Kwa mujibu wa Standing Orders, DAS ni mtumishi wa Umma

Wana UKAWA mnatia sana aibu, nyie ndo mlıtaka mkabidhıwe nchi kweli?Kwanı Mkurugenzi na Wakurugenzi wa idara na vitengo ndani ya Wizara, nafası zao hutangazwa na ufanyiwa usailı?Je hawa si watumishi wa umma?Je makatibu wakuu wa wizara,RAS,DAS lini ukasıkia nafasi zao zikitangazwa?Usikali kijana, hao wote nafasi zao ni za teuzi na ni watumishi wa umma.Sio kweli kwamba kuwa mtumishi lazma afanyiwe usaili.
hapo hakuna cha ukawa wala uccm bali ni maslahi mapana ya taifa letu. rais kateleza.
sio kila uteuzi anapaswa kuweka yeyote. tafuta standing Order ujielimishe.
 
Wana UKAWA mnatia sana aibu, nyie ndo mlıtaka mkabidhıwe nchi kweli?Kwanı Mkurugenzi na Wakurugenzi wa idara na vitengo ndani ya Wizara, nafası zao hutangazwa na ufanyiwa usailı?Je hawa si watumishi wa umma?Je makatibu wakuu wa wizara,RAS,DAS lini ukasıkia nafasi zao zikitangazwa?Usikali kijana, hao wote nafasi zao ni za teuzi na ni watumishi wa umma.Sio kweli kwamba kuwa mtumishi lazma afanyiwe usaili.
Mkuu wewe huelewi kitu, na bahati mbaya hutaki kupata uelewa kwa wajumbe humu, sasa JF inakusaidia nini?msome mwenzio hapa
Mleta mada tuwekee sawa. Nijuavyo mimi ni kwamba Afisa Tawala wa Wilaya ni Dstrict Administrative Officer. Si nafasi ya uteuzi bali ni ya uajiriwa kulingana na mahitaji ya wilaya. Nafasi hizo hutangazwa na Mkoa kwa kufuata taratibu za ajira Serikalini. Si nafasi ya kisiasa hata kidogo na kama Mtela Mwampamba kapatikana kwa style hiyo basi hilo litakuwa doa kubwa kwa serikali yangu ya CCM.
 
Naomba kunukuu Para A1 (21) ya Standing Orders ya 2009 kama kanuni za kudumu za Utumishi wa Umma........inasema "District Administrative Secretary" means a public servant in-charge of administration in a district; Ikimaanisha kuwa ni mtumishi wa umma atakayewajibika na shughuli za kiutawala ofisi ya Mkuu wa Wilaya.....Kwa kifupi kabisa huyu ni mtumishi wa umma ambaye upatikanaji wa upo wazi kabisa.

Mtumishi wa umma hateuliwi, mtumishi wa umma anapatikana katika namna ya ushindani ambapo mamlaka ya serikali iwe ni utumishi au mamlaka nyingine, hutangaza nafasi na zifa za mwombaji huanishwa. Usaili hufanyika na uchambuzi wa majina hufanyika hatimaye washindi huitwa kazini na kuwa watumishi wa umma ajira ya kudumu ''Permanent and Pensionable''.........

Sasa kati ya watumishi hao wa umma bila kujali ni kada gani huteuliwa kuwa ma-DAS ambao ni makatibu tawala wa wilaya ambao kimsingi majukumu yake ni kufanya shughuli za kiutawala katika ofisi ya mkuu wa wilaya.DAS huwa chini ya ofisi ya RAS-Katibu Tawala wa Mkoa.
Hivyo basi uteuzi wa DAS ni kama ulivyo uteuzi wa DED/MD/TEC Mkurugenzi wa Halmashauri, ni lazima awe mtumishi wa umma kwanza. Hii sio nafasi ya kisiasa.
Nimeonelea nitoe ufafanuzi huu baaada ya kuona jambo la ajabu sana kutokea jioni ya leo. Hatimae siasa zinanajisi utumishi wa umma. Tunaona Mwanasiasa Mtela Mwambamba na wenzake ghafla wameteuliwa kuwa ma-DAS. Sina hakika sana na wengine lakini ni dhahiri shahiri Mtela Mwampamba sio mtumishi wa umma.
Tunajua haja yenu ya kulipa fadhila makada, tunajua mnawarundika pale Ubungo ili kuikomoa UKAWA na Saidi Kubenea lakini kwa namna mnayofanya ni wazi mnaleta aibu kubwa sana. Tafadhalini fuateni utaratibu.

