tikatika
JF-Expert Member
- May 6, 2011
- 2,330
- 4,119
Sera ya awamu hii ni Tanzania ya viwanda. Waziri akasema serikali haijengi bali kazi ni kupiga sound waje wawekezaji. Sasa kwa staili hii wawekezaji watakuja?
Kwa mgeni na yanayoendelea hapa Tanzania nauliza hili baada ya tukio la rais wetu kuzuia mchanga wa ACACIA. Hofu kwa wenye uelewa mkubwa sio athari zitakazo tokea kutoka kwa ACACIA pekee, swala kubwa hapa nani atakua tayari kuweka mtaji wake kwenye nchi ambayo iko kwenye mfumo wa mpito? Tuamue moja tunaanza upya na Sera za uwekezaji au tunaendeleza zile zile? Na kama zile zile na hatuzitii basi tutegemee uwekezaji wa cherehani 4 kuwa kiwanda. Lakini kwa wawekezaji wapya na wakubwa tutasubiri sana kama kusubiri meli stand ya mabasi.
Tunachotengeneza ni hofu kwa wawekezaji. Niwakumbushe kitu. Wahindi mpaka kesho wameishiakuwa wapangaji baada ya kuwanyang'anya nyumba miaka ile. Hawana hamu tena ya kujenga kwa hofu iliyowakaa kwa takrbani miaka 40. Sio kwamba hawana hela bali hawana imani na misimamo yetu.
Njia salama ni kukaa na kujadili kwa mapana njia gani sahihi ya kunufaika na mali zetu japo tuliwapa wageni kwa kwa maandishi.
Lakini kwa mwendo huu Tanzania ya viwanda itageuka kuwa Tanzania ya vi_wonders!