Kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, Bunge linaweza kumwondoa madarakani Rais

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
“46A.-(1) Bila ya kujali masharti ya ibara ya 46 ya Katiba hii, Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa rais madarakani endapo itatolewa hoja ya kumshitaki rais na ikapitishwa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii.
(2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, hoja yoyote ya kumshtaki rais haitatolewa isipokuwa tu kama inadaiwa kwamba rais-
(a) ametenda vitendo ambavyo kwa jumla vinaivunja Katiba au Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;
(b) ametenda vitendo ambavyo vinakiuka maadili yanayohusu uandikishwaji wa vyama vya siasa yaliyotajwa katika ibara ya 20(2) ya Katiba au
(c) amekuwa na mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano”.
------------------------------------------
Hicho kifungu C kinaweza kutumika kumuondoa Raisi madarakani.

1) Akiwa nchini Ufaransa kwamba hajui umaskini wa Watanzania unatokana na nini.
Akiwa na waandishi wa nje aliamua kuwa wazi na kuwaambia kwamba hata yeye hajui umaskini wa nchi yetu unasababishwa na nini.

Tafsiri yake ni kwamba wakati anagombea urais ‘aliwadanganya’ Watanzania alipowaambia ataleta neema na maisha bora kwa kila Mtanzania.

2 ) Aliporejea nchini na kutimiza miaka miwili Ikulu, aliwaambia waandishi wa nchini kwamba ahadi zote atazitimiza (ikiwamo ya maisha bora kwa kila Mtanzania, ambayo hajui sababu ya kwa nini Watanzania hawana hayo maisha bora na hivyo kuwa maskini). Huku ndiko ‘kudhalilisha’ kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kunakokataliwa na katiba.

3 ) Rais akilihutubia Bunge Desemba 30 mwaka 2005 alisema: “Serikali ya Awamu ya Nne itaendeleza vita dhidi ya umaskini, ujinga na maradhi, tena kwa ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya”. - Ataendeleza vipi vita wakati haelewi adui umasikini anakujakujaje.

Nimeshangaa kuona kwamba hata pesa ya Rwanda na Burundi, nchi zilizokuwa na vita miaka mingi, ina thamani kuliko shilingi ya Tanzania. Amani tunayodai kuilinda kwa kila hali ni ya nini? Inatusaidia nini?

Kama nchi zinazopigana vita ya wenywe kwa wenyewe baada ya vita watawala wanakuwa na adabu na kuwatumikia wananchi sawa sawa, basi na sisi tupigane.

Baadhi yetu tufe kama kafara ili tuokoe maisha ya vizazi vijavyo, vinginevyo kwa ari hii, nguvu hii na kasi hii, Tanzania ijayo itakuwa maskini sawa na jalala na Watanzania wa kizazi kijacho watakuwa maskini sawa na vichaa na chokoraa wanaokula majalalani.

3 ) Mimi sitembei na fuko la pesa -Kiti Cha Urais kimedhalilishwa

4 ) Anasema serikali hii yenye kitivo cha sheria cha kwanza kwa nchi za Afrika Mashariki, haina wataalamu wa kujua hilo! Hii ni aibu na kwa kweli kwa mkuu wa nchi kuwatangazia mataifa ya nje kwamba nchi yake haina wanasheria wa kujua mambo madogo kama hayo ni kukidhalilisha kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano.

Na wanasheria wa nchi hii sijui kwa nini hawajajitokeza kupinga kauli hii ya rais iliyowadhalilisha sana!

Kama nchi zinazopigana vita ya wenywe kwa wenyewe baada ya vita watawala wanakuwa na adabu na kuwatumikia wananchi sawa sawa, basi na sisi tupigane.

Source : Kalamu ya MWIGAMBA
 
Kuna taarifa kuwa siku chache zijazo ataanza safari ya kwenda Marekani.Zile trip za Iringa na Muheza zilikuwa ni cover tu kwa ajili ya safari ndefu ya Marekani.

Na tatizo lake ni kuwa ziara hizi nyingi ni za kimatanuzi! na gharama zote hulipwa na fedha za walipa kodi!

Na haelekei kuelewa kuwa kuna watu wanaishi kwa mlo mmoja na kukosa huduma muhimu za kijamii kama afya,maji,chakula n.k.

