Yaliyojiri Ikulu: Mazungumzo kati ya Viongozi wa dini nchini na Rais Magufuli

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 23 Januari, 2019 atazungumza na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya Dini, Ikulu Jijini Dar es Salaam, kuanzia saa 3:30 asubuhi hii. Mnakaribishwa kufuatilia kupitia Redio, Televisheni na Mitandao.

=======




Rais Magufuli

Nashukuru kwa kuja, nashukuru kwa kunichagua, ningependa leo nisikie kutoka kwenu. Karibuni


Mahimbo Askofu wa Dayosisi ya Tanga Anglikana

Mashirika ya dini yanawajibika kwa raia kama Serikali inavyowajibika. Tulikubaliana tushirikiane kupitia PPT. Siku za karibuni kumetokea sintofahamu serikali za mitaa na ngazi za Wilaya. Kumekuwa na kuvutana. Utakuta mahari shirika la dini limekubaliana na Serikali kujenga Hospital. Hapo hapo Serikali na wao wanakuja kunenga hapo hapo. Kwanini wasijenge kwa umbali kuwasaidia wananchi kusafiri muda mrefu?

Nashauri kungekuwa na forum za mara kwa mara. Tukikaa pamoja ingesaidia.

Eneo la pili ni Elimu. Kumekuwa na kuvutana katika elimu za mashirika ya dini na Serikali. Tungekaa karibu kwaajili ya kushauriana.


Askofu Kissa Cheyo wa Kanisa la Moravian.

Tatizo la maji katika nchi yetu ni kubwa sana. Tulishaenda kumuona waziri mkuu akatupa mipango.

Kuna kijiji walituambia kwamba "Maji haya hata kutumia kujitawaza yanatuwasha ndo tunayo yanywa" nmewanukuu wanakijiji. Umeme tumejitahidi lakini maji ni tatizo kubwa kule chini.

Jambo la pili ni ajira. Tunashukuru kwa kusafisha wafanyakazi hewa na Vyeti. Baada ya hapo tulitegemea watu waajiriwe, lakini tunapokwenda vijijini watu wapo hawana ajira. Kuna taaluma za kujiajiri lakini zingine wakijiajiri ni hatari. Wengine wanaweza kutumia taaluma zao vibaya.


Shekh Mussa Kundecha kutoka baraza kuu la Kiislam Tanzania

Tulienda sehemu, MC akaanza kusema pale kantini ni ya Waaslam, watasali pale.. Tukajiuliza kwanini wanatutenga.. Wakajibu Waslam Wasumbufu sana.. Chakula wanauliza nani amechinja, kwenye Semina wanataka kila saa kusali. Inakuwa ni tatizo

Waislam wanataka wasali kwa siku mara tano. Tofauti na wenzetu.

Naomba kwenye shughuli za kijamii, tuweze kupata sehemu ya kufanyia swala.

Wiki mbili zilizopita tulijiwa na wenzetu waislam wa Dodoma. Taarifa ya chuo imesitisha uendelezaji wa maeneo ya kifanyia ibada. Gereda limeingia limevunja.. Hela yetu ya sadaka..

Kazi ya nyumba za Mungu ni kuwatengeneza wanadamu Kiroho.


Haidali kamburi Mkurugenzi wa hija BAKWATA taifa

Changamoto yangu ni pale tunapopata scholarship ya kuniendeleza kielimu. Ni changamoto, kumekuwa na usumbufu vijana wetu wanaposafiri pale Uwanja wa ndege. BAKWATA tunawaandikia barua wale vijana lakini wakifika pale uwanja wa ndege barua hazitambuliwi. Wengins wanaweka rockup hadi kwa siku mbili..

Sisi tunachukulia kama changamoto kwa sababu tunajua mamlaka fulani hazina taarifa. Kama kuna weakness katika hizo scholarship watuambie.


Mchungaji Aman Rimo wa kanisa ya KKKT.

Sisi wachungaji tuliomba tupate Rais kama wewe.

Mimi nlikuwa naomba kwa ajili yako. Nlikuwa nakuombea tangu ukiwa Waziri wa Ujenzi ukaja wa ardhi.

Yale yaliyokuwa yanazungumzwa na upinzani mengi umeyafanya. Unafanya kazi kubwa. Kipindi chako cha pili tuna uhakika utapita, wasisi wangu ni mwaka 2025 itakuwaje.

Nina ya kukushauri.

1. Ushauri kuhusu dini zetu.

Kipindi cha Mwalimu Nyerere kama ni dini mpya inayoanza, wachungaji na Maaskofu walikuwa wanalijadili kabla ya kusajiliwa. Hatu kwa wenzetu Waislam walikuwa na utaratibu wao.

Nashauri kuwe na kamati ya wazee ya kusaidia kusajili dini zinazochipuka.

Umekuwa na watendaji wazuri.

Nampongeza Ndalichako Wizara ya Elimu. Anafanya kazi nzuri.

Pamoja na Elimu Bure kuna changamoto bado zipo. Wazazi wanapokubaliana wanaweza kuchangia, nashauri waruhusiwe ili kuboresha elimu kwa pamoja.

