Kwa mwana JF mwenzetu FORGIVE na wengine wenye matatizo kama yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa mwana JF mwenzetu FORGIVE na wengine wenye matatizo kama yake

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by CPU, Feb 27, 2011.

 1. CPU

  CPU JF Gold Member

  #1
  Feb 27, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  [FONT=&quot]Ndugu wana JF, heshima mbele.
  Napenda nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa Neema na Rehema zake kwangu mpaka sasa.
  Nimekuwa nikisikitishwa sana mpaka nashindwa hata kutoa mchango wa kimawazo kwa wana JF wenzetu walikumbwa na mikasa mbalimbali ya kusikitisha na ya kutisha kama huyu mwenzetu FORGIVE. Naomba sana waupokee huu msaada wangu kwao. Ingawaje nimetumia jina la Forgive ktk huu msaada wangu (tukio lake ndio msukumo mkuu) naomba msaada huu uwafikie wote wenye matatizo kama yake
  [/FONT]

  [FONT=&quot]Katika jina kuu linalotikisa falme na mamlaka la Bwana wetu Kristo wa Nazareth, katika jina litendalo maajabu la Bwana wetu Yesu Kristo wa Nazarethi, Baba wa Mbinguni, Ninaita uwepo wako mahali hapa, ninaita uwepo wa Bwana.[/FONT]

  [FONT=&quot]Asante Mungu Yesu Kristo na Roho Mtakatifu kumsaidia huyu binti FORGIVE katika vita hivi. Baba vita si vya kwake bali ni kwa Roho yako utampigania huyu binti katika jina la Yesu[/FONT]
  [FONT=&quot]Baba ninakushukuru kwa kuwa upo pamoja nae kwa ajili ya kumtia nguvu, kumsaidia, kumshika na kuwa na Mungu wake, moyo wake utiwe nguvu, katika vita hii katika jina la Yesu. [/FONT]

  [FONT=&quot]Roho Mtakatifu ninaomba uwe pamoja na huyu binti FORGIVE katika vita dhidi ya shetani na wajumbe wake. Roho Mtakatifu wewe ni mfariji wake. Pigana vita hivi kwa ajili yake na umfariji katika jina la Yesu. Siwezi kuomba kama vile uombavyo wewe. Nakusihi sema sasa ukitumie kinywa chake katika Jina la Yesu.[/FONT][FONT=&quot] Roho Mtakatifu nakuomba umuongoze na umlinde, umfundishe jinsi ya kuomba atumie kama shoka lako katika vita hivi, dhidi ya shetani na wajumbe wake. Roho Mtakatifu wewe ni mfariji wake.[/FONT]

  [FONT=&quot]Katika jina lenye nguvu la Bwana wetu Yesu Kristo wa Nazarethi. Ninaruhusu malaika wa vita kutoka ufalme wa Mungu sambaeni kila mahali sasa, mjieneze katika Anga, Nchi na Bahari, muangamize nguvu zote za giza na mumpige shetani bila kukoma, haribuni mipango yote waliyoifanya dhidi ya huyu binti FORGIVE. Ninawamuru enyi malaika na Bwana wamzunguke kama wigo sasa[/FONT]

  [FONT=&quot]Ninamfunika kwa damu ya Yesu Kristo. Ninawaloweka watu wa familia yake, ndugu zake, nyumba yake, ofisi yake, chakila chake, fedha zake, rafiki zake, majirani zake, n.k katika damu yenye nguvu ya Yesu Kristo wa Nazareth. Ninalifunika anga lote, nchi yote na bahari yote kwa damu ya Yesu Kristo; [/FONT]

  [FONT=&quot]Wewe Shetani, imeandikwa katika Ufunuo 12: 11 ''Nao wakamshinda shetani kwa damu ya Mwanakondoo na kwa Neno la ushuhuda wao '' nimetumia damu ya Yesu kukushinda sasa na hata milele katika jina la Yesu! [/FONT]

  [FONT=&quot]Ninakemea, na kufunga na kuharibu mapepo yote yanayozuia ukombozi wake na mafanikio yake. Ninaharibu kazi zenu dhidi ya maisha yake, ninawatupa wote katika giza la milele na kamwe msiweze kuinuka tena hata siku ya hukumu ya Bwana. Ninawatumia moto wa Roho Mtakatifu kuwateketeza wote[/FONT]
  [FONT=&quot]Ninaharibu kila kifuniko, minyororo, mafundo na uchawi dhidi yake. Ninauamuru moto wa Roho Mtakatifu kuviteketeza vyote na kuvifanya majivu kabisa. Ninauzimisha moshi wangu shetani dhidi ya maombi yangu. Ninatumia damu ya Yesu kuviharibu vyote, katika jina la Yesu

  [/FONT] [FONT=&quot]Wewe Shetani, imeandikwa katika kitabu cha LUKA 1:13 kusema ''Hakuna lisilo wezekana kwa Mungu”[/FONT]
  [FONT=&quot]Katika Jina la Yesu ninavunja nguvu zote za giza zilizomfunga. Ninamuweka huru kutoka kwenye nguvu za giza. Ninamuweka huru kutoka kwenye vifungo vya Uchawi, Waume wa Kipepo, Watoto wa kipepo, Makazi ya kipepo, Mali za Kipepo, Mapepo ya kurithi, Majini Bahari, Maruhani, Misukule na Mizimu, Subians, Maruani, Zakuani.nk. [/FONT]
  [FONT=&quot]Baba wa Mbinguni, ninajishusha na kumtenganisha na laana zote, maagano, mazindiko n.k aliyofanyiwa awe huru sasa, hivyo anayo haki ya kuchagua atakayemtumikia. Hakika atachagua kumtumikia Baba wa mbinguni, Yesu Kristo na Roho Mtakatifu. Awe kiumbe kipya na mpya kila siku ya maisha yake. Roho Mtakatifu yu juu yake sasa. [/FONT]