Nafikiri kuna umuhimu wa kuanza kuprotest kila mahala atakapokuwa anatembelea ili japo kumpa signal kuwa makubwa yanaweza kutokea kama serikali yake itaendelea kupuuzia matatizo ya wananchi.

Wembe.
 
Kumwondoa Rais wakati Bunge lina zaidi ya Asilimia 80 ya Wabunge wa Chama Chake, na katika Bunge ambalo kila jambo linaloletwa na Serikali linaweza kuchanwa chanwa na hatimaye kuptishwa kwa asilimia 100 mmh! mmh! may be years to come?

Jambo jema kuwa na hasira ya namna hiyo tunapuguswa hata hivyo.....
 
Kwanini nyie watanzania mnaoishi huko nchi za ughaibuni msitusaidie haya mambo
Kwa kuwa nyie mmeonyesha sana kuchoshwa na porojo za huyu Commedian, na kila akija mnataka kukutana naye eti kuzungumza naye, kwa nini pakiandaliwa vikao kama hivyo mvisusie kabisa na akienda pale ajikute yuko na balozi wake tu

Labda ingeonyesha kuwa watanzania hawataki safari hizo zinazotugharimu mapesa kibao wakati watu wanakufa kila kukicha kwa kukosa huduma muhimu

Kwani huku anakuja kukutana na watanzania ama wafadhili?
Maana hata huu ubalozi huku si ni kwa ajili ya wawekezaji?
 
..lets be real, this is wishful thinking!

One day your wish will be granted. Especially if we decide that we have had enough, and take actions. They might be temporarily painful but the result will be lasting. Hakuna atakae dhubutu kuchezea fedha na Haki za umma kiasi hiki tena.
 
Kumwondoa Rais wakati Bunge lina zaidi ya Asilimia 80 ya Wabunge wa Chama Chake, na katika Bunge ambalo kila jambo linaloletwa na Serikali linaweza kuchanwa chanwa na hatimaye kuptishwa kwa asilimia 100 mmh! mmh! may be years to come? Jambo jema kuwa na hasira ya namna hiyo tunapuguswa hata hivyo.....
Hilo sio tatizo kwani ikiwa mtaweza kufikia hatua ya kudai jambo hilo ,basi Watanzania nao watasikia na kuona ,kupima na kufikiri,watazidi kuelewa umuhimu wa kura yao.

Na kiasi itakuwa somo na kuona ,kumbe jambo hili linaweza kufanyika.Vile vile yanayotetewa ni maslahi ya wananchi au taifa kwa ujumla hivyo ,hata humo ndani ya CCM kuna mwamko fulani ambao umejitokeza siku hizi,japo hatujaona ukweli wa makeke yao ,au kuungana katika hoja zinazolitetea taifa (Pengine wamewahi ila sina kumbukumbu) na wabunge watokeao vyama vingine.

Tuseme CCM hawawezi kujitokeza kudai kuwa Raisi aliyepo madarakani amekidharaulisha kiti cha Uraisi wa Tanzania , lakini Je hawa ambao ni vyama pinzani ambavyo vinatakiwa viwe vinapigilia msumari kila pale ambapo sheria inawaruhusu ,hivyo huoni kama hili amelitenda ni wakati muafaka kwa vyama au upinzani kusimama kwenye Katiba na kutumia kifungu hicho. Hapa ni Tanzania hali ya wabunge kutoka Chama cha CCM inajulikana tofauti na nchi za Ulaya ambapo wabunge wanawathamini zaidi wananchi waliowapigia kura kuliko Raisi hata kama wanatoka Chama kimoja.

Mbunge ni raisi katika jimbo analotoka ,maana hata mtu akiumwa,akishitakiwa basi mbunge anapashwa habari kuwa fulani ameshitakiwa na tunaona hatatendewa haki,ikiwa mwananchi huyo yupo au amepata matatizo hayo,mbunge wao itambidi aijulishe serikali na serikali ni lazima ifuatilie kwa kutumia Mabalozi wao wa nchi za nje husika,na kama hakufuatilia na serikali nayo haikufuatilia basi inakuwa balaa kubwa sana na huonekana ni jambo la aibu kwa serikali nzima na wananchi wote hukaribia kuungana au huungana ndio ,ukaona raia wa nchi za nje wanaringa na hawana wasiwasi wanapofika nchi za kwetu si kwa sababu Marekani ni nchi yenye nguvu au nchi nyengine yeyote kwa kuwa tu ni ya kizungu lakini ule msimamo wa mshikamano baina ya wabunge na raia zake ndio unaowafanya waheshimike.