Elimu ya juu kuna watoto wengi wa masikini wamekosa mikopo, wengine tunawasaidia sisi. Namuomba mama Ndalichako aangalie hili.. Kama mtashindwa kuwabaini tuombeni ushauri.

Nashauri kufanyike uchunguzi maalum, wengine wana uwezo

Naomba nishauri bima ya afya. Kule Kilimanjaro wanasema Bima ya afya haipatikani. Sijui kwa mikoa mingine.. Wananchi wengi hawana uwezo wanakosa matibabu. Waziri aangalie hili

Watanzania walio wengi wanahofuu juu ya Demokrasia. Nakuomba watu hawatachagua maneno watachagua kazi, nakuashauri waachie pumzi wazungumze.. Hawatakishinda maneno watakushinda kazi.


Askofu Gwajima wa Ufufuo na Uzima

Nimenyosha Mkono kumuweka sawa Pastor Rimo. Kwamba tuweke utarstibu wa kuanzisha madhehebu ya dini.

Bar zipo nyingi. Madhehebu yakiwa mengi ni baraka kwa nchi.. Naahauri yaongeze yahubiri kile kinachotakiwa

Kuna Askofu anaitwa Agostini Pemba. Kuna wakati kulitokea mtafaruku wa kuchinja nyama. Waziri alilitatua lakini Askofu huyu akawa muhanga na akakimbilia marekani. Inaonekana amezuiliwa kurudi hapa. Naomba utamke neno juu yake ili tuwe naye hapa

Gwajima Shekh Kundecha anaema kuhusu mahari pankuabudia ni letu sote. Wakristu na Waislam. Mfano Uwanja wa ndege kuna sehemu ya kuabudia Waislam lakini kwa wakristo hawana. Naweka sawa hili ni hitaji letu sote.

Asante Rais kwa kutuleta pamoja na Mungu atakuinua


Aurelian Ngonyani Askofu mkuu wa Truth ministries.

Nmekuwa nikipeleka watu Israel kuwsfundisha mambo ya kidini. Nakupongeza kwa kifungua ubalozi Israel.. Imerahisisha sana watu wanaotaka kutembelea maeneo matakatifu ya kibiblia kutopata tatizo.

Katika safari zangu za kwenda Israel, kuna vijana wengi wa Afrika wanajifunza kilimo cha kisasa. Israel imebadilisha Jangwa na kuwa sehemu ya kuzalisha matunda sasa inalisha dunia. Watanzania nliwakuta pale ni wachache kutoka SUA. Na wanaenda kibinafsi sio kiserikali. Naomba Serikali ifsnye mpango vijana wapelekwe waende kusoma warudi hapa.. Israel 75% ni jangwa na wanalisha dunia.

Vijana hawa wakirudi watarisha dunia.


Makamu mwenyekiti wa Jumuiya ya Mabohora

Hapa tumekutana na dini zote. Na wote tunafundisha Kamali ni haramu. Kila sehemu kwenye mitandao ni Kamali.

Atakayeshinda anapewa zawadi na mkuu wa mkoa mkuu wa wilaya na anasema nlikuwa siamini slendelea kucheza.

Nguvu kazi yetu leo inacheza kamali


Baba Askofu Gervas Nyaisonga

Kwenye elimu kuna tatizo. Vyuo vilianzishwa kwa sheria na shule zilianzishwa kwa sheria. Kuna vyuo vimezuiwa visidahili wanafunzi, na huyo anayezuia anatumia sheria.. Tunategemea ufafanuzi juu ya hili. Sisi wadau wa elimu tungekaa na waziri mkuu pia kujadili hili kwa kina.


Hasan Chizenga katibu wa Maurama

Sisi tunakuridhia na Mungu kakutengeneza kuwa madini bora. Ukiona mtu anawajali wanyonge jua huyu ni madini bora. Tunakuombea kwa dhati sana.

Ni jambo zuri sana kutuita. Naomba utuwekee misingi ya kudumu. Sisi viongozi wa dini tuna michango mizuri sana lakini hatuna platform ya kutoa michango yetu. Sijui litaitwa baraza nasaha.. Tunataka tupate sehemu ya kutolea rai ya kuendesha nchi yetu. Hili zuri uliendeleze lakini kwenye nchi yetu tupate hiki kitu.

BAKWATA kuna kitu tunacho. Tumejikuta sisi vyeti vya ndoa vinavyotolewa na RITA havitutoshelezi haja zetu sawasawa, tukaanza kuwa na vyeti vyetu vya ndoa. Sasa tupo tunavihakiki hivi vyeti katika mtindo mpya tutakaouzindua hivi karibuni.

Tatizo ni mtu tunayempa cheti chetu akaenda nacho sehemu wanasema hawakitambui. Wakitaka uhamisho wakaonesha hawakubali. Wakina mama wakienda kudai matunzo akaonesha cheti hicho anakamatwa mhusika na anachukuliwa sheria. Naomba vyeti vyetu vitambuliwe.