Naitaka mamlaka iliyomteua Mtela na wengine ambao hawakuwa watumishi wa umma itengue mara moja au itoe ufafanuzi ni kwa mazingira gani uteuzi umezingatia taratibu za kupatikana kwa watumishi wa umma

Nachosisitiza hapa ni kwamba KATIBU TAWALA WA WILAYA HUTEULIWA LAKINI NI LAZIMA AWE MIONGONI MWA WATUMISHI WA UMMA
Tafadhali sana Mods msiunge uzi huu. Kuna hoja nzito sana hapa,nawaombeni sana wakuu
Nilikuwa sijaiona hii nikaruka na Uzi mwingine kuhusu hili. Utumishi wa serikali kwa kweli sasa una najisiwa
 
najua nakufundisha vitu hapa ukawaeleze na wenzio. Katibu Tawala wa Wilaya anateuliwa lakini miongoni mwa watumishi wa umma
DAS lazima awe mtumishi Wa Umma mzoefu siyo fresh Mtumishi. Jamani hizi ajira za wilaya mbona kama zinafanana majukumu? DC, DAS, Mbunge, District development Director,
 
Mkuu wewe huelewi kitu, na bahati mbaya hutaki kupata uelewa kwa wajumbe humu, sasa JF inakusaidia nini?msome mwenzio hapa

Kwa Mara ya kwanza nadhani..
.lizaboni kaweka uchama kando na kuweka utaifa mbele baada ya kubanwa mbavu lakini...mwanzo mzuri tutafika tu..
 
Hii Ni Honi Bado Gari Lenyewe
Mtaona Maajabu Awamu Hii Hadi Mshangae
CCM Hii Imekosa Pumzi Jamani
Mengine Tunaionea
Wizi Mbaya Sana Kwasasa Hawana Uelekeo
Wanatamani Warudishe Ushindi Walioiba
 
Ndio tayari ni maDAS , hivi wakati mnamchagua Lowasa kuwa mgombea alitimiza vigezo vya kuwa Mgombea vilivyopo kwenye katiba yenu?, au kulikuwa na vimamruki vyenu nini mliviweka stand by?, acheni watu wafanye kazi
 
Ndio tayari ni maDAS , hivi wakati mnamchagua Lowasa kuwa mgombea alitimiza vigezo vya kuwa Mgombea vilivyopo kwenye katiba yenu?, au kulikuwa na vimamruki vyenu nini mliviweka stand by?, acheni watu wafanye kazi
mkuu sio kila kitu ni siasa. tunazungumzia taratibu za uteuzi. wengine tunalipenda zaidi taifa kuliko hivo vikundi vyenu viitwavyo vyama.
 
Kama "uteuzi'' huu ni wa kweli basi watumishi watakaokuwa chini ya hao wateuliwa wa jiandae kupelekwa puta ki - chama chama na siyo kwa misingi ya utumishi wa umma. Subiri utasikia kama si kuona kabisa.
Uzuri ofisi ya Mkuu wa Wilaya watumishi Wake hawazidi 10
 
1467784181362.jpg
1467784195434.jpg


Huyu Siyantemi naye vp jamani
 
Nchi ya ajabu sana hii

Wabaompigia makofi magufuli inabidi wajiulize sasa

Kwanza kuwapekeka wanasiasa uchwara ubungo bw polepole na mtela inaonyesha dhahiri kuwa magufuli ni mchanga sana kisiasa
Hana kabisa kifua cha siasa
 
Sijui kama JPM hata anaelewa nini anafanya! Ana washauri kweli huyu??

Stop being too negative. Wewe unawafahamu sana wateuliwa kuliko mamlaka zao za uteuzi? Wakati mwingine tuache kufikiri kwa mazoea, tubadilike!

Kuzungumzia sheria na taratibu za kuendesha nchi ni kufikiri kwa mazoea, nchi yetu Chaitanya kuendelea kamwe, kwa kufanya mambo kinyume cha sheria na taratibu zilizopo
 
DAS ni mtumishi Wa umma na huwa ni nafasi ya uteuzi inayopatikana kwa njia ya promotion kwa maafisa tawala wasaidizi mkoani, au maafisa tawala Wa wilaya au maafisa tarafa hawa wote wanaweza kuwa promoted kupewa UDAS, na Mara nyingi elimu yao huwa haitakiwa kupungua shahada ya pili. Ila kwa mtu freshi from mtaani kuteuliwa kuwa DAS mshangao kidogo na pia itawadimorolize watumishi wengine Wa ofisi za wakuu Wa mikoa, na wilaya. Kuna nafasi zingine Kama hii zinahitaji experience ya kutosha Sana. siasa zikiingilia utawala tumekwisha.
 
Back
Top Bottom