Hivyo upinzani usingojee kupata idadi kubwa ya wabunge kwani msimamo wanaochukua ndio utakaowageuza wananchi kuchagua chama kingine badala ya CCM,kama ulivyosema labda Years to come ! ni sawa lakini miaka hiyo huanza na hatua moja ,vitendo vya ujasiri ndivyo vitakavyowaongezea wabunge na sio malumbano ya ukali na makeke ndani ya bunge,vitendo ambavyo wananchi wataviona vina ukweli ,kama hili ambalo kwa nchi za Ulaya tayari Raisi asingekuwepo ,huko wanategemea wananchi hivyo wabunge wote wasingeweza kukwepa kwa sababu tu Raisi anatoka Chama Chao na naamini na hapa ulingano huu wa kusimamia vifungu vya Katiba mkivianza na wananchi kuvielewa na nyie mkivitumia hivyo hivyo mlivyo basi itakuwa rahisi kwa years to come utekelezwaji kuwa ni jambo la kawaida na heshima ya kiti hicho itabakia milele na milele.
 
Kumwondoa Rais wakati Bunge lina zaidi ya Asilimia 80 ya Wabunge wa Chama Chake, na katika Bunge ambalo kila jambo linaloletwa na Serikali linaweza kuchanwa chanwa na hatimaye kuptishwa kwa asilimia 100 mmh! mmh! may be years to come? Jambo jema kuwa na hasira ya namna hiyo tunapuguswa hata hivyo.....

Mkuu,

unajua kwa jinsi katiba yetu ilivyo na hasa ukiangalia wording ya hiyo ibara ya 46A na mamlaka mengine aliyonayo Rais,wabunge hata kabla hawajafikia hitimisho la kumuondoa Rais madarakani ayari Rais anaweza kuwa ameshalivunja bunge kwa mamlaka aliyonayo na likelihood ya Rais kurudi madarakani ni kubwa kuliko wabunge aliowaondoa kwa kutokuwa na imani naye.

Kama unavyosema Dr.Kutumika kwa ibara hiyo kunawezekana tu iwapo kuna majority oppositions na pia mamlaka mengine ya Rais kikatiba yakawa yamerekebishwa.

Utaratibu wa kumuondoa umewekwa kuwa mgumu hivyo ili ishindikana kumtoa madarakani kiurahisi, kwani wakati ibara hiyo inawapa nguvu wabunge kumuondoa madarakani, kuna ibara inamruhusu Rais kulivunja bunge, kulihutubia akitaka, kutangaza hali ya hatari na vilevile kuna ibara inayosema atashika madaraka hadi kipindi chake kiishe,hivyo si mahakama wala mtu yeyote mwenye mamlaka ya kumuondoa madarakani.

Hebu rudini nyuma kumbukeni kesi ya MWL. PAUL JOHN MUHOZYA V.AG ambapo alijaribu kumshitaki mwinyi kwa kuvunja katiba baada ya ZANZIBAR kujiunga OIC na hivyo kutaka mahakama itamke kuwa amevunja katiba na hivyo anapaswa kuondoka madarakani
 
Uwezo wa kumwondoa upo au haupo ? Sababu zipo au Hazipo ? Nia ipo au haipo ?

Naamini kabisa ikiwa Wabunge watasimama kidete kuanzisha libeneke hili basi tutauona Uungwana wa Muungwana .

Ikiwa amejitapa kuwa yeye ana uwezo mkubwa hivi nani asietambua kuwa raisi wa Tanzania ana mamlaka zaidi ya kiasi anachotakiwa awe nacho.

Naona pengine mafisadi wana siri za ndani za Kikwete na hizo ndizo pengine wanazoringia nazo ,siri ambazo kama zipo ,na mafisadi watuhumiwa wakiamua kuzianika basi Kikwete itambidi ajiuzulu kikamilifu kuliko Lowasa maana pengine hata kwenye Chama atakuwa hafai ,kuna nini baina ya Kikwete na mafisadi ?