Mwenyekiti wa taasisi ya Markaz Tabligh makao makuu yapo Kiwalani

Anasema sisi tunasaidia Waslam, ila tunapokuwa tunazunguka sehemu mbalimbali tunakamatwa kwa kuhusishwa na ugaidi. Tunaomba utusaidie.. Sisi tunatengeneza watu wanaacha maovu.. Majambazi, mateja wamemrudia mwenyezi Mungu.

Pale uwanja wa ndenge terminal I kuna msikiti terminal II Hakuna msikiti. Walipkuwa wanajenga kwakuwa huwa tunajenga Misikiti, tuliomba kujenga msikitini. Wakatuonesha kiwanja katikati ya Terminal II na Terminal III. Tukafanya maombi pale, lakini hadi leo hakuna kinachoendelea. Kama ni kujenga Mskiti na kanisa tupo tayari. Kama wenzetu watasema wajenge Kanisa pia hakuna tatizo

Tulikutanisha Mashekh wote. Waislam tuna umoja. Sasa hatuna kisemanasemana tunaomba utambue hilo. Tuna umoja wetu waislam


Boniface Zakaria anaongoza makanisa ndani na nje ya nchi.

Sasa hivi maadii tuliyokuwa nayo ni ya nje si ya Tanzania.

Dada zetu wanavaa nguo zisizo na maadili. Wakina Kaka wanavaa nguo zisizo na maadili. Nawapongeza Waislam kwa hili, wamejitahidi sana..

Nawapongeza wenzetu Wakristo wa Katoriki. Juzi nlisikia wanatangaza wakina mama wavae nguo za Heshima.

Naomba Serikali ichukue jambo hili. Secretary wa Waziri mkuu au rais inakuta nguo zao hazifai. Makanisani tunakemea lakini ukienda ofisini unakuta mavazi hayafai.

Wazazi tumeshindwa kukemea. Kuna waziri nlienda kumtembelea, watoto wake wanavaa nguo zisizo faa.


Muhammed Mkurugenzi BAKWATA makao makuu

Matumizi mabaya ya fedha sasa hivi hamna. Hilo ni jambo zuri.

Walimu wa dini wapo wengi sana. Waajiri mashuleni ili tuweze muwaadabisha watoto wetu wangali wadogo. Tuna vijana wengi wamesoma

Mkuu wa mkoa dar kuna wakandalasi walikataliwa kwa sababu wanatengeneza chini ya kiwango. Kuna barabara kijitonyama na ya africana kwenda Goba. Ila hii ya Goba kutabomolewa msikiti. Naomba utusaidie, matofali ya pale hayazidi elfu tatu. Tunaomba mkuu wa mkoa atufikiri. Kuna mtu anajiita Mtume Hamza, sisi kwenye imani ya dini yetu Utume uliishia kwa mtu Muhammad. Tusaidie juu ya hili.


Pili Abdallah mwenyekiti wa wakinamama Waislam mkoa wa Dar es Salaam.

Wengine wanakuombea lakini mimi nasema Mwenyezi Mungu akukuze..

Tuna shule nyingi za kata, hili tunamshukuru Mungu.

Mtoto wa kata wa Kibada, anachaguliwaje kwenda kata ya mbali Pugu. Hawa ni watoto wa Masikini.

Watoto wanaanza kusoma asubuhi hadi saa moja jioni. Wataenda saa ngapi Madrasa.

Naomba Mawaziri husika nao waende kukutana na viongozi wa dini. Tuna mengi kama tungempata waziri Husika.


Doctor Panasekra mkuu wa madhehebu ya budha Africa

Nlichukua uraia wa Tanzania miaka minne iliyopita.

Sisi kama budha tunaweza kusaidia mambo mbalimbali

Nje ya mji comittee yetu haitambuliki.

Kuna watoto barabarani, sipendi kuwaona.. Tusiruhusu watoto kifanya biashara barabarani. Ni vibaya.. Tutafute namna ya kuwasaidia.

Barabara zetu zinasikitisha hasa pale Jangwani. Mvua ikinyesha maji yanajaa.. Fanya kitu pale.

Polisi wanatusumbua sana barabarani.

Pugu Sekondari tangu Nyerere ipo Vilevile.

Rais tunaomba huduma ya afya iwe bure.


Askofu Mwingira

Naomba ushirika wa Serikali na viongozi wa dini uwe kati muondo huu. Sisi tunaongoza Serikali ya Mbinguni, ninyi Serikali ya binadamu.

Umechelewa kutuita. Ilitakiwa tukutane pamoja tupange pamona Sera ili tuitekeleze pamoja. Peke yako huwezi

Miundombinu ya taifa letu inaleta kizungimkuti. Hatina mipango ya miaka 50 hadi miaka 100. Ni vizuri tiweke mikakati katika miundo mbinu hivi. Watu wa barabara, umeme, maji, wakae pamoja wajadili kila mtu atapita wapi. Mipango miji ni ya Mungu na vurugu za shetani. Hata kama hatuwezi lipa, lakini watu wajue hapa kutapita kiti fulani.

