdomo wazi, yeye ni mtu wa kuwaza tumbo lake tu (anauwezo wa kukataa hata jina lake huko tunakoenda).

Kwenye bunge la katiba alianza kuonesha haya mambo ya ajabu, alikuwa tayari kuwa bubu kwa kitabu alichokiandika mwenyewe kwa sababu alijua kwa kufanya hivo atakosa ulaji. Sakata la sasa la Bashite ndio kituko kingine, kila kitu kipo wazi kaja na kuanza kuikataa report ya Nape coz anajua akiongea ukweli huenda akatumbuliwa na kukosa kula.

Swali: Je hakuna uwezekano kwamba jamaa alitumwa kumchafua Lowassa kwenye Richmond kwa manufaa yake binafsi? Maana ni aina ya mtu ambaye yupo tayari kuongea uongo ili anufaishe tumbo laki.
Hata ukiwa na mashaka hairudishi usafi Wa lowasa katika saga LA Richmond na wala hairudishi uwaziri mkuu endeleen kumbadilisha majina kutoka fisadi Wa Richmond mpaka kiongozi Wa chama hah hah hah sindano mahala pake
 
Back
Top Bottom