Kwa mwendo huu, sijui kama ATCL itamudu ushindani wa kimataifa wa biashara ya anga

Bad timing, kwa ugeni mkubwa huu kuna vitu hatupaswi kusema.
P
Seriously, Pascal? Kuna siku unaweza ku-suggest case za kubaka watoto au ufisadi zisiwe zinaandikwa kwenye vyombo vya habari kwa kuwa zinadhalilisha taifa letu.

Unaelewa maudhi ya kufanywa usubiri airport from 10.00am to 20.00pm? Kwanza Prof amepkuwa very diplomatic. Mie ningewatukana ATC kuwa wajinga hawajui wafanyalo, kwa kuwa ni mara ya pili Prof. Mwandosya anakutana na ujinga huu. I believe ni suala la management, it could not have been a technical problem. Na hauwezi kusema kuwa ujinga huu unatokea kwa Mwandosya tu, inaonekana wengine hawauweki hadharani, eidha wakidhani ni kawaida ya mashirika ya ndege au kwa kuwa na uzalendo uliopotoka kama unavyo-suggest hapa. Kukosoana ni jambo nzuri ili kuborosha mambo. Sasa hapa Prof. alichofanya ni kukosoa ATC waone aibu na kujirekebisha, kama wana uso wa aibu lakini. Kukaa kimya kwa issue kama hizi ati kwa kuwa tuna wageni nchini borders hypocrisy. Kwani ni wakati gani Tanzania tunakuwa hatuna wageni nchini ili ndio uwe wakati muafaka wa kusema kitu kama hiki?

Kuna mtu alikuwa hajafunga zipu ya suruali na hajavaa chupi hivyo akawa exposed. Kwa kuwa hapo kulikuwa na wakwe, mtu aliyeoona akaamua asimwambie mbele za wakwe kwa kuona atamdharirisha. Akaamua kusubiri wakwe waondoke. Sasa badala ya wakwe kuondoka, na wanawe yule mtu nao wakaja. Na kisha wazazi wake. Na kisha majirani. Sasa hadi kufikia jirani kuja ikatokea kwamba kwa kutoambiwa mapema zipu ilikuwa wazi, wote waliokuwapo waliiona aibu yake. Ndipo mtu aliyemuona mara ya kwanza akatambua kwamba ingekuwa bora kumwambia yule mtu mapema mbele ya wakwe zake tu kabla watu wengi zaidi hawajafika na kisha kujua alikuwa exposed! Aibu ya kuonwa na watoto ilikuwa mbaya zaidi ya aibu ya kuona na wakwe watu wazima.

Sasa unaona aibu kwa Mwandosya kutamka hili tukiwa na ugeni wa SADC, nchi ambazo tunataka hata tuwe federation pamoja?

Just as a matter of curiosity, kipi kibaya zaidi, dunia kujua Tanzania ina wabakaji wa watoto na mafisadi au kuwa shirika letu la ndege lina matatizo ya management?

On a positive note, tweet ya Mwandosya inaweza kutoa mwangaza wa fursa kwa mashirika kupendekeza ubia na ATC ili kuliwezesha. Kumbuka KLM walitufuata kuomba tuwe wabia walipoona ATC wakati huo inasua sua, japo tuliwakatalia kwa sababu za kiwendawazimu tu wakaenda Kenya Airways.
 
Huu upuuzi nilikutana nao na Egypt Air, walikuwa na back log abiria kibao tulikuwa Heathrow. Airport management waliwaambia watatue tatizo kwani tulikuwa wengi sana Airport. Walituchukua na Airbus kufika Cairo hakuna connection ya Dar. Nilikaa Cairo siku tatu bila kupenda
Egypt Air is not an airline I would fly with even if it was the only airline left.
 
Anaandika Mark J.Mwandosya kupitia mtandao wa twitter:

I guess I am not lucky when it comes to travelling with Air Tanzania.I was booked for a 10.35am flight to Entebbe.The flight was delayed to 18.20hrs.Checked in early only to be informed the flight had been delayed again to 20hrs. Still waiting at the departure gate,full of hope.
Hili shirika kuna watu wanalipwa kulihujumu......
 
Hili ni tatizo dogo ambalo linaweza kutatuliwa bila hata kukimbilia tweeter..

Tatizo hili linayapata mashirika mengi tuu ya ndege si ATCl peke yake....

Kama Mwandosya ameona tweeter ndio atapata suluhu basi tunamtakia kila la kheri....
Sidhani kama anatafuta suluhisho bali anawataarifu wahusika na wenye mali ili wasishangae siku moja inapoonekana shirika badala ya kupanda likawa linadidimia.
 
AT LC ni swala la muda tu tumeanza kwa pupa mno ilitakiwa tujiimarishe kwanza route za ndani halafu regional baadaye ndio twende huko Bombay na kwingineko,kwa nahati mbaya sana mambo mengi yanafanyila kutafuta political mileage
 
MARK Mwandosya alikuwa waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi wa Mkapa!

Miaka ile ndio walilili run down shirika...

Leo anaongea nini huyu ?
 
MARK Mwandosya alikuwa waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi wa Mkapa!

Miaka ile ndio walilili run down shirika...

Leo anaongea nini huyu ?
 
