Kwa mtu mwenye akili timamu huwezi kuwa mfuasi wa mwanasiasa

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
5,347
11,447
Miaka yangu yote 40+ niliwahi kuwa mfuasi wa mwanasiasa nilipo kuwa kwenye 10s, nilipokuja kupata akili niliacha kumfuata mwanasiasa nikawa nimetengeneza tabia ya kuangalia hoja za mwanasiasa husika.

Wanasiasa wa Tanzania ,Afrika na pengine dunia nzima siyo waaminifu, ni vigeu geu waongo na hawana misimamo. Nadhani wa Tanzania ni zaidi hawana aibu ni wapuuzi na wanafiki wanajali matumbo yao tu.

Unaweza enda linda "kula" ya mtu ukidhani unalinda "kura" zako. Kumbe ni " kula" yake. Wanasiasa vigeu geu hawaaminiki.

Angalia maisha yako. Wanaokusifu leo kesho hawatakuwa nawe. Nani anakumbuka kuwatumia pesa wazazi/mke wa Ben Saanane?
 
Unapokazana kuhakikisha anakuwa Mbunge ukiamini anataka kuwasaidia wananchi kumbe anataka isaidia familia yake.keshokutwa anaenda chama ambacho alikuwa anasema hakifai,cha hovyo n.k kwa sababu amegundua huko aliko sasa hapawezi mpa tena nafasi ya kuwa Mbunge. Au anapohama chama hiki sababu kakatwa /hajapitishwa kuhamia kile halafu akiona kule nako hakueleweki anarudi huku.

Unalindaje kula ya mtu ??
 
Back
Top Bottom