Hata Muungwana ikawa mgumu kuwachukulia hatua za nguvu anazotamba nazo kwenye Bunge letu ,maana kuwachekesha watu kwa kumtumbulia macho mtu na kumwambi ninaweza kuamrisha ukamatwe ,huku ni kujitangazia madaraka ya kiubabe, kuna msemo usemao na nataka nanyi muujue kwani ni wa maana sana na una elimu iliyojificha ,msemo wenyewe unasema kila kwenye masihara basi kuna ukweli fulani.

Hivyo Rais amesema kimasihara lakini kiundani kuna kajiukweli fulani.

Wabunge ni lazima sasa wawe na meno au waonyeshe meno yao ili kukilinda kiti cha Uraisi kisiwe kinafanyiwa biashala na kutishana ,wabunge wanadhamana kwa wananchi hawakuchaguliwa kwenda bungeni kuonyesha meno.
 
Kweli mumechanganyikiwa, Lakini mengine ni hivyo kwa kuwa taifa linapita kwenye transition, kutoka demokrasia iliyobanwa kwenda kwenye true democratic state.

Taifa lina Mh. Rais ambaye anataka kuwezesha mifumo ifanye kazi as opposed na Rais wa kukurupuka, kuropoka na kukunya sura kama akidhani huo ndio urais.. huo ni Urais wa Miaka ya Arobaini.

Wakati ameongelea Rushwa utagundua ndicho anachotaka kuwe na mifumo... sio mtu mmoja ndiye ategemewe kwa kila kitu....

Mfano kwenye rushwa amesema yafuatayo:-
-Kurekebisha tume ya maadili, sheria kanuni
-Kuboresha sheria ya TAKUKURU
-Kutunga sheria ya mchakato wa Uchaguzi - ndani na nje ya vyama.
Baada ya hapo vyombo husika vitafanyia kazi...

Kuna mambo mengi hamjaelewa mtaelewa baadaye ni ngumu kuelewa especially kwa kuwa mnatoka kwenye tawala zilizokuwa semi-dictactorship.

Siku zote mabadiliko hayapokewi vizuri... hata Mkapa alichukiwa sana miaka yake ya Mwanzo wa Utawala wake... lakini eventually alivyoondoka alitoka kidedea.... mumesahau... the so called 'UKAPA"

Marais madikteta wa kutoa siku saba Mungu atuepushe nao!
 
46A.-(1) Bila ya kujali masharti ya ibara ya 46 ya Katiba hii,
Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakani
endapo itatolewa hoja ya kumshtaki Rais na ikapitishwa kwa
mujibu wa masharti ya ibara hii.

(2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, hoja
yoyote ya kumshtaki Rais haitatolewa isipokuwa tu kama
inadaiwa kwamba Rais-

Sheria ya …. (a) ametenda vitendo ambavyo kwa jumla vinaivunja
Katiba au Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;

(b) ametenda vitendo ambavyo vinakiuka maadili
yanayohusu uandikishwaji wa vyama vya siasa
yaliyotajwa katika ibara ya 20(2) ya Katiba, au

(c) amekuwa na mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais
wa Jamhuri ya Muungano, na haitatolewa hoja ya
namna hiyo ndani ya miezi kumi na miwili tangu hoja
kama hiyo ilipotolewa na ikakataliwa na Bunge.

(3) Bunge halitapitisha hoja ya kumshtaki Rais isipokuwa tu
kama-

(a) taarifa ya maandishi, iliyotiwa sahihi na kuungwa
mkono na Wabunge wasiopungua asilimia ishirini ya
Wabunge wote itawasilishwa kwa Spika siku
thelathini kabla ya kikao ambapo hoja hiyo
inakusudiwa kutolewa Bungeni, ikifafanua makosa
aliyoyatenda Rais, na ikipendekezwa kuwa Kamati
Maalum ya Uchunguzi iundwe ili ichunguze
mashataka yaliyowasilishwa dhidi ya Rais;

(b) wakati wowote baada ya Spika kupokea taarifa
iliyotiwa sahihi na Wabunge na kujiridhisha kuwa
masharti ya Katiba kwa ajili ya kuleta hoja
yametimizwa, Spika atamruhusu mtoa hoja
kuiwasilisha hoja hiyo, na kisha Spika atalitaka
Bunge, bila ya kufanya majadiliano, lipige kura juu ya
hoja ya kuunda Kamati Maalum ya Uchunguzi na
kama ikiungwa mkono na Wabunge waiopungua
theluthi mbili ya Wabunge wote atatangaza majina ya
wajumbe wa Kamati Maalum ya Uchunguzi.