Huu upuuzi nilikutana nao na Egypt Air, walikuwa na back log abiria kibao tulikuwa Heathrow. Airport management waliwaambia watatue tatizo kwani tulikuwa wengi sana Airport. Walituchukua na Airbus kufika Cairo hakuna connection ya Dar. Nilikaa Cairo siku tatu bila kupenda

Pole sana mkuu, mwendo wa kula kulala bila kazi ni adhabu sana
 
Mark ni mzee msomi sana na anaonekana ana busara. Aachane na mambo ya kuandika tweeter kama ana Msaada wa kimawazo anashindwa nini kuwaona atcl?
Ni bora kuwa na ucheleweshaji lakini usalama ukazingatiwa kwanza . Hata mashirika makubwa yanakuwa na ucheleweshaji. Atcl Ndiyo imetoka kuzaliwa upya baada ya kufa hata Mtoto anazaliwa anatambaa anatembea .
Enzi za Mark kulikuwa na ndege moja tena ndogo na wakati mungine kukawa hakuna ndege kabisa hata moja
 
NAIKUMBUKA ATC YA 2009. NILKOSA NDEGE YA PRECICION NIKIWA MWANZA ILIKUWA CANCELLED. NIKAOMBA WAN ITAFUTIE NDEGE MBADALA KWANI NILIKUWA NA SAFARI NYINGINE YA NJE YA NCHI KESHOKUTWA YAKE WAKANIZUNGUSHA. NDEGE YA ATC ILIKUWA NA SAFARI MWANZA DAR SALAAM JIONI SAA MOJA. MCHANA WOTE MPAKA SAA 11 JIONI NILIKUWA NAENDA KATI YA OFISI YA PRECISION NA ATC. ATC WALINIAMBAIA HAKUNA NAFASI. SAA 12 NA ROBO JIONI NIKAAMUA KWENDA UWANJANI. NIKAKUTA WATU WANAENDELEA KUINGIA KWENYE NDEGE. WAKANIAMBIA KAMA NINA PESA NAFASI ZIPO. KWENYE NDEGE HATA WATU HAWAKUFIKIA NUSU. HII NDIO ILIYOIUA ATC. NI NANI HAWA WALIOKUWA WAMEHWEKWA NAFASI HIZ MPAKA SAA 11 NA ROBO. JE WALILIPIA NAFASI HIZO WALIZOZUIA. IKIENDELEA HIVI ITAKUFA TU.


ATC ilikuwa na maadui toka ndani ya serikali nadhani ni wale waliokuwa na hisa kwenye mashirika mengine shindani
 
Mimi nilifikiri ndege zimeshindwa kuruka sababu ya mafuta,kumbe mtu mmoja alichelewesha,wapo waliohairishiwa safari british wala hawakupost kitu!
Mimi nilikuwa mshabiki mkubwa was ATCL lakini baada ya kupata experience mbaya mara 2 jambo ambalo liliniharibia biashara yangu, nimeachana na ATCL kimya kimya!
 
Hili ni tatizo dogo ambalo linaweza kutatuliwa bila hata kukimbilia tweeter..

Tatizo hili linayapata mashirika mengi tuu ya ndege si ATCl peke yake....

Kama Mwandosya ameona tweeter ndio atapata suluhu basi tunamtakia kila la kheri....
Wewe itakuwa umepitwa na ule msemo "mzaha mzaha utumbu......" huko twitter na huku kwenye mitandao ndio sehemu sahihi kusemea, wahysika ni jukumu lao kutokea ufafanuzi na kurekebisha. Kuchelewa kupo lakini isiwe ndio kawaida. Na kama wanajua kuchelewa kwa nini wasiweke ratiba kuendana na kuchelewa kwao.
 
Mwaka 2012 au 2013, kuna waziri alikuwa anaitwa Chibumunje kama sijakosea (aliwahi kupata ajali ya gari maeneo ya Singida) siku moja aliulizwa swali bungeni "kwanini ATC inaoperate huku ndege zake 2 Boeing (sijui zilikodiwa toka wapi) zikiwa mbovu, je waziri huoni unahatarisha usalama wa watu?" Akajibu "ni kweli Mh. Mbunge ndege zetu ni mbovu lakini tumeamua ziendelee kufanya kazi ili kulinusuru Shirika lisife"
 
No wonder mnakuwa maskini na kuishia kuwa wanafiki na kujipendekeza. Hakuna kitu muhimu kama muda katika suala la maendeleo wewe unasema ni jambo dogo? Nyie watu kwa nini msipate elimu hata ya kawaida tu kuwafungua ubongo? Waswahili walisema wakati ni mali.

Hili ni tatizo dogo ambalo linaweza kutatuliwa bila hata kukimbilia tweeter..

Tatizo hili linayapata mashirika mengi tuu ya ndege si ATCl peke yake....

Kama Mwandosya ameona tweeter ndio atapata suluhu basi tunamtakia kila la kheri....
 
Hahaaaa zama zmebadlika co kila homa ni malaria
Tulipokuwa wadogo tulifunzwa kukaa kimya siku kama kuna wageni. Hata kama baba na mama wamegombana na wamenuniana, akija mgeni watazuga kuongea ili mgeni asijue akishaondoka kununiana kunaendelea.
P
 
Ahsante bbe
Ruta,

Kwa dunia ya leo "cancellation" ya masaa 10 si tatizo dogo. Labda, tena labda, kama zilikuwa sababu zisizoweza kuzuilika "force majeure".

Usijekuta ni ushamba wetu wa wageni wa sadc tukachelewesha wasafiri wengine.
 
Back
Top Bottom