Viongozi wetu wa Wilaya wanatia watu Rockup. Unamuweka mtumishi wa Mungu ndani kule Sengerema wakabomoa na kanisa. Ukipiga simu anamuachia. Tunaomba viongozi wetu wa Wilaya tusifsnye hivyo. Unamuweka mtu ndani himfungulio mashitaka. Unamuabisha. Mengine mtaongea na wewe binafsi ukinipa nafasi.


Kasim katibu mkuu Ismailia Tanzania

USALAMA.

Yaliyotokea Kenya sio mazuri.. Tunawaombea kwa Mungu. Ukiona mwenzio ananyolewa wewe kaa macho.

Tunazo kamati za mikoa na viongozi wa dini tupo. Mambo kama hayo ni sababu ya watu kukosa kazi, ajira na elimu.

Kwa upande wa Serikali iangalie hii kitu. Tuna jukumu la kukaa na vijana wetu kama wazazi na viongozi wa dini


Riona Kimaro wa KKKT Kijitonyama

Unafanya kazi kubwa katika uchumi. Mimi ni mchumi. Ni vizuri muwe mnatushirikisha.

Katika Swala la Viwanda: Hatuwezi kuwa na Viwanda bila kilimo. Kilimo kwa kutegemea mvua peke yake ni vigumu. Na tanzania hii maji ni shida vijijini katika nchi hii na dunia maji yanapungua. Nchi hii tuna maji hadi yanaleta uharibifu. Haya maji tukiweza kuyatumia yatatisaidia sana. Kwanza kuongeza ajira

Pili Soko la nje ni muhimu sana kizongatia katika ulimwengu wa Viwanda.

MAJI

Tanzania hatuvuni maji ya mvua.

Botswana hawana mto wala mfereji na ni jangwa, lakini wanavuna maji ya mvua na wanalisha dunia nyama kwa ufugaji wao.

Ombi langu. Bahati nzuri una vichwa. Kama tukiwa na uwezo wa kuwa na kauli mbiu kila mkoa kuwa na bwawa moja. Tutatunza barabara, haya mabwawa tunaweza kufuga samaki. Tutaanzisha kilimo cha umwagiliaji. Lakini sasa tunayaachia haya maji yanatusumbua na kutuletea shida. Haya maji yakitumika vizuri, vina watazalisha.

MASOKO YA NJE

Hauwezi kiwa na Viwanda bila masoko ya nje. Nlienda Nairobi nikakuta wanaandika tunapika mchele wa Tanzania. Juzi tulitangaziwa kwamba tutapika mchele wa Tanzania. Tafuta watu wakatafute masoko ya tanzania.

Kumpeleka mtu aliyesoma uchumi kwenye Masoko ya kwa sadala, Mwanjela kulumba ni kumdhalilisha. Masoko yetu ya ndani hayatoshi. Tutafute masoko ya nje. Tunatamani kuona soko la pamoja nchini. Tafuta think tank. Kasi ya soko la nje ni kilio


Mchungaji Esther Mkasa wa Boko.

Sisi huku nyuma tunakuombea sana. Tunakupongeza mno. Tunaiombea familia yako.

Tunaosafiri na Mabasi tunakosa sehemu ya kujisaidia. Imekuwa ni kero.

Tunahitaji Sehemu za kuomba sehemu Muhimu kama uwanja wa ndege.


Naibu katibu mkuu wa SUNI

Tuna tatizo ya hizi kadi za Ujasiliamali. Tuna wakina mama 32 wanafanya ujasiliamali lakini tumeorodhesha kwa afisa mtendaji wamesema kadi zimeisha. Tuna wanachama 37{rais ameingilia na kusema hizo utazipata leo)}


Bishop Jenny Muhege

Nlikwenda likizo nikakuta kuna mila zinatesa Watanzania. Bado kuna watu wanathubutu kupiga mwanamke. Unakuta anachapwa hadharani mbele ya watu wote. Baba analazwa chini anachapwa kwamba amefanya kosa fulani. Tafuta namna watu wataenda sehemu nyingine.. Kwamba kuna watu wanasema mzee akikasirika atatoa laana.

Mchungaji Vernon Fernandes

Wewe ni kama mtume. Unafanya kitu wengi e hawajafanya. Mimi nmekuwa naiombea nchi hii tangu 1979. Mimi ni. Mchumi, tangu 1982 niacha kazi nikaanza kumtumikia Mungu. Nchi hii sio Masikini sisi ni Tajiri. Marais wote walisema nchi ni Masikini lakini Mungu akakufungua macho na ukaona ni tajiri

KAMA UNATAKA TUWE TAJI

1. Ni kilimo. Mungu alimuweka Adam kwemye bustani alime.

2. Madini. Kwenye biblia imeandikwa mwanzo sura 2. Mungu kwenye bustani aliweka dhahabu safi.

3. Utalii. Mungu aliwapa Adamu na Eva uhuru wa kutaja Wanyama. Huu ni utalii. Kila mtanzania anaweza kupata milioni

Kanuni ya Mungu haibadiliki.

Zaka. Kikumi ni cha Mungu. Tukigusa titakuwa na laana. Laana inakuja ndani ya nchi.

Kama kina wezi ndani ya kanisa hata nje kutakuwa na laana. Hii laana ikilndolewa tutakuwa donor County.

