Kwa mwenendo huu, Humphrey Polepole amepotoka!

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
125,742
239,380
Mwenendo na kauli za huyu jamaa tangu apewe ukatibu uenezi na itikadi wa CCM , hauwezi kupita hivi hivi tu bila kujadiliwa .

Mchungaji Msigwa aliwahi kumtuhumu Polepole kwa kushirikiana na Kasesera kufanya vikao usiku wa manane ili kuhujumu manispaa ya Iringa mjini , sasa naamini huyu ni mamluki mbaya sana na hatari mno.

Huyu kwa sasa amejikita Arusha kujaribu kutumia madaraka ya nchi iliyonayo CCM ili kuhujumu CHADEMA , hataweza ! ni vema akawaona hawa , Monaban , Buriani , Mrema na Yule RC aliyehamishwa ili akachote busara kwanza .

Polepole sasa amedhihirisha unafiki uliotukuka wa kujipachika hata usemaji wa familia za watu ! Hivi Kinana hana ndugu zake ambao wanaweza kumuongelea , ni lazima awe Humphrey ?
 
Kuna dharau za aina mbili mkuu, ya moyoni bila ya vitendo na ile ya dhahiri kwa vitendo we umemchagulia ipi au zote hizo?? Ila huyu jamaa kaota vibanda vya nyigu kwenye mapembe yake kwa sasa
 
Mwenendo na kauli za huyu jamaa tangu apewe ukatibu uenezi na itikadi wa ccm , hauwezi kupita hivi hivi tu bila kujadiliwa .

Mchungaji Msigwa aliwahi kumtuhumu Polepole kwa kushirikiana na Kasesera kufanya vikao usiku wa manane ili kuhujumu manispaa ya Iringa mjini , sasa naamini huyu ni mamluki mbaya sana na hatari mno.

Huyu kwa sasa amejikita Arusha kujaribu kutumia madaraka ya nchi iliyonayo ccm ili kuhujumu chadema , hataweza ! ni vema akawaona hawa , Monaban , Buriani , Mrema na Yule RC aliyehamishwa ili akachote busara kwanza .

Polepole sasa amedhihirisha unafiki uliotukuka wa kujipachika hata usemaji wa familia za watu ! Hivi Kinana hana ndugu zake ambao wanaweza kumuongelea , ni lazima awe Humphrey ?
Nani amekulazimisha uwe Chadema? Chadema ni SACCOSS ya kutafutia Ruzuku, mtaisoma Namba.
 
Completely !
Mkuu Erythrocyte,, umenichekesha eti umeamua kukadharau kwa kipindi chote katakachokuwapo nacho hapa duniani? Mkuu hako kajamaa ni kanafiki sana wewe si unakaona kalivyokaukiana? Tumekazamisha kwenye pipa la mafuta lakini hakanawili hata siku moja, mwili umekosa shukrani kutokana na unafiki wa kenyewe!!
 
Kibabu kile cha 80yrs,,,,
Mkuu mbona hata hiyo 80's umekapendelea sana,, kale tumecheza nako sembo/chandimu miaka ya 80's hivyo hako ni ka 70's. Kale ni kazee, kama mtakaita ka kijana na mimi kuanzia leo naanza kuwapiga makofi watakaoniita mzee!!
 
Siasa siasani. Siku akihamia upande wa pili mabaya yote yatasahaulika na kusamehewa kimya kimya
 
Hata nape mlimchukia hapo kabla sasa hivi mnamuita shujaa nyumbu tumeshawazoea ...
 
...

Polepole sasa amedhihirisha unafiki uliotukuka wa kujipachika hata usemaji wa familia za watu ! Hivi Kinana hana ndugu zake ambao wanaweza kumuongelea , ni lazima awe Humphrey ?

Mengine uliyoyandika ni hoja mfu kwa kuwa inakinzana na madai ya chama unachowakilisha ya 'uhuru wa kuendesha siasa'. Kama mnaona jimbo linatishiwa kuchukuliwa na CCM msikae na kulalamika tu, hakuna wa kuwabeba maana mbereko zimechanika.

Hilo nililonukuu, ni la kushangaza kwa kuwa umtajaye ni Katibu Mkuu wa Chama na msemaji ni mhusika mkuu. La ajabu ni tamko la Mh Lema bungeni kuhusu lisilo mhusu. Wewe na Mh Lema, kwa hoja hiyo, mnajitahidi kufitinisha wanachama na viongozi wa CCM.

TOENI VIBANZI MACHONI MWENU KWANZA
 
Hujui kitu , jikalie kimya tu mjomba usubiri kuvishwa fulana siku ya uchaguzi .
 
Back
Top Bottom