  [FONT=&quot]Atayaweza mambo yote katika Yesu Kristo amtiaye nguvu (Fil 4:13). [/FONT]
  [FONT=&quot]Neno la Mungu linasema kwa maneno yako utahesabiwa haki na kwa maneno yako utahukumiwa (Mathayo. 12:37) [/FONT]

  [FONT=&quot]Baba mfanye kuwa na haki kwa maneno ya kinywa chake kwa kuwa uzima na mauti vimo katika uwezo wa ulimi (Mithali 10:21). [/FONT]

  [FONT=&quot]Basi mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kwelikweli (Yohana. 8:36)[/FONT]

  [FONT=&quot]Kamwe hatateswa tena na Shetani pamoja na wajumbe wake kwa maana tayari yuko huru sasa, katika jina la Yesu Kristo. Amen.[/FONT]
   
 2. CPU

  CPU JF Gold Member

  #2
  Feb 27, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Feb 27, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Aaaaamen!

  Ubarikiwe sana mtumishi...Naamini yote haya yanaenda kutendekaKWA DADA FORGIVE JIONI YA LEO, katikajina lipitalo majina yote...AMINA.
   
 4. WiseLady

  WiseLady JF-Expert Member

  #4
  Feb 27, 2011
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 3,248
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Amen to that,i pray for their breakthru in the might work name.

  CPU what can i say!bless u abanduntly
   
 5. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #5
  Feb 27, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Mungu akubariki sana CPU,sala nzuri na yenye nguvu.nafurahi kuona tunaombeana hapa JF japo hatujuani.Mungu ni mwaminifu hakika atamshindia vita yake yote.Mungu atamwinua kwa namna ya pekee na atashangaa uwezo wake.Kila mtu duniani ana mapito yake ila Mungu hamwachi mwenye haki wake.Umenifurahisha sana sana na tuendelee hivi hivi.
   
 6. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #6
  Feb 27, 2011
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Amen to that CPU. I am glad umelitambua tatizo la huyu binti na kuelewa suluhisho lake liko kiroho zaidi. Naamini Mungu ametenda. Gloly be tp God,
   
 7. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #7
  Feb 27, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Inshallah!
   
 8. LD

  LD JF-Expert Member

  #8
  Feb 27, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Asante sana mtumishi CPU, Mungu akubariki utokapo na uingiapo. Ashughulike na mambo yako kama vile wewe ulivyojitoa kwa ajili ya wengine.
   
 9. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #9
  Feb 27, 2011
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Komredi hii ndo plan B mbona hujanishtua unataka kua kama TF?
   
 10. Lily Flower

  Lily Flower JF-Expert Member

  #10
  Feb 27, 2011
  Joined: Oct 16, 2009
  Messages: 2,555
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Amen, utukufu juu mbinguni.
   
 11. CPU

  CPU JF Gold Member

  #11
  Feb 27, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Komredi Mkuu hebu niPM kilongalonga chako
   
 12. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #12
  Feb 27, 2011
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Nakusalimu katika majine yote matatu!
   
 13. LD

  LD JF-Expert Member

  #13
  Feb 27, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Msasha unaharibu upako hapa lol!!
  Kwa nini umemuacha mama mlimani peke yake. Haya rudi mlimani!!
   
 14. CPU

  CPU JF Gold Member

  #14
  Feb 27, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Daaah
  Komredi bana
  Kweli wewe kiboko
   
 15. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #15
  Feb 27, 2011
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Kumbe na wewe UMO CPU? safi sana
   
 16. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #16
  Feb 27, 2011
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Tena ASHINDWE na ALEGEE
   
 17. CPU

  CPU JF Gold Member

  #17
  Feb 27, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mola wangu Mlezi (Allah)! Mjaalie na mpe uwezo, nguvu na maarifa huyu binti FORGIVE dhidi ya nguvu za shetani katika kizazi chake,
  Mola wetu! na upokee maombi yangu kwa ajiri yake FORGIVE
  Himidi zote zinamstahiki Mwenyezi Mungu, kisha rehma na amani ziwe juu ya huyu kiumbe wa Allah na kizazi chake kitakasifu kitoharifu.
  Tunakuomba Mola Mtukufu akafanye maombi haya yawe yenye manufaa kwa binti huyu, kizazi chake na hasa maisha yake ambapo wewe Allah ndio tegemeo la mustakabali wake, na tukubalie ombi letu katika kuyalinda maisha yake.

  Allah amuangazie Nuru ya Neema na Rehema zake zimfikie popote alipo
  Ewe Mola wetu! Tukubalie, hakika Wewe ni Msikivu, Mjuzi.
   
 18. CPU

  CPU JF Gold Member

  #18
  Feb 27, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Ha ha ha
  Lakin mimi nipo tofauti na wengine wengi unaowajua.
   
 19. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #19
  Feb 27, 2011
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  mshiki
  Mama kanikumbia na mimi nimeshuka!
   
 20. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #20
  Feb 27, 2011
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mh nishindwe kipi mpendwa?
   
Loading...