Kwa mujibu wa Waziri wa fedha, wastani wa pato la mtanzania kwa siku ni Tsh. elfu sita, je hii inatosha mahitaji? Bei ya nyama,mkaa,pango,sukari....?

Hiyo ripoti ya IMF wewe hujaielewa uko gizani kabisa.Yaani uko mweupe kichwani.Kila MTU hapo Pato lake mi 6500 .Kwa hiyo Kwa hapo Pato la familia Kwa siku no 6500 mara idadi yenu ambayo ni 8 Kwa hiyo jumla ya Pato lenu Kwa siku ni shilingi 52,000 sio 6000
Mkuu kwa wewe unaeishi kwenye mwanga akili yako inakutuma kuwa kwa ripoti ya imf na kula kwa mama ntilie vina mahusiano? Mkuu ama kweli nyani haoni kundule.
 
Hii kukuwa kwa kipato ndani ya miaka 3,sijui watumishi wameongezewa mshahara! Au wao si wananchi?
Hali ya maisha japo raia wanajibana lakini hali bado ngumu. Hii haingii akililini?
 
Mkuu kwa wewe unaeishi kwenye mwanga akili yako inakutuma kuwa kwa ripoti ya imf na kula kwa mama ntilie vina mahusiano? Mkuu ama kweli nyani haoni kundule.
Mkuu kwa wao wanaolishwa na kupata shibe zisizo rasmi "kuchafua hewa" si kitu cha ajabu
 
Wastani wa wa pato ni tsh 6500,japo haijafafanuliwa sana kwa sababu haiwezekani IMF waseme uchumi umeshuka kutoka asilimia 7 mpaka 4,halafu hao ambao wanaishi kwenye uchumi huo pato lao liongezeke!
Tukiacha IMF,hata mtaani kilio ni kikubwa sana kuhusu uchumi,halafu leo anakuja mtu anasema hao wanaolia kuhusu uchumi kuwa mbaya eti mapato yao yameongezeka!
Turudi kwenye hoja,je huo wastani wa tsh 6500/ unamfanya mtanzania aishi kama binadamu au anategemea miujiza?
Kilo ya nyama tsh 5000, unga,mkaa,nyanya,ada ya shule, nauli za wanafunzi,pango la nyumba,mavazi, kulipia maji,umeme,chumvi...... .
Pia,je kipato hicho kitawafanya watoto waondokane na utapia mlo ili tupate wasomi wazuri watakaoingia katika dunia ya sayansi wakiwa timamu?
Hii pesa inatosha sana ukiongeza na ile buku saba ya Lumumba inakuwa 13,000/= .
 
Hiyo pesa inatosha . Tatizo watanzania tunapenda kujipikia nyumbani .Kale kwa mama nitilie Chai na chapatii 1000 chakula cha mchana 2000 cha jioni 2000 unabakiwa na 1500 .Maisha yanaendelea
Watoto na Mama yao je?....au wewe ukitafuna wao kule home wanameza.
 
Hiyo Hesabu ya IMF inaonyesha Pato kwa mtu mmoja akiwemo huyo mwanao na hao tegemezi Kila Moja kapigiwa humo humo kuwa ana Pato la 6500.Kwa hiyo kwa Hesabu hizo za IMF kama una mtoto ina maana wewe 6500 na mtoto 6500 jumla Pato lenu kwa siku 12500.Hao wa kijijini wamo nao wanahesabika kuwa Kila mmoja ana Pato kwa siku la 6500.Kwa hiyo mkiwa kumi bila kujali kuna mkubwa au mtoto mchanga kwa Hesabu za IMF mnatambulika kuwa kwa siku Pato lenu ni Elfu Sitini na tano.Si haba kwa Pato hilo kwa watu kumi kwa siku mwaweza Kula na kusaza na zingine mkaenda kulewa.Ndio maana nikasema zinatosha.
Kwa hizo hesabu mnakula pilau daily, yenye asilimia 80 nyama, na ishirini ndio mchele na viungo vingine, kisha mnaenda kulala kusubiri buku 65 za siku inayofuata.

Alafu utashangaa wale Wa ethiopia hapa wanapita kukimbilia South Africa, sijui ni kukosa taarifa.

Na utashangaa ikija orodha ya wakosa raha duniani mpo, sasa wale wanaoshindia ugali na ngogwe wasemaje.
 
Sasa mmekadiriwa 6500 mnalalamika, makadirio yanayokuja tutapunguza iwe 4000 ndio muipate fresh.
 
Watu nchi imewashinda imebaki ngonjera na mazingaombwe ,Alikuwa anafikiri kuongoza nchi ni sawa na kukariri kilometa za Barabara na idadi ya samaki ..
 
Back
Top Bottom