Sisi tunashaidia nchi na hatuma matangazo lwenye vyombo vya habari. Sisi hatufanyi biashara.. TCRA wametunyang'anya leseni. Watu wanataka tulipe sisi tuna waumini.


Jabir Muruba naibu katibu mkuu Bakwata

Sisi ni Walinzi wa amani ya nchi wasiotumia Silaha bali neno la Mungu.

Naomba tudumishe haya mawasiliano ili serikali wananchi na Wanadini katika sehemu yao.

Chuo kikuu cha UDOM limekuja katika sura si nzuri. Mfiti wa Tanzania alitembelea hiyo sehemu ambapo patajengwa Msikiti. Ulijengwa baada ukavunjwa. Kuvunjwa kake sio kuzuri. Tumelituliza lile jambo ili tulitatue kwa namna yenye afya. Baadae tuonaomba tulipatie ufimbuzi.

Maeneo ya ibada yanayosemwa yatengwe na yaoneshwe na yaheshimiwe kwa dini zote.

Elimu bure imesaidia watoto wengi wa masikini. Sisi mashirika ya dini tunasaidia ndugu zetu. Wale wa serikali ikifika kipindi cha mitihani wanapanga hadi gharama za mitihani. Wale wa Serikali wanalipiwa na Serikali. Naomba hawa private nao walipiwe na Serikali.

Hawa viongozi wa chini nao wafanye kawa wewe kuwepo hii Forum.


David Mwasota askofu mkuu Pentekoste

Sisi tuliunda baraza na mabaraza wengine walitukibali. Siku tatu tuliomba na tukaorodhesha sifa za rais tunauemtaka.. Ndo hizo ulizo nazo.

Sisi pama Pentecost tuna changamoto kwenye vyombo vya habari vya taifa hatupewi nafasi. Tulienda kwa Waziri mkuu hatukupata usaidizi sawa sawa. Makanisa yanakosa nafasi ya kupeleka ujumbe wa Mungu. Mkutano kama huu unaweza kutupa mwafaka.

Tunashindwa kupeleka elimu kwenye shule zetu. Tunhependa kupata utaratibu pa kuanzia ili tukawafundishe watoto wetu.


Mchungaji Sizza

Uchumi wa Viwanda unawezekana. Kwenye viwanda kuna Vitu viwili biashara na uzalishaji.

Mimi naona tunaweza kuanza na kitu kingine. Mimi ni mfanya biashara. Hatukuamza na Kiwanda bali tulianza na biashara.

Tutengeneze chombo cha watu wenye ndoto ya kutengeneza bidhaa. Kimjenge na kumtengenezea kivuli.

Adhima ya nchi hii kwenda kwenye viwanda itafanikiwa.


Mchungaji Jacob Mtashi wa EAGT Mwanza

Maadili yamemong'onyoka. Sisi ndio tuna watu tuisaidie Serikali. Tujikite kwenye malezi ya watoto na ndoa. Tuwe na mafundisho kwa vijana.

Sura hii kama ulivyotuita, inafanyika kitaifa. Sasa hii ifanyike hivyo kadi kiwilaya. Kamati za mikoa za amani zinafanya vizuri sana

Shehe Mzee wa jumuia ya Gongo la Mboto tunajihusisha na kuhibiri dini ndani na nje ya nchi. Tunakukaribisha katika jumuia yetu.


Kassim Mwalimu wa Kiwalani

Tunapata changamoto kibwa kwa wazazi kuleta watoto. Kuna watoto ambao hawawezi kiendelea katika masomo ya shule. Wanaletwa elimu ya dini. Isiwe kwa upande mmoja.

Dar ni ndogo lakini haipanuliwi.


Father Kitma, Katibu wa baraza la maaskofu Tanzania

Tunapongeza serikali kwa kupiga vita rushwa, madawa ya kulevya, kutambua tunu za binadamu. Sisi ti apinga ndoa za jinsia moja.

Tunaomba serikali kuhusu elimu wakae na wazazi wapange future ya watoto wetu vizuri. Kwenye elimu huwa hatutabiriki katika sera zetu.

Serikali imeajiri mil 2 lakini nguvu kazi ipo zaidi ya mil 20


John Mchopa wa Kanisa la Biblia Tanzania

Naungana na waliokupongeza.

Nina mambo mawili

1. Kuomba rasmi. Kule tuna hospital ya kiuma. Tunaomba wale madaktari ambao tumewaajiri wakipata ajira Serikalini wabaki pale kwaajiri ya kusaidia Tanzania

2. Kuhusu korosho. Jambo ulilolifanya ni zuri lakini kuna dosari. Uhakiki haifanyiki vizuri. Kuna hata wakulima wa kilo 100 hawajalipwa. Naomba hili jambo la uhakiki liende kwa haraka. Dhamili yako ni njema lakini kwenye kutenda kuna watu wanapenda kuumiza watu.


Askofu Manaso

Chuo cha Mount Meru kuna unadhilifu kwa upande wa Serikali na kanisa Bil 3.3 zilichukuliwa. Tunaomba utusaidie.. Sasa chuo kinataka kuuzwa. Nlishamueleza mkuu wa Wilaya na Waziri ndalichako.

