Kwanza kabisa ni declare interest ya kwamba niliwahi kuwa padre wa kanisa katoliki. Niliamua kuachana nao kwasababu nilitaka kuoa. Hiyo ni haki yangu. Kwa sasa kitaaluma ni mwanasheria.
Kwa mujibu wa canon law MSIMAMO RASMI wa baraza la maaskofu(Episcopal Conference) kwa TZ TEC, lazima uwe ni TUNDA la MKUTANO wa baraza hilo. Maana yake, lazima mkutano wa baraza uitishwe, mkutano huo ufanyike, maamuzi ya mkutano huo(resolusion) ndiyo huwa ni msimamo wa kanisa.
Aidha, kwa mujibu wa canon law, mwenye mamlaka ya kuutangaza msimamo huo rasmi ni Mwenyekiti wa Baraza la maaskofu, Makamu wake au Katibu mkuu wa baraza hilo. Ipso facto, hao watu watatu ndio wasemaji rasmi wa baraza la maaskofu popote pale duniani.
Kwa mukitadha huo, Askofu Niwemugizi alisema, anataka Katiba mpya. Ana haki kusema hivyo. Lakini ni maoni yake binafsi. HAKUSEMA ni msimamo wa kanisa katoliki. Hana kosa. Askofu Pengo alisema kwa sasa hataki katiba mpya. Ana haki ya kunena. HAKUSEMA huu ni msimamo wa kanisa katoliki. Hana kosa.
Kwa mantiki hii, hukukuwa na sababu(reasonable cause) ya askofu moja kumlaumi mwenzake hadharani. Figisu hii inatufundisha kuweka akiba ya maneno.