For CHADEMA Followers: What comes around goes around

digba sowey

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
7,892
14,347
Naomba niwasabahi wanachama wa jf,hamjambo?

Naomba niende kwenye hoja yangu juu ya wafuasi na wanachama wa CHADEMA,Naomba niweke kumbukumbu sawa, hakuna mwaka ambao chadema aliwahi kuvuna wanachama wengi toka CCM kama mwaka wa Mafuliko 2015, ambapo watu mashuhuri toka CCM walijiunga na CHADEMA huku chadema akishangilia na kujitanua juu ya anguko la CCM.

Kwa kuwa vile unavyo mtenda mwenzako ndivyo nawe utakavyo tendwa(what comes around ,goes around) Leo hii chadema amesahau kuwa wakati CCM inasikitika kupoteza wanachama wake wakongwe mwaka 2015, yeye Chadema alikuwa anashangilia, mambo yamekuwa kinyume chake chadema ameanza kulialia na kulalamika eti CCM inanunua wapinzani,hii ni hoja mfu ambayo haina nashiko na inapaswa kupuuzwa, kama ndivyo hao chadema watuambie waliwanunua kiasi gani Lowassa na Sumayi maana inaonekana wana uzoefu mkubwa wa kununua na kuuza wafuasi wa vyama.

NB: Chadema wavumilie ,huu ni ubatizo wa moto,kwani ngoma bado mbichi sana hii,kufikia Oct 2020 tutaheshimiana tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ccm ndo ilileta mfumo wa chama Vinci,hivyo pia inazo mbinu lukuki za kuhakikisha vyama uchwara vyenye kulaghai raia vinapotezwa katika ulimwengu wa siasa
CHADEMA haikununua watu ila sasa kuna madai ya watu wananunuliwa na wengine kutishwa.

Kitakachotokea ni watu kupuuza na kususia siasa na wengi kutopiga kura wakati wa uchaguzi mkuu baadae mwaka huu.

Tambueni CCM haiwezi kukubaliki kwa mbinu hizi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CHADEMA haikununua watu ila sasa kuna madai ya watu wananunuliwa na wengine kutishwa.

Kitakachotokea ni watu kupuuza na kususia siasa na wengi kutopiga kura wakati wa uchaguzi mkuu baadae mwaka huu.

Tambueni CCM haiwezi kukubaliki kwa mbinu hizi.
Hii hoja ya kununuliwa inashangaza. Wanasiasa wakubwa wakubwa kabisa eti wananunuliwa kama maembe sokoni.

Yawezekana pia kukawa na matatizo ama ya kiutendaji na hata kiulaji huko wanakopakimbia. Na badala ya kukalia kusema kuwa wananunuliwa, si vibaya pia kujifanyia tathmini kama kuna sababu nyingine inayowafanya watu hawa wazima na akili zao kutimka. Kujifanyia uchunguzi wa kina wa afya mara kwa mara kwa kawaida ni jambo jema.
 
CHADEMA haikununua watu ila sasa kuna madai ya watu wananunuliwa na wengine kutishwa.

Kitakachotokea ni watu kupuuza na kususia siasa na wengi kutopiga kura wakati wa uchaguzi mkuu baadae mwaka huu.

Tambueni CCM haiwezi kukubaliki kwa mbinu hizi.
Ndoto ya Arnacha
 
hata ka chembe ka ushahidi, tuweke hpa mkuu, siyo kukaririshwa muda woote na story ya kununuliwa, mkiambiwa mjitathimini kwenye chama chenu na kutafuta tiba ya hama hama mnakimbilia neno hilo hilo huku ushahidi hamna, nani aliyenunuliwa ukaona hela yake?
CHADEMA haikununua watu ila sasa kuna madai ya watu wananunuliwa na wengine kutishwa.

Kitakachotokea ni watu kupuuza na kususia siasa na wengi kutopiga kura wakati wa uchaguzi mkuu baadae mwaka huu.

Tambueni CCM haiwezi kukubaliki kwa mbinu hizi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mleta mada hebu nijibu hili nijue kama una akili timamu;

Hao viongozi wa CDM walijichagua wenyewe au walichaguliwa na wapiga kura ambao kimsingi ni wanachama na washabiki wa CDM ambao ndio wanawakilisha existance ya chama?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Walitumia mamlaka yao kubaki madaraka ni,rejea kauli ya mwambe,nyie watu kibano kikiwageukia huwa mnageuka hayawani kabisa
Mleta mada hebu nijibu hili nijue kama una akili timamu;

Hao viongozi wa CDM walijichagua wenyewe au walichaguliwa na wapiga kura ambao kimsingi ni wanachama na washabiki wa CDM ambao ndio wanawakilisha existance ya chama?!

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CHADEMA haikununua watu ila sasa kuna madai ya watu wananunuliwa na wengine kutishwa.

Kitakachotokea ni watu kupuuza na kususia siasa na wengi kutopiga kura wakati wa uchaguzi mkuu baadae mwaka huu.

Tambueni CCM haiwezi kukubaliki kwa mbinu hizi.
Bajeti ya ajira mpya ndio imeingizwa kwenye manunuzi , ni hela za hazina .
 
Kama wamepoteza aliyekuwa Katibu wa Chama ambaye aliletwa na mwenyekiti kuokoa jahazi basi ni wazi Chama hiki kamwe hakiwezi kuaminiwa na watanzania.

RiP Chadema.

VIVA WASSIRA kwa kutabiri haya.

Ni uwendawazimu kuamini kuwa Chadema itaweza kupata japo jimbo moja tu la Ubunge.
 
Kwa kweli Chadema imeshapitea kama NCCR mageuzi. Kosa kubwa alilofanya Mbowe ni kugombea tena Uenyekiti. Angekaa pembeni Leo hii angejizolea umaarufu mkubwa sana wa kukijenga chama mpaka kikawa chama kikuu cha Upinzani.

Mbowe ameua chama kwa akili na mikono yake mwenyewe. Kwa sasa kuna kaharufu ka kutambika tambika ndani ya Chadema na serikali ya CCM. Sasa watu wanaangalia wapi penye kondoo wa kutambika aliyenona. Wanaona bora CCM mana kuna ulaji wa nyama ya mabeberu ya tambiko.
Bora mtu ajiunge na Serikali apate posho kuliko kutambika ndani ya Chadema.

Amini ,amini ,amini nawaambia kiroho safi kabisa kuwa Wale wote wasio wa Ukanda na kabila la Mbowe watahama na kukimbilia kule kwenye serikali mana wataona ni bora tambiko la kule litawapa angalau hata Udiwani wa kuteuliwa. Karne ya 21 bado watu wanapeana madaraka kwa makabila ndani ya vyama.

Naona tunataka kutambika.

Kwa Heri Mwalimu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom