kwa mwendo huu HATUTA FIKA N`GOO!

ThinkPad

JF-Expert Member
Apr 11, 2008
1,844
232
Nimeona kila kukicha sasa zahanati zinafungiwa ili WATU WASIPATE HUDUMA,

Ukweli ni kwamba kila kitu hapa Bongo ukikikagua kamwe hauto kosa kasoro kama ni oparation iwe nchi nzima kwa kila kitu mpaka viongozi kama kweli serikali inania ya dhati kusafisha na kuboresha maisha Yetu.

Hivi kwa mtindo huu tutafika kwa hilo wanaumiza wananchi wa kipato cha chini maana sio kila mtu anauwezo wa kwenda Mikocheni hospital, hivyo kwenye tuzahanati tudogo tudogo tunasaidia saana kwa wamaskini waliojazana hapa mjini.

Turudi kwenye Ukweli je Hao wakunga kule vijijini wanaozalisha ktk mazingira TASA mbona hawaendi kuwafungia au hakuna Dili?

Wangewafungia kwanza hao wa vijijini ambao wabebanisha wazazi huko mwananyamala...
Yaani tuombe Mungu atuepushie mbali haya mabalaa ya serikali kufunga Zahanati maana ndugu zetu watakosa sasa sehemu ya kutibiwa.


Siielewi hii Nchi imekuwaje sasa kila mtu anafanya anavyotaka Badala ya serikali kuwaunga hawa watu mkono nakuwarekebishia mazingira ya zahanati sasa serikali ndio naona imeamua KUMWAGA MBOGA hizo Zahanati zinasaidia Wananchi wa Serikali serikali haiweki mkono kwe zahanati

Nachoka.............. na haya mambo.
 
Sasa ndio tuwache tuhudumiwe katika kiwango ambacho ni substandard, kupewa madawa feki na mengine ambayo hatuyahitaji?

Tafadhalini endeleeni na kukagua na kufunga madispensari yote ambayo yako substandard. Sisi huwa tunalipia hizo huduma kwa nini wao watufanyie vitu vya kughushi?
 
Back
Top Bottom