Leo hatuwezi kudahili na waliotufikisha hapo wapo.

Rais: Nani alichukua hela?

Askofu Manasa: bodi na aliyekuwa mkuu wa chuo. Watendaji wa chuo


Dr. Leonard wa EAGT Arusha

Haya tunayoyaona ni lashalasha ma masika yanakuja. Nimefurshishwa na unuenyekevu wako. Hata wakitaka uendelee ndani ya miaka 10 wewe kibali tu. Nmefurahishwa ma moyo waunyenyekevu

Wakati umefika kwa Serikali yetu tuhame hii siku ya jumapili. Wakristo wengi wanakosa haki yao ya kuchagua. Kama itakupendeza isiwe siku ya jumamos wala Ijumaa. Hilo ndo ombi langu.

Hali ya kubalance kwemye dhifa za kitaifa. Pentecost tupo hata kabla ya uhuru.

Serikali imefika mahali ianze kutoa zaka kwa viongozi wa dini.

Rais: Sio kwamba hizo zaka tuzipike Tax?

Daniel Moses Kulola kutoka Mwanza

1. Endelea kuwa na roho ngumu ya kufanya maamuzi magumu kama ulivyo sema Tanzania hakuna njaa.

2. Washirika wanapofiwa wamekuwa wanalia. Sababu kubwa ni Sheria za mirathi sababu hazijakaa vizuri.

3. Kuna watu wanasema wanakula raha hapa Tanzania kwenye nchi ya Wajinga. Umebadilisha mengi.

Kuna nchi nilienda, nikakaribishwa. Yule rais anaalika mabaraza yake anawaita watu wa dini wanawahubiria.

Watendaji wakiokoka wanakusaidia wewe.

Wewe ni Mwanaume. Mungu akubariki.


Alfonce Temba kitoka Kibaha

Mimi nmeleta mfanyabiashara wa Thailand. Wapo tayari kuleta soko la madini hapa nchini. Tatizo Thailand hakuna ubarozi wala hapa Tanzania.

Kwa upande wa utalii kule Kilwa Vunjo na njia zote zilizofungwa zifunguliwe

Katoro kuna nyumba ambazo Masaki hakuna.. Madini yanatoroshwa sana.


John Wambura kutoka Musoma

Mugumu mwalimu Nyerere aliomba tujenge Hospital. Wafanyakazi wetu pale hawapandishwi madaraja.. Mkataba hausainiwi. Hivi karibuni umeletwa malimbikizo kwamba tunadaiwa kodi ya ardhi. Sisi hatuna hata hati. Ile nyererw ndo aliagiza. Sasa kumeingia siasa eti wanajenga hospital yao.

Askofu alikabidhi Serikali sisi tunataka kukirudisha.. Hatuna hati ya yale majengo ya chuo. mennonite tulikuwa na shule nyingi sasa hatuna.


Michael Ndonya wa Dodoma wa kanisa la Baptist

Mimi nashukuru kwa kutuita. Wanasiasa wanapokuchosha tuite viongozi wa dini tutakufariji. Watendaji wa Ikulu ni watu wema, wametupokea vizuri.

Nampongeza Lugola anafanya kazi kubwa. Ila namuomba ukiona huko kwenye dini kuna mambo tuote tukae.

Tamisemi Jaffo anafanya kazi kubwa. Kuna mikanganyo juu ya ada. Leo vyombo vya habari vinaongea hivi. Simu za Askofu Mawaziri hawapokei.

Mnapotokea kauli zenye Mikanganyo mtoe taarifa mapema kama Ikulu inavyofanya. Nampongeza Gerson Msigwa.


Brown Mwakipesile Askofu Mkuu EAGT.

Tunakupongeza sana. Asante kwa kuhamia dodoma.

Asilimia kubwa ya waoongea wanampengeza sana rais. Amefanya kazi kubwa. [sababu wanarudia maneno yaliyokwisha kusema sijaandika ntaandika kama kuna kipya hakinaongelewa]


Matumora wa Tunduru

Hakuna ukwezeji wa kimaendeleo uliofanyika kule kusini. Katikatika ya Nyasa na Selous hakuna anayetukumbuka. Tupo isolated sana..umasikini utaendelea.

Tulishasema sana hadi Mheshimiwa Pinda alitubatiza jina na kusema atatupa mkoa unaoitwa Selous.

Masasi na Songea pale katikati pametengwa mno. Tunajua ulishasema haya mambo ya Mikoa tukuache kwanza lakini jaribu kutukaribia kule. Samahani kwa kusema hilo. Kule watu ni wanyonge sana.

Method Constantine natokea Geita Wilaya ya Chato.

Wewe rais ni sawasawa na Gedion wa kwenye biblia.

Naomba msaada wako kwa hivi vikundi vya wakina mama wanaochangiana wasamehewe ushuru


Shekh Hamis Nassoro kiongozi wa maimamu Chalinze

Rais Magufuli uliyosema kwamba sitawangusha ni kweli tunaona hautuangushi. Ulipambana na ufisadi na uongo. Taifa likiwa na watu wakweli wachamungu analitengeneza.

