simplemind
JF-Expert Member
- Apr 10, 2009
- 16,418
- 9,205
Dola ya Zanzibar kabla ya kuuundwa Tanganyika
Tunatimiza miaka 53 ya Ukoloni wa Tanganyika kuinyakuwa na kuitawala nchi na dola ya Zanzibar. Miaka 53 ni wastani wa maisha ya binaadamu lakini kiutawala unaonekana muda wa kawaida.
Katika machapisho mawili yaliyopita tuliona muda uliodumu Ukoloni wa Kireno hadi pale ulipotimuliwa katika ardhi ya Zanzibar ambapo ulikuwa umedumu kwa takriban miaka 200. Halkadhalika tuliona baada ya kuja Utawala wa Kisultani ambao nao udumu wake ulikuwa miaka 265.
Kabla ya yote tufahamu na tukubali kuwa Watawala wote lazima wapate support kutoka miongoni mwa viongozi na wananchi. Hata Wareno walipofika kulikuwa na baadhi ya watu waliokuwa wamewakaribisha na kuwaunga mkono iwe kwa matakwa au maslahi yao binafsi. Halkadhila, inajulikana wazi kuingia kwa Sultani ilikuwa ni kwa mualiko uliotokana na mashirikiano ya karibu na viongozi na wananchi wa Zanzibar ili kusaidiwa kuwaondoa Wareno.
Ukoloni wa Tanganyika umeingia Zanzibar kwa njia kama hii aliyoingia Sultan. Inafahamika kuwa Chama cha Afro-Shirazi Party (ASP) kilikuwa na mashirikiano mazuri na chama cha TANU. Baada ya TANU kufanikiwa kupata uhuru wake pamoja na mashirikiano na ASP, ndipo ASP ilipoomba TANU kuja kuivamia Zanzibar na kumuondoa Sultan. Mipango yote ya mapinduzi, silaha, na wanajeshi walitoka Tangayika.
Ukoloni wa Tanganyika umefanikiwa kuingia na sasa unatimiza miaka 53. Ukoloni huu umekabiliana na upinzani muda mfupi tokea kuanza himaya yake. Lakini dhahiri ni baada ya miaka 8 tu ilipofikia hatua kubwa na ndio sababu ya kifo cha kiongozi na Rais wa Zanzibar, Sh Abeid Aman Karume. Pamoja na juhudi za kuimarisha himaya yake, Ukoloni wa Tanganyika, ndio juhudi za wananchi zilivyokuwa zinaongezeka. Kuondoshwa madarakani na kuekwa kizuwizini Rais mwengine wa Zanzibar Sh Aboud Jumbe Mwinyi, ilikuwa ishara nyengine ya kuupinga Ukoloni wa Tanganyika. Hadi sasa Wazanzibar wanaendelea na juhudi zao za kuuondosha Ukoloni huu wa Tanganyika.
Leo nataka tutazame jee ni muda gani Ukoloni wa Tanganyika utadumu kuitawala na kuikalia nchi yetu ya Zanzibar?
Mimi nampa Mkoloni miaka 53 mengine, hivyo itakuwa miaka 106 jumla. Ingawa miaka 53 ijayo nitakuwa sipo tena dunia, wale watakao kuwepo naomba munitumie japo text message. Tukisoma waliyofanya mababu zetu zama zao, tukachanganya na ya kwetu kwa zama zetu sinashaka muda huu unaweza kufupika.
Wakati wa kumtowa Mreno wananchi wa Msikitichooko, Tumbe na Mkamandume, kwa nyakati tofauti walikuwa mstaari wa mbele na walionyesha ujasiri na mbizu za hali ya juu.
Mambo manne yafuatayo ni muhimu kuwa nayo, pengine yanaweza kupunguza muda wa kutawala:
1. Nia: bado hatuja nuwia ipasavyo. Wengi bado hawajautambua ukoloni huu, wanadhani ni muungano. Hivyo kuupigia chapuo hasa pale anapopewa kipande cha ardhi kulima au pale anaporuhusiwa kuuza vitambaa vyake.
2. Ujasiri: bado wengi wetu ujasiri wetu uko level ya chini. Kulalamika zaidi kuliko kukabili udhalilishwaji.
3. Mbinu: wasomi wetu bado hawajazaa mbinu (model) wa kumkabili mkoloni na kumshinda. Hasa tukitilia maanani muda na mazingira tuliyonayo. Ukisoma namna Mreno alivyopigwa kule Msikiti Chooko, Tumbe ilikuwa wananchi walimwaga tunda zenye miba njia zote, kisha wakaanzisha tifu. Mkoloni alipokuwa anakanyaga tunda zenye miba anaanguka wanamkata kwa upanga.
4. Fedha: umasikini nao unaturudisha nyuma kwani tunashindwa hata kumudu mahitajio yetu wakati wa kupambana na mkoloni.
Mtawala anaendelea kujidhatiti na kuimarisha himaya yake. Hatuna budi Wazanzibar nasi kwa upande wetu kuongeza juhudi na kukabiliana na kila hatua Mkoloni anayojipangia.
Kutoka Mzalendo net.