Kwa mwenendo huu Diamond tutamsahau baada ya miaka miwili ijayo

Nikiwa kama shabiki kindaki ndaki wa Diamond Platnumz since kamwambie hadi leo hii, nauona mwisho wa msanii huyu kuwa hauko mbali.

Diamond wa miaka miwili iliyopita siyo huyu wa sasa. Kila analogusa linaangukia pua skendo zake, kiki, na vitu vingi vya kimaendeleo hiviwi kama ilivokuwa mwanzo.

Nimeshangaa sana kiki yake ya kutoka kimapenzi na msanii wake Zuchu kuto trend na kuzima faster kama moto wa mabua, wasafi Bet nayo inapumlia mashine, Media yake haina content za kutosha zenye ushawishi imekuwa local local local.

Tukihamia kwenye kazi yake ya mziki ndo hamna kabisa anachoimba siku izi kwa mwaka mzima katoa nyimbo zaidi ya tano na zote zimezima zimekosa tension kwa mashabiki pamoja na kuzi-promote kwa nguvu lakina hazifiki kule tunapotarajia kwa kwl inasikitisha sana.

Angalizo kama mashairi yameisha kichwani ni bora atafute mtu wa kumtungia nyimbo maana anaimba utopolo mtupu. Au awekeze nguvu nyingi tu kwenye biashara zake izo zingne ambazo nazo kiuhakika zinapumulia mashine so ili kutopoteza nguvu na mtaji alowekeza kwa mda mrefu.
Chibu pafyum
 
Ww mwenyewe na shuhuda je huoni kama diamond huyu siyo yule tuliyekuwa tunamfahamu wa miaka miwili iliyopita.
Diamond wa kutoa nyimbo zaidi ya tano kwa mwaka mmoja na zote ziangukie pua, inasikitisha.
Ni kweli Mond wa sasa sio wakipindi kile alipokua anawaza tuzo
Mond wa sasa anawaza namna ya kutengeneza hela zaidi maana muziki umkwisha mmpa connections za kutosha
 
Back
Top Bottom