Viongozi wote wa chini watambue kama kuna kiongozi wa dini kama unavyofanya wewe.

Jaffo na Makonda wanafanya kazi kibwa. Wanaivuta Serikali gari zima linavuta gari bovu. Maji ni Tatizo kubwa Chalinze. Mradi wa maji wa Wami ni jipu bado tunanunua ndege tunafika mbali sana.



HOTUBA YA RAIS MAGUFULI

Waheshimiwa sana viongozi wa dini. Narudia tena kiwashukuru sana kwa kija kiungana nasi hapa. Ikulu ni ya Watanzania wote, haina dini, chama wala Makabila. Kwahiyo nmeshukuru sana. Viongozi wa dino mliochangia mpo 42. Kujibu mmoja mmoja muda haitatosha. Ila michango yenu uahauri wenu yote tumeichukua.

Baba askofu wa Tundulu amezungumzia Korosho. Nmetoa maagizo kwamba waziro wa kilimo na biashara wahakikishe hasa wakulima wenye kilo ndogo ndogo walipwe wote. Kamati za uhakiki za korosho washirikiane. Wakague maeneo. Wasaini watu walipwe kutokana na sehemu walipo. Wasikae wanawachelewesha watu kulipwa. Narudia tena.. Nataka wakulima wa korosho walipwe mapema na fedha zote zipo. Lakini kwa mashirika kama ya dini, katibu tarafa anafahamu mkuu wa wilaya anafahamu wasaini mlipwe.

Kwenye hili la kuwa na Mkoa la Baba Askofu Matomola...

Kutatua matatizo sio Mikoa na Wilaya, kule ni kuwapa ulaji watendaji wa Serikali bali kuwapelekea huduma. Mfano bado km67 za barabara hazina lami. Zamani kutoka songea namtumbo na kila sehemu hamkuwa na lami. Mimi ninaamin kuliko kuanzisha mkoa, zile fedha bora ziwasaidie. Namtimbo kuja Tunduru maeneo yanazungukwa na Selous. Nafahamu wengi wa Tunduru ni Waislam ila sio kigezo cha kuwa mkoa. Sisi watanzania hatuna ubaguzi.

Vita vya makaburu ndo vilisababisha hayo maeneo yasiendelezwe.. Ilikuwa sehemubya kupigania. Serikali ipo pamoja na watu wa tundulu. Barabara zaidi ya km 600 zimeisha. Haya ya mzee Pindi inawezekana aliahidi wakati anataka kugombea Urais. Sijakataa hili swala lakini kipi kitangulie? Kupanga ni kuchagua

Kuna swala limezungumzia juu ya Elimu na afya. Taasisi za dini zonamiliki Zahanati 791 vituo 160 hospital 116, vyuo vikuu 14 vyuo vikuu vishiriki 12. Tutaendelea kutoa mikopo.

Tukibaini elimu inayotewa haikizi viwango chuo tunakifungia. Ilifikia mahali kila mmoja anaanzisha chuo kikuu. TCU ilikuwa inapangia watu baada ya kuacha wanafunzi wajichagulie. Pakatokea rushwa mpaka bodi ya chuo kikuu nikaivunja. UDOM Wanafunzi zaidi ya 7628 kidato cha nne walipelekwa kudahiliwa, wote tuliwafukuza tukawapeleka wanapostahili kusoma.

Kampala University walikuwa wanafanya udanganyifu.

Kwenye elimu bil 427 zinatolewa kama mikopo. Kuna watoto wa masikini wanakosa mikopo ni kutokana na walivyojaza fomu zao. Tangu vidudu upo private hadi form six, ukienda chuo si rahisi kukusikiliza. Tunafanya hivi tusijesomesha watoto wa Waziri mkuu

Kuhusu swala la Misamaha ya kodi kwa taasisi za dini halijafutwa linasimamiwa na sheria.

Misamaha ya kodi ni sehemu moja wapu watu walikuwa wanatumia kukwepa kodi. Kutambua hilo, Serikali ikafuta mianya yote ya kodi. Taasisi za dini pale zinapositahili watapata bil 16.66 zilitolewa kama msamaha 2016. Mwaka 2017 bil 17.6, Mwaka jana bil 46.84.

Wengine tunawasemehe wakifika kule wanafanya biashara.

Mishahara itaendelea kutolewa.

Kuhusu Demokrasia

Nataka niwahakikishie ndugu zangu Demokrasia ipo. Demokrasia sio kirihusi maandamano tu. Demokrasia ina mipaka yake.

Mumekuwa mkitembea kila mahala, sijui kama mnaona maandamano. Tukifanya hivyo tutashindwa kutawala. Uchaguzi ukishaisha wale waliochaguliwa ndo wanafanya mikutano. Tunazuia ni katika kutunza amani.

Tunataka vyama vyetu viheshimiane kama dini zetu. Mtu asiende kutukana kwa mwenzie. Hakuna mtu aliyekatazwa kufanya mkutamo mahali alipo.

