Hapana, hizo zote kawaida siyo msahafu.Kuna vitu uumepotosha nadhani kwa makusudi. Bunge likishapitisha hiyo hoja, rais hajiuzuru bali anavunja bunge na kuandaa uchaguzi mkuu chini ya usimamizi wa tume ya uchaguzi. Hajiuzuru bali bunge ndilo huvunjwa, yaani hali inakuwa kama inavyokuwa miezi 3 kabla ya uchaguzi mkuu wa kawaida unaotokana na kipindi cha miaka 5 kufikia tamati. Baada ya bunge kuvunjwa kampeni zitafanyika. Wananchi ndiyo watatoa uamuzi kupitia kura zao. Kwa kawaida wabunge wengi hawatashinda kurejea mjengoni na kwa kawaida rais hushinda huo uchaguzi mkuu wa aina hiyo. Rais akishindwa huo uchaguzi mkuu basi atakabidhi madaraka kwa yule aliyeshinda kama inavyofanyika baada ya uchaguzi mkuu wa kawaida, na yeye atapata heshima na haki zote za kuwa rais mstaafu.