(4) Kamati Maalum ya Uchunguzi, kwa madhumuni ya ibara
hii, itakuwa na wajumbe wafuatao, yaani-

(a) Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, ambaye
atakuwa ndiye Mwenyekiti wa Kamati;

(b) Jaji Mkuu wa Tanzania Zanzibar na

(c) Wajumbe saba walioteuliwa na Spika kwa mujibu wa
Kanuni za Bunge na kwa kuzingatia uwiano wa
uwakilishi baina ya vyama vya siasa
vinavyowakilishwa Bungeni.

(5) Endapo Bunge litapitisha hoja ya kuunda Kamati Maalum
ya Uchunguzi, Rais atahesabiwa kuwa hayupo kazini, kisha kazi
na madaraka ya Rais yatatekelezwa kwa mujibu wa masharti ya
ibara ya 37(3) ya Katiba hii hadi Spika atakapomfahamisha Rais
juu ya azimio la Bunge kuhusiana na mashataka yaliyotolewa
dhidi yake.

(6) Ndani ya siku saba baada ya Kamati Maalum ya Uchuguzi
kuundwa, itakaa ichunguze na kuchambua mashataka dhidi ya
Rais, pamoja na kumpatia Rais fursa ya kujieleza, kwa kufuata
utaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge.

(7) Mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote vile katika muda
usiozidi siku tisini, Kamati Maalum ya Uchunguzi itatoa taarifa
yake kwa Spika.

(8) Baada ya Spika kupokea taarifa ya Kamati Maalum ya
Uchunguzi, taarifa hiyo itawasilishwa Bungeni kwa kufuata
utaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge.

(9) Baada ya taarifa ya Kamati Maalum ya Uchunguzi
kuwasilishwa kwa mujibu wa ibara ndogo ya (8), Bunge litaijadili
taarifa hiyo na litampa Rais fursa ya kujieleza, na kisha, kwa kura
za Wabunge wasiopungua theluthi mbili ya Wabunge wote,
Bunge litapitisha azimio ama kuwa mashtaka dhidi ya Rais
yamethibitika, na kwamba hastahili kuendelea kushika kiti cha
Rais, au kuwa mashtaka hayo hayakuthibitika.

(10) Endapo Bunge litapitisha azimio kuwa mashtaka dhidi ya
Rais yamethibitika na kwamba hastahili kuendelea kushika kiti
cha Rais, Spika atawafahamisha Rais na Mwenyekiti wa Tume
ya Uchaguzi juu ya azimio la Bunge, na hapo Rais atawajibika
kujiuzulu kabla ya kuisha kwa siku ya tatu tangu Bunge
lilipopitisha azimio hilo.

(11) Endapo Rais ataacha kushika kiti cha Rais kutokana na
mashataka dhidi yake kuthibitika, hatakuwa na haki ya kupata
malipo yoyote ya pensheni wala kupata haki au nafuu nyinginezo
alizo nazo kwa mujibu wa Katiba au Sheria yoyote iliyotungwa na
Bunge.
 
46A.-(1) Bila ya kujali masharti ya ibara ya 46 ya Katiba hii,
Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakani
endapo itatolewa hoja ya kumshtaki Rais na ikapitishwa kwa
mujibu wa masharti ya ibara hii.

(2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, hoja
yoyote ya kumshtaki Rais haitatolewa isipokuwa tu kama
inadaiwa kwamba Rais-

Sheria ya …. (a) ametenda vitendo ambavyo kwa jumla vinaivunja
Katiba au Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;

(b) ametenda vitendo ambavyo vinakiuka maadili
yanayohusu uandikishwaji wa vyama vya siasa
yaliyotajwa katika ibara ya 20(2) ya Katiba, au

(c) amekuwa na mwenendo unaodhalilisha kiti cha Raiswa Jamhuri ya Muungano, na haitatolewa hoja ya
namna hiyo ndani ya miezi kumi na miwili tangu hoja
kama hiyo ilipotolewa na ikakataliwa na Bunge.

