Kwa mujibu wa Sheria, oversee Committees (PAC, POAC na LAAC) lazima Wenyeviti wake watoke Upinzani. NEC na CCM wanahaha kuwatafuta

Course Coordinator

JF-Expert Member
Jul 27, 2019
1,681
3,063
Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika ametoa taarifa kwa vyombo vya habari kuwa chama hicho hakijapeleka orodha yoyote ya majina NEC kwa ajili ya uteuzi wa viti maalumu. Lakini NEC inahitaji majina orodha hiyo haraka iwezekanavyo ili iwatangaze, wahudhurie kikao cha kwanza cha bunge jumanne pamoja na kuapishwa.

Kwa kuwa Chadema imekataa kupeleka orodha hiyo, Mnyika amesema NEC inadaiwa kughushi. Yani NEC imeamua kutengeneza orodha "feki" ya wabunge wa viti maalumu wa Chadema, halafu leo usiku kabla ya saa sita itawatangaza ili jumanne wakaape.

SWALI: Kwanini NEC wameamua kufanya uharamia huu?

JIBU: Kila mwaka serikali hupewa $900M (zaidi ya shilingi Trilioni 2) kwa masharti kuwa "oversee committees" za bunge ziongozwe na kambi ya upinzani na kutoa theluthi moja au zaidi ya wajumbe. Kamati hizo ni ya hesabu za Serikali (PAC), kamati ya hesabu za mashirika ya umma (POAC) na kamati ya hesabu za serikali za mitaa (LAAC).

Lakini kuna dalili ya kupoteza fedha hizo kwa sababu hakuna wabunge wa upinzani wa kutosha kuongoza PAC, LAAC wala POAC. Kwahiyo ili tusipoteze fedha hizo inabidi wabunge wa upinzani wapatikane kwa "gharama yoyote"

Na huu ndio msingi wa hoja ya Mnyika kwamba NEC imeamua kughushi majina ya wabunge wa viti maalumu wa Chadema na itawatangaza ili jumanne wakaape. Kwa lugha rahisi ni kwamba serikali ya CCM ilifanya uharamia kwenye uchaguzi bila kujua uharamia huo utakuja kuwagharimu baadae (that's karma).

Sasa wanahaha kuokoa "matrilioni" hayo ya mabeberu. Wanataka kufanya uharamia mwingine wa kutangaza wabunge "feki" wa viti maalumu wa Chadema ili angalau wasipoteze pesa hizo.

Lakini kama uchaguzi ungekua huru na haki, wakapatikana wabunge wengi wa upinzani kuongoza kamati hizo, yote haya yasingetokea. CCM na NEC wasingekua wanahaha muda huu kulazimisha Chadema ipeleke majina ya viti maalumu wala wasingetuhumiwa kutengeneza orodha feki ya wabunge.

Hata hivyo Chadema imeshaweka wazi kuwa haitawatambua wabunge hao hata kama NEC itawatangaza.

Tutaelewana tu huko mbeleni.
Mambo ni fire ...Magufuli na CCM wameishiwa mbinu kisiasa.
 
Wenyeviti ni rahisi sana kuwapata, rais atateua wabunge 6 kutoka vyama vya upinzani vilivyoshiriki uchaguzi.Mbunge wa cuf na Chadema wapo pia.Case closed,leteni drama nyingine.
Chadema wanajiona ni wajanja sana kumbe ni maboya
Chadema ina mbunge 1 Nkasi, CUF Wana wabunge 2 Zanzibar , Rais akiteua 2 tu kutoka wapinzani wazarendo game over
 
Wamewakeshesha vijana kuomba ajira za walimu usiku kucha, mwezi wa pili sasa wamekaa kimya,

Ajabu walivyozinduka wamekuja na viti maalum 94. So sad

Nina mdogo wangu kaomba uwalimu, anatia sana huruma.
Aisee hali itakuwa ngumu ,kama una uwezo mpe dogo mtaji. Hizo ajira zilikuwa za danganya toto japo zaja mbeleni lkn itategemea na waziri atakaye teuliwa
 
Aisee hali itakuwa ngumu ,kama una uwezo mpe dogo mtaji.
Hizo ajira zilikuwa za danganya toto japo zaja mbeleni lkn itategemea na waziri atakaye teuliwa
Waziri anaweza kufanya nini kuhusu ajira?

Anayewanyima vijana ajira huko serikalini unamjua vzr lkn zigo umeamua kumuangushia waziri.
 
Nia ya CCM sio kupata wenyeviti hao au 1/3 ya wajumbe wa kamati hizo-maana hao wanaweza kuteuliwa kwenye vyama vingine.

Nia kuu ni kuionesha ulimwengu kuwa uchaguzi ulikuwa wa guru na haki maana Chadema ndio kilikuwa chama pinzani bungeni hivyo malalamiko yao yatakuwa hayana maana kama wakikubaki viti maalumu.
 
Back
Top Bottom