Walifanya mikutano dar es salaam hapa. Hakuna mtu aliyezuiliwa kifanya mikutano. Iliyokatazwa ni kwenda kufsnya mkutano kwenye jimbo la mtu mwingine. Kila mtu afsnye mkutano mahali pake. Kama wa Ubungo afsnye ubungo. Hakuna aliyemzuia mbowe kifanya mkutano jimbo la Hai. Kila mtu afanye mkutano kwenye eneo lake. Baada ya miaka 5 wakipewa uhuru wa kizunguka na kutukana wafanye hivyo.

Unapochaguliwa manaake umepewa nafasi katika mida wake wote.

Maji

Suala la maji limekuwa na changamoto na changamoto hazikuanza mwaka huu.

Tunatengeneza miradi mipya ya maji. Ile ya zamani iliwatosha wale wa zamani kwani nchi imepata uhuru wakiwa watu mil 10.

Mliyoyasema ni muhimu sana. Nawashukuru. Kuna taasisi wanatangaza dini na wachimba visima. Na ninyi niwaombe chimba hata kisima hapo kanisani au msikitini. Kwenye zile sadaka zinazotolewa, chota kidogo chimba kisima.

Ushauri wenu mlioutoa ni muhimu na tumeupokea wote na nimekubaliana na ninyo.

Kama nlivyokutana na nyie, wakuu wa mikoa, wakuu wa Wilaya na makatibu tatafa wafanye hivyo hivyo. Wakijenga tabia ya kiwaheshimu viongozi wa dini tutafika mbali. Tatizo tunakuwa watawala mno. Naomba mzidi kuniombea nisiwe na kiburi. Nafanya kazi yangu kama mtumishi sio kama mtawala. Uongozi unawapa wati viburi, anajiona yeye ni yeye.

Waziri wa elimu waziri wa tamisemi anaweza akawatafuta.. Wakisolve matatizo haya wanapata baraka. Nakubaliana na ninyi.

Matatizo tunayakuza kwa kutoyatatua. Matatizo ya viongozi wa dini yatatuliwe. Saa nyingine tunajipa laana.

Na ninyi mtusaidie kwa waumini wenu jui ya hili la maadili. Swala la mitandao limeharobi kanuni na taratibu za kibinadamu. Hii mitandao ni kama panga. Ukiitumia vizuri u apata maendeleo ukiitumia vibaya unajikata mwenyewe.

Twende mbali na hapo wasiovaa vizuri sio wasiruhusiwe kanisani bali wasiruhusiwe mahalinpopote

Nashukuru waumini wa Kakobe hawataki kuonekana nywele japo nywele za kakobe tunaziona.

Hili la kamali tumelisikia na waziri mkuu amesikia.. Hii inajenga tabia ya uvivu na tabia kutokufanya kazi. Kamali ni mbaya hata kwenye vitabu vya Mungu. Lakini huwezi kujua.. Ukute shehe au mchungaji kashapata tatu mzuka.

Kikao kama hiki ntakuwa nakifanya ikiwezekana kila mwaka. Leo nmekuja na Mawaziri wachache, siku nyingine ntakuja nao wote na kamatibu wakuu wote.

Nchi ni yetu sote na tukiharibikiwa tutaharibikiwa wote.
Nawashukuru sana

Umimi unaweza usilipeleke kuzuri taifa hili.

Nlienda Kigoma Mguruka nlimkuta Baba mtakatifu Eliya amejenga hospitali akaikabidhi Serikali. Tukatoa vitanda.

Natoa mfano ifakara st. Francis gharama ni kibwa kuliko kituo cha pale wakati madaktari wanalipiwa na Serikali. Sasa, wananchi wananchagua. Gharama ni kubwa. Mfano Bugando hospital asilimia kubwa inalipiwa na serikali lakini pamekuwa na wizi wa ajabu. Wanabishana kumfanyia upasuaji kisa 3000. Kina sister pale alijiua. Watumishi wa kule wanafanya kazi za ajabu. Waliouza mali za bakwata ni Waislam.

Pale Bugando wameenda Maaskofu wakashughulikia haya mabaya. Taasisi tunazoziongoza tukazisimamie watwkeleze maelekezo mnayoyapa. Lengo liwe kuwasaidia wananchi masikini.

Nmeyasikia yote na ushauri nmeubeba.

Karibuni kwa chakula lakini tuwasubiri wenzetu Waislam waende kuswali.

Asanteni sana
 
1) Shida zinazoikabili Nchi...

A) Visasi

B) Chuki

C) Ubaguzi

D) Uonevu

E) Haki za Binadamu

2) Mkifanya Mkutano wenu uwe jukwaa la kampeni, kusifiana Mkasahau shida za waumini wenu Ole wenu TUTAPOTEZA IMANI NA NYIE WOTE MDA NI HAKIMU MZURI SANA KILA LA HERI

Mwanahabari Huru

Kwa niamba ya Watanzania wote
Hoja yako nzuri. Lakini nani amekuteua kuwakilisha watanzania wote?
 
Kama ni hizi dini za wazungu na waarabu, ambazo dini moja viongozi wake wakipigania haki wanaitwa MAGAIDI.
 
Back
Top Bottom