(3) Bunge halitapitisha hoja ya kumshtaki Rais isipokuwa tu
kama-

(a) taarifa ya maandishi, iliyotiwa sahihi na kuungwa
mkono na Wabunge wasiopungua asilimia ishirini ya
Wabunge wote itawasilishwa kwa Spika siku
thelathini kabla ya kikao ambapo hoja hiyo
inakusudiwa kutolewa Bungeni, ikifafanua makosa
aliyoyatenda Rais, na ikipendekezwa kuwa Kamati
Maalum ya Uchunguzi iundwe ili ichunguze
mashataka yaliyowasilishwa dhidi ya Rais;

(b) wakati wowote baada ya Spika kupokea taarifa
iliyotiwa sahihi na Wabunge na kujiridhisha kuwa
masharti ya Katiba kwa ajili ya kuleta hoja
yametimizwa, Spika atamruhusu mtoa hoja
kuiwasilisha hoja hiyo, na kisha Spika atalitaka
Bunge, bila ya kufanya majadiliano, lipige kura juu ya
hoja ya kuunda Kamati Maalum ya Uchunguzi na
kama ikiungwa mkono na Wabunge waiopungua
theluthi mbili ya Wabunge wote atatangaza majina ya
wajumbe wa Kamati Maalum ya Uchunguzi.

(4) Kamati Maalum ya Uchunguzi, kwa madhumuni ya ibara
hii, itakuwa na wajumbe wafuatao, yaani-

(a) Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, ambaye
atakuwa ndiye Mwenyekiti wa Kamati;

(b) Jaji Mkuu wa Tanzania Zanzibar na

(c) Wajumbe saba walioteuliwa na Spika kwa mujibu wa
Kanuni za Bunge na kwa kuzingatia uwiano wa
uwakilishi baina ya vyama vya siasa
vinavyowakilishwa Bungeni.

(5) Endapo Bunge litapitisha hoja ya kuunda Kamati Maalum
ya Uchunguzi, Rais atahesabiwa kuwa hayupo kazini, kisha kazi
na madaraka ya Rais yatatekelezwa kwa mujibu wa masharti ya
ibara ya 37(3) ya Katiba hii hadi Spika atakapomfahamisha Rais
juu ya azimio la Bunge kuhusiana na mashataka yaliyotolewa
dhidi yake.

(6) Ndani ya siku saba baada ya Kamati Maalum ya Uchuguzi
kuundwa, itakaa ichunguze na kuchambua mashataka dhidi ya
Rais, pamoja na kumpatia Rais fursa ya kujieleza, kwa kufuata
utaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge.

(7) Mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote vile katika muda
usiozidi siku tisini, Kamati Maalum ya Uchunguzi itatoa taarifa
yake kwa Spika.

(8) Baada ya Spika kupokea taarifa ya Kamati Maalum ya
Uchunguzi, taarifa hiyo itawasilishwa Bungeni kwa kufuata
utaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge.

(9) Baada ya taarifa ya Kamati Maalum ya Uchunguzi
kuwasilishwa kwa mujibu wa ibara ndogo ya (8), Bunge litaijadili
taarifa hiyo na litampa Rais fursa ya kujieleza, na kisha, kwa kura
za Wabunge wasiopungua theluthi mbili ya Wabunge wote,
Bunge litapitisha azimio ama kuwa mashtaka dhidi ya Rais
yamethibitika, na kwamba hastahili kuendelea kushika kiti cha
Rais, au kuwa mashtaka hayo hayakuthibitika.

(10) Endapo Bunge litapitisha azimio kuwa mashtaka dhidi ya
Rais yamethibitika na kwamba hastahili kuendelea kushika kiti
cha Rais, Spika atawafahamisha Rais na Mwenyekiti wa Tume
ya Uchaguzi juu ya azimio la Bunge, na hapo Rais atawajibika
kujiuzulu kabla ya kuisha kwa siku ya tatu tangu Bunge
lilipopitisha azimio hilo.

(11) Endapo Rais ataacha kushika kiti cha Rais kutokana na
mashataka dhidi yake kuthibitika, hatakuwa na haki ya kupata
malipo yoyote ya pensheni wala kupata haki au nafuu nyinginezo
alizo nazo kwa mujibu wa Katiba au Sheria yoyote iliyotungwa na
Bunge.

Penye rangi nyekundu, JK bado hana sifa za kudhalilisha kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano?

- Kutoa msamaha kwa wezi wa pesa za EPA kabla ya kufikishwa mahakamani na kuhukumiwa.
 
