Kada wa CHADEMA
JF-Expert Member
- Feb 27, 2016
- 289
- 615
Kuna mambo yanakera sana tena yanakasirisha.
Siku zote chama chetu kimekuwa kikijinasibu kuwa ni chama makini sana. Siku zote tumekuwa tukiutangazia umma kuwa sisi ni tofauti na CCM ambao tunasema kuwa hawana dira wala mwelekeo. Tunawasema kuwa CCM wamechoka na wameishiwa pumzi.
Sasa haya yanayoendelea ndani ya chama chetu hakika manenomyetu yanatusuta. Nayasema haya kutokana na hoja zifuatazo ambazo kwa hakika zinakera na zinasikitisha.

- Haiwezekani Makada watiifu wa CCM kama Sumaye tunawateua kuwa wajumbe wa Kamati Kuu bila hata kuwa wanachama wa chama chetu. Sumaye hajawahi kuwa Mwanachama wa CHADEMA lakini leo hii Mbowe anatutangazia kuwa amemteua kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu na sisi wanachama tunaridhika tu.
- Lowasa anaitwa kuwa ni Mjumbe wa Kamati Kuu lakini hakuna uthibitisho wowote kuwa aliwahi kuteuliwa na chama kwenye nafasi hiyo, sisi wanachama bado tunakaa kimya.
- Chama kimegawanyika makundi makuu hasimu mawili na sisi tunabaki kimya. CHADEMA Asilia na CHADEMA Maslahi.
- Nafasi ya Katibu Mkuu inashikiliwa na watu wawili na sisi wanachama hatuhoji. Salum Malimu ndiye pendekezo la Lowasa na Mashinji anaungwa Mkono na Mbowe pamoja na Baregu. Wanachama tupo kimya.
- Jukumu la kuimarisha chama Mikoani tunawakabidhi watu ambao hawakijui chama; Lowasa na Salum Mwalimu.
- Mbaya zaidi, Lowasa anatangaza kuzunguka nchi nzima kuimarisha chama ameishia Monduli tu kupiga Selfie na Balozi wa Japan nchini. Hakuna Ratiba ya ziara hiyo mikoani na sisi wanachama tumekaa kimya.