Kwa mujibu wa kanuni, Chikwende hatocheza mechi yoyote CAF group stage akiwa na Simba

tyc

JF-Expert Member
Feb 25, 2014
1,179
2,955
Inasikitisha Simba tumesajili mchezaji mwenye kiwango kizuri, uzoefu wa kutosha katika mashindano ya kimataifa ngazi ya klabu lakini hatoweza kuichezea Simba katika hatua ya CAF group stage (16 round)

Hii ni kutokana na kanuni ya CAF kwamba timu yoyote ikifuzu kuingia group stage basi haitotakiwa kusajili mchezaji aliyeshiriki michuano hio kwa msimu husika
 
Una uhakika?! Jaribu kupitia upya maana sheria zilibadilishwa mwaka jana baada ya COVID-19
 
Mbn yeye Chikwende moja ya sababu ya kukubali kuja Simba, ni kuhakikishiwa nafasi ya kucheza Michezo yote ya Makundi?
 
Una uhakika?! Jaribu kupitia upya maana sheria zilibadilishwa mwaka jana baada ya COVID-19
Nafikiri hiyo sheria ni kwa mchezaji ambae hajacheza champions league round za awali

Yani mfano mngemsajili sarpong angecheza
 
Kama hatocheza, haina shida! Tutaongeza tu idadi ya Mapaka Meusi ya kuingia nayo uwanjani!

Halafu ushindi utakua nje nje tu. Al Ahly tunampiga 5-0 pale kwa Mkapa! Unachezea Paka wewe!!
 
Mbn yeye Chikwende moja ya sababu ya kukubali kuja Simba, ni kuhakikishiwa nafasi ya kucheza Michezo yote ya Makundi???

Julio Cesar golikipa wa Kimataifa wa Brazil aliposajiliwa na QPR ya England 2012 alisema lengo kuu la kuja pale ni kuiwezesha timu yake ichukue ubingwa wa EPL,, lakini kiuhalisia kila mmoja alikuwa anaelewa QPR itakuwa wapi mwisho wa msimu na nini hasa kilichomleta pale Julio
 
Mkiambiwa yanga ni utopolo mnakasirika. Simba haikurupuki hata siku 1 CAF ndio wamepitisha timu kuongeza wachezaji kwenye kipindi hiki cha covid. Hivyo chikwende Atacheza kama kawaida.
Kwa Morison Simba ilikurupuka au haijakurupuka? Ukiweza kujibu hapa ni sawa ila ukiamua kujijibu mwenyewe kimya kimya ni sawa pia
 
Ni uhakika mkuu, hio ni kanuni ya mashindano na haijabadilika

Pia mtandao wa goal.com wameelezea hilo

Pitia hapa,

Kanuni za mashindano zimebadilka sana mfano juzi CAF wamesema kama club inawachezaji 11 inaruhusiwa kucheza hata kama hakuna golikipa , mchezaj yeyote anakaa golini , msipochezaji timu pinzani inapewa ushindi wa goli 2-0

Lakini pia club zilitakiwa kuongeza wachezaji 10 kutoka wale wa awali

Hizi zote sio sheria as sheria , zinatumika muda huu pekee wa covid , wala haziingi kwenye vitabu vya sheria ya kudumu
 
Tatizo CAF huwa wanaigiliza kanuni zao na sheria zao toka UEFA, UEFA wao walishabadilisha hiyo kanuni mwaka jana, hao CAF bado wako nyuma kama kawaida yao wanasubiri muda ufike ndio waitishe kikao cha kuwaiga UEFA.
 
Kanuni za mashindano zimebadilka sana mfano juzi CAF wamesema kama club inawachezaji 11 inaruhusiwa kucheza hata kama hakuna golikipa , mchezaj yeyote anakaa golini , msipochezaji timu pinzani inapewa ushindi wa goli 2-0

Lakini pia club zilitakiwa kuongeza wachezaji 10 kutoka wale wa awali

Hizi zote sio sheria as sheria , zinatumika muda huu pekee wa covid , wala haziingi kwenye vitabu vya sheria ya kudumu

Lakini katika kanuni zilizobadilishwa hv karibuni hii tunayojadili haipo katika mabadiliko, yaani haijatangazwa kubadilika

Pitia hapa katika website ya CAF uone regulations

 
Wakati tunacheza na Tp mazembe wanatutoa...mazembe walimnunua Samatta bahati mbaya samatta hakucheza kipindi kile kwani mazembe walitolewa kwakua walikosea kanuni ....inawezekana CAF ni tofauti na UEFA
 
  • Thanks
Reactions: tyc
Lazima tuhangaike kwakuwa msimu huu tuna malengo makubwa matatu:
1. Vpl cup
2. CAF semi final or final
2. Azam federation cup

Vikombe vingine vya bonanza hatuna habari navyo, ni changamsha mwili, sehemu ya warm up tu visije kutuumizia wachezaji wetu
Wenzetu kuchukua lile birika la kuvutia shisha wanajiona kama wamekuwa mabingwa wa dunia vile.
 
Back
Top Bottom