Kwa mwendo huu muda si mwingi watumishi wa umma watapunguzwa indirect au direct na baadhi ya taasisi kuunganishwa.

Bonde la Baraka

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
4,580
7,934
Kwema wakuu!
Kampuni nyingi binafsi zimeshawapunguza wafanyakazi wake ili kubana matumizi. Na baadhi ya kampuni zingine kuhamishwa nchini au kufa kabisa maana ustawi wake umekuwa mdogo.
Serikali ina taasisi kama 450 hivi, zipo zinazojiendesha kwa mfumo usio wa kibiashara na zipo zinazojiendesha kibiashara.
Kampuni, mashirika na wakala za kiserikali ambazo ziko kibiashara kuna possibility ya baadhi kufutwa au kuunganishwa kwa maslahi ya nchi.
Taasisi A ikiunganishwa na taasisi B baada ya kuona zinawiana kidogo kiutendaji hapo watumishi kadhaa lazima watakalishwa bench.
Hii ni forecast yangu tu na si tetesi.
 
Si jambo geni hilo!mzee Mwinyi yeye alipitisha fagio la chuma kabisa! Na ikumbukwe siku hizi technolojia inakuwa.,ajira lazima tu zipungue.
 
Kupunguza wafanyakazi haina maana kwamba huajiri. Unaweza kupunguza na ukaajiri . Ila kama itatokea kuweka watu mahali palipopunguzwa watu basi ni kwa idadi ndogo sana
Kwa hiyo sisi job seekers tutaendelea kukaa benchi.
 
Ushauri wa bure tu mkuu,ajira ni kama nguo ya kuazima wakati wowote hutoweka,Cha msingi wekeza achana na zzk eti Bata sijui ngedere huko anakudanganya tu ili umpe kura yako yeye apate kula.
 
Serikali Hii Ipo Stable Sana Sidhani Kila Jambo Linalosemwa Jamiiforums.com Linakuwa Kweli
Laa Hasha!!!! Mengine Hayana Ukweli Wowote
 
Jumla wa wafanyakazi wote wa serikali (polisi, manesi, waalimu, wanajeshi n.k) ni laki 7 na hii inchi ina watu milioni karibu 60! Hawa na wafanyakazi wachache sana nafikiri serikali ingeajiri zaidi angalau jumla ya wafanyakazi ifike milioni moja au mbili!
Kupunguza wafanyakazi kwa taifa kubwa hivi ni aibu!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom