Kwa mujibu wa katiba ya CUF, Lipumba hakujiuzulu!

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,950
29,532
Kwa kuwa katibu mkuu hakupeleka barua ya kujiuzulu ya Mwenyekiti kwenye mkutano mkuu basi Lipumba ana haki ya kutengua uamuzi wake.

Source:mdau anayejadili kupitia Channel ten.
 
Sasa kama barua ya kujiuzulu haijapelekwa kwenye mamlaka iliyomteua utasemaje chama hakina mwenyekiti. Ifikie wakati katiba za vyama vya siasa ziheshimiwe
 
Hv hawa wakina mbowe na lipumba jinsi walivyo waroho wa madaraka cku wakipata urais watakubali kuachia madaraka kweli..mungu atuepushe na hawa watu.
Uenyekiti tu hawataki sijui urais ingekuaje.
Lipumba kaanza kuwa Chairman wakati mtoto aliezaliwa leo hii yupo kidato cha sita lakin bado anapigajia kurudi. Mbowe nae kaanza kuwa chairman Jk akiwa Waziri wakati wa chenkapa lakin bado anajiona Taifa la kesho
 
Kwa kuwa katibu mkuu hakupeleka barua ya kujiuzulu ya Mwenyekiti kwenye mkutano mkuu basi Lipumba ana haki ya kutengua uamuzi wake.

Source:mdau anayejadili kupitia Channel ten.
Mbona unaweka hoja ya upande mmoja? ni vema ungeweka na hoja za yule aliyekuwa akipinga juu ya Lipumba kutaka kulejea kwenye nafasi yake, kwani imezungumzwa wazi hauwezi kuweka kiongozi juu ya kiongozi tayari mamlaka za juu zenye haki kikatiba ya CUF ziliisha teua mwenyekiti wa muda(Kaimu mwenyekiti) wa kukalia nafasi hiyo hadi uchaguzi utakapo fanyika. Nakushangaa wewe Kubwa la wajinga(Jingalao) kwa kuja na kihoja kama jinsi huyo aliyekuwa akimtetea Lipumba alivyoumbuka katika mjadala huo
 
Wanaomtakaa lipumba ni wanaCUF, kama mnabisha ruhusu demokrasia mnayosema kila siku humu awanyoshe. Maana amegundua chama kimekaliwa na kakikundi ka kigaidi na kifisadi.
Lumumba kama mnamuona Lipumba anafaa uenyekiti Mchukueni na mumpe chama chenu lakini sio huku kwetu!!

Tumewachoka na maigizo yenu.
 
Kwa jinsi prof anavyo tetewa na Lumumba ingefaa awe mshauri wa mambo ya siasa huko Lumumba, wabunge ambao wanaocheza mpaka wanavuliwa kofia halafu wanajifanya kulalamika wasingekuwepo kabisaaa.
 
Lipumba naye atulie, asizingue watu. Ukishajiudhuru unaachia kabisa sio kurudi kurudi, anarudi kufanya nini?
 
Anarudi kutekeleza kazi aliyopewa na magamba baada ya kukubali kunun ulika! Ametumwa so, msishangae take it easy.
 
Hivi tu uenyekiti, je wakipata Urais, hii Nchi tusithubutu kuwapa upinzani
 
Wanaomtakaa lipumba ni wanaCUF, kama mnabisha ruhusu demokrasia mnayosema kila siku humu awanyoshe. Maana amegundua chama kimekaliwa na kakikundi ka kigaidi na kifisadi.
Lipumba hajakataliwa kuchukuwa fomu ya kugombea uwenyekiti lkn huwezi kumfukuza kaimu mwenyekiti kwasababu yule aliyejiondoa anarudi hiyo sio demokrasia labda ya ccm
 
Back
Top Bottom