Kwa mujibu wa Zitto, hiki ndicho kiwango cha akiba ya chakula Tanzania

Hivi ndivyo alivyoandika Zitto kupitia mtandao wa twitter:

Mwezi Oktoba mwaka 2015 Taifa lilikuwa na Akiba ya Chakula Tani 253,600. Tangu Serikali ya CCM ya Awamu ya 5 iingie madarakani haitengi Fedha za kununua chakula cha Akiba na ilichokikuta iliuza ili kununua Ndege. Sasa kuna akiba ya Tani 55,000 tu sawa na kilo 1 tu kila Mtanzania.

Zitto alituambia kwamba CAG Mstaafu Pro.Asad haonekani, vipi mbona hajatuhabarisha kama keshaonekana au la?
 
Mndali ndanyelakakomu, akula ya taifa, wewe unaorodhesha majina ya watu hapa, zimo kweli wewe??

By the way, Zito katoa maoni yake kwa kuambatanisha na takwimu za akiba ya chakula kwa mujibu wa NFRA wenyewe ambayo ni taasisi ya serikali, yet unakuwa bado huelewi tu na unataka tumjadili Zito badala ya takwimu??

Ungeeleweka sana tu kama ungemshambulia Mh Zito Kabwe kwa kukosoa takwimu alizozileta kuwa ni za uongo na badala yake uweke zako za ukweli na kisha watu tupime....

Lakini hujafanya hivyo, badala yake unawaka hasira na matusi ya kumtukana mjumbe....!!

Hili tu linaonesha na kutoa picha wewe ni binadamu wa namna gani kabla hata mtu hajaona sura yako, kwamba, ni kiumbe usiye na ufahamu, uelewa wala hoja katika meza ya majadiliano....!!
 
Hivi hapa hoja ni zito au akiba ya chakula,mkuu nisaidie na mie nielewe ili nichangie hoja
Hoja ni zote mbili zitto na akiba ya chakula


Maanake tunajadili mpaka chanzo cha taarifa ili kujiridhisha na ukweli wake

Na tunajadili taarifa baada ya kujua chanzo ni sahihi au sio sahihi
 
ZZK ni mpiga dili tu na wakala wa mabeberu, hii nchi ni tajiri na awamu ya tano imewezesha uchumi kukua kwa zaidi ya 7%, pato la Mtanzania limekuwa pia, mabarabara kila kona, Madege angani, SGR, Stieggler's.

Huyu ZZK ndio wale wanaomkatisha tamaa Rais wetu JPM kipenzi cha wanyonge wa nchi hii, nchi imeliwa sana hii JPM anainyoosha balaa..
Hahaah uchumi unakua mbn hawez kuajil ila anaeeza tu kufkza wafnykz hew Mbn hamuongez mshara naona mmejfch nyuma ya stglas ,SGR na ndege ambazo iyo mirad ni pesa za mkopo den la Taifa from 25 to 54 mi naona uchum haukui tuwen wawaz tu co aibu kua muwaz
 
So ajabu ndio maana wananchi waliambiwa kauli za kifedhuli kabisa kuhusu bei za chakula na huyu jamaa. Maana kwa hali ya kawaida kukiwa na upungufu unaopelekea kupanda kwa bei za chakula, food reserve ndio ingepunguza bei kwa kuwauzia wafanyabiashara kwa bei nafuu . kumbe kelele zote zile Ni kwa kuwa food reserve imekauka. Huyu jamaa hafai kabisa. Hana lolote alijualo.
 
Nyumbu ni nyumbu tu, unajazwa upepo na maujinga ujinga tu. Akiba ya chakula si lazima iwe chini ya serikali yote, hata hiyo iliyo chini ya watu binafsi na makampuni pia ni akiba ya watz na itauzwa Tz.

Lengo la serikali kununua chakula ilikuwa ni price control kwa kiasi kikubwa, sera ya saivi ni kuachia wakulima wa nafaka uhuru zaidi kwenye bei, muwe mnatumia na akili zenu kabla hamjalishwa ma ujinga ujinga na nyumbu wenzenu.
Mtakula hayo mandege yenu.
 
ZZK ni mpiga dili tu na wakala wa mabeberu, hii nchi ni tajiri na awamu ya tano imewezesha uchumi kukua kwa zaidi ya 7%, pato la Mtanzania limekuwa pia, mabarabara kila kona, Madege angani, SGR, Stieggler's.

Huyu ZZK ndio wale wanaomkatisha tamaa Rais wetu JPM kipenzi cha wanyonge wa nchi hii, nchi imeliwa sana hii JPM anainyoosha balaa..




Utaendelea kuwa MNYONGE MPAKA UNYONGEKE.
 
Back
Top Bottom