Ibara ya 46A YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, 1977; INAYOHUSU KUMUONDOA MADARAKANI (IMPEACHMENT) RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA. katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 [Cap. 2 R.E. 2002.]

ZOEZI HILI HUCHUKUA JUMLA {KAMA KILA KITU KINAKWENDA SAWA - ceteris paribus} YA SIKU 150 au miezi mitano. Kwa mfano huu mchakato ukianza leo, mwezi wa tano Raisi anakuwa kaondolewa.

Rais (Mhimili wa Utawala) anaweza kuondolewa madarakani chini ya Ibara hii kwa tuhuma za aina nne:
- kuvunja katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.
- Kukiuka Sheria ya Maadili ya Viongozi [Leadership Code]
- Kukiuka vipengele vilivyomo katika maadili yanayohusu uandikishwaji wa vyama vya Siasa yaliyotajwa katika Ibara ya 20 (2) ya Katiba, au
- Amekuwa na mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

1. Ili kuanzisha mchakato huo inahitaji idadi ya asilimia 20 (20%) ya Wabunge waliopo wafikishe Notisi ya maandishi na kuiwasilisha kwa Spika. Siku 30 zipite kabla ya kikao cha kujadili hizo tuhuma: ( wabunge wa CDM pekee wanatosha kufika 20% (

2. Baada ya kupita hizo siku 30, MTOA HOJA ATAIWASILISHA BUNGENI.

-Aidha tuhuma zitupwe au
- Wapendekeze kuunda Kamati ya Kuchunguza tuhuma hizo.

3. Bunge litapiga kura ili iundwe Kamati ya Kuchunguza tuhuma hizo; lakini kura hizo lazima zifikie au zizidi theluthi mbili ya kura zote. Kama ndio,

4. Spika anatakiwa kutaja majina ya Kamati ya Uchunguzi chini ya Ibara ya 46A(4) ambao ni:
(a) Jaji Mkuu (Mwenyekiti)
(b) Jaji Mkuu wa Zanzibar
(c) Wajumbe saba wanaoteuliwa na Spika; kwa kuzingatia Kanuni za Bunge na Uwakilishi wa Vyama vya Siasa Bungeni.

Matokea ya No. 3 hapo juu chini ya Ibara 46A (5) ni kwamba

- RAis anasimamishwa kazi
- Vivyo Ibara ya 37 (3) inafanya kazi. (Edapo Rais hatakuwepo madarakani wakati huo)

Jambo hili la kumsimamisha kazi Rais litaendelea hadi hapo Spika atakapomfahamisha Rais juu ya matokeo ya uchunguzi uliofanywa [Ibara ya 46A (5)]

Na. 4 hapo juu Kamati inapewa siku 7 kukamilisha uchunguzi wake na kumpa fursa Rais ya kujieleza [Ibara ya 46A (6)]

Kamati ya uchunguzi inapewa siku 90 kukamilisha ripoti yake na kuiwasilisha kwa Spika.

Ibara ya 46A (8) - Spika anawasilisha Ripoti ya Uchunguzi kwa Bunge

Ibara ya 46A (9) - Bunge lenye idadi isiyopungua theluthi mbili litajadili Ripoti hiyo na kumpa Rais fursa ya kujieleza.

Bunge linatakiwa liibuke na aidha ya majibu yafuatayo:

(i) Kwamba tuhuma zimethibitishwa.
(ii) Kwamba Rais hafai kuendelea kufanya kazi
(iii) Kwamba Rais hafai kuwa Rais
(iv) Kwamba tuhuma hazikuthibitishwa.

Ibara 46A(10) - Baada ya hilo kufanyika, endapo ni (i) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatakiwa kuachia ngazi (resign) ndani ya siku tatu.

MCHAKATO HUO WOOOOTE ULIOTAJWA HAPO JUU UKIFUATAWA KAMA UNAVYOTOLEWA kisheria unatakiwa kumalizika ndani ya siku 150 sawa sawa na miezi 5 kamili.
 
bahati mbaya Rais katiba hiyo hiyo imempa mamlaka Rais ya kulivunja Bunge kwajiyo kabla hamjafanya tendo lolote anaweza kuwaondoa nyie kwanza na pili kuwa impeached it means you have been found guilty na siyo to be removed.
Raisi hana mamlaka ya kuvunja Bunge
 
Back
Top Bottom