Kwa mtu mwenye akili na busara hili ni tusi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa mtu mwenye akili na busara hili ni tusi.

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by BWAXY, Sep 9, 2010.

 1. B

  BWAXY Member

  #1
  Sep 9, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ushabiki wa vyama hauna maana ndugu zangu.tufungue macho yetu, masikio yetu na akili zetu tuangalie mambo ya msingi yanayogusa taifa letu kwa ujumla wake.

  Angalia rasilimali zilizoko nchini zimetumika kwa kiasi gani na zimemnufaisha nani?
  Angalia usimamizi wa sera na mipango ya serikali iliyoko madarakani sasa na utekelezaji wa ahadi tunazopewa kila siku zimetufikisha wapi?
  Karibu miaka 50 ya uhuru bado tunadanganyika, hatujiamini, hatujapata elimu ya kutosha na fikra zetu kweli bado ni butu kiasi cha kushindwa kuingia mikataba yenye tija kwa taifa letu au tunafanywa mazoba?
  TULIWAVUMBIKA CCM WAKIWA WABICHI TUKAJISAHAU WAKAIVA KUPITILIZA SASA TUKIJIFANYA MABINGWA WA KUVUMBIKA WATATUOZEA MIKONONI TUNUKE WOTE.MWENYE AKILI HAWEZI KUFANYA HIVYO.

  Nani leo hii anaweza kuniambia serikali ya kikwete imewafanya nini mafisadi waliofichuliwa na bunge, kama si ubabaishaji ili mradi siku ziende na kiini macho cha kesi mahakamani ziishie kiholela.hivi kweli mbona kibaka mtaani akiiba haambiwi arudishe na iwe ndio amesalimika? Iko wapi kesi ya zombe aliyoingia nayo kikwete kwa mbwembwe tukapambiwa kwenye magazeti kuwa ni jambazi na sasa anakula good time. Hivi kweli anayeiba mabilioni ya fedha na kulisababishia taifa hasara ndiye wa kufungwa miaka miwili tu? Huyu si ni sawa na mbakaji wa uchumi wa nchi? Tunakwenda wapi jamani na udanganyifu huu? Taifa hili lililojengewa misingi mizuri na j.k.nyerere ya kuchukia rushwa, misingi ya kuheshimiana na misingi ya kutokuwa na ubaguzi wa aina yoyote,taifa lenye amani inayoridhisha inashangaza kuendelea kuwa masikini ilihali tuna rasilimali za kutosha.
  HAPA SASA NAKUMBUKA STATEMENT YA BALOZI WA MAREKANI HAPA NCHINI ALIPOSEMA “TANZANIA ISIPOJICHUNGUZA KWA NINI HAIENDELEI WAKATI INAPATA MISAADA MINGI NA INA RASILIMALI NYINGI KULIKO NCHI NYINGI ZA AFRIKA HAITAKAA IENDELEE DAIMA”. AKUTUKANAYE HAKUCHAGULII TUSI.KWA MTU MWENYE AKILI NA BUSARA HILI NI TUSI.
  Unajua mimi siamini kabisa kuwa akili zetu zimelala kiasi kwamba tunashindwa kutambua ya kuwa kuna wazembe wengi sana huko serikalini, wanaofanya kazi ilimradi wapate mshahara, hawatumii profession zao kutatua challenges (changamoto) zinazolikabili taifa.hawa hawatufai jamani.lets be serious ndugu zangu black is black and white is white,lets call spade, a spade ndipo tunaweza kuona mabadiliko. Ccm inafahamu kuwa katika taasisi za elimu ya juu, wanafahamu nini wanaambiwa na wanajua kutafakari. Wanapodanganywa wanajua tumedanganywa na penye ukweli wanajua huu ni ukweli, halikadhalika maeneo ya mjini.hawana mtaji huko. Wanakimbilia vijijini na ngoma zao wakapate wa kuwadanganya. Kauli mbiu ya maisha bora kwa kila mtanzania imeishia wapi? Mimi sihoji watanzania kupewa maisha bora ila ni mazingira gani watanzania wamewekewa ili wajitafutie maisha bora? Yako wapi?
  My friends, taifa hili linahitaji ukombozi wa kweli.utakaotutoa kwenye mikataba mibovu isiyokuwa na tija kwa taifa, utakaowakurupua mafisadi wote huko serikalini, utakaopunguza matumizi makubwa ya serikali na kuelekeza fedha hizo katika maendeleo, ukombozi wenye kutoa dira kuu ya taifa na si kushabikia uanachama. Wewe unayesoma ujumbe huu una nafasi yako ya kuleta mabadiliko. Jiulize umelifanyia nini taifa lako la tanzania? Hata kwa kulichagulia kiongozi bora tu anayeonesha uhai katika kupambana kwa vitendo na matatizo mengi ya nchi yetu. Lets Wake up and dare for change!!
   
 2. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #2
  Sep 9, 2010
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  point nzuri kabisa tunaongoza kwa kupokea misaada toka Nchi za magharibi lakini faida hatuioni ni ufujaji wa rasilimali za Taifa na siasa zisizo na mashiko kwa watu masikini, ushabiki wa ovyo bila kuangalia hali halisi ya maisha
   
 3. B

  BWAXY Member

  #3
  Sep 9, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Jiulize umelifanyia nini taifa lako la tanzania?
   
 4. Beauty

  Beauty JF-Expert Member

  #4
  Sep 9, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 540
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Binafsi nimelifanyia mambo mengi sana mazuri taifa langu, lakini naona waendesha Taifa hawapendi nilitendee Taifa langu haki, haki,rasilimali etc, zinayeyuka bila mimi mwananchi kupewa ukweli wa mambo, basi shida tupu.
   
 5. B

  BWAXY Member

  #5
  Sep 9, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hapa sasa nakumbuka statement ya balozi wa marekani hapa nchini aliposema "tanzania isipojichunguza kwa nini haiendelei wakati inapata misaada mingi na ina rasilimali nyingi kuliko nchi nyingi za afrika haitakaa iendelee daima". Akutukanaye hakuchagulii tusi.kwa mtu mwenye akili na busara hili ni tusi.

  wewe una maoni gani?
   
 6. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #6
  Sep 9, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ifikie wakati iyo misaada ikome,wamerekani hao hao wameleta MCC kujenga mabarabara kumbe lengo lao kuondoka na URANIUM yetu na madini zingine.
  Yaani Tz twaonekana mazoba at the expense of watu wachache wasiojua ata nini maana ya kuwa Viongozi
   
 7. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #7
  Sep 9, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Hilo jina lako inaonessha weye ni bingwa wa kupigishwa rivas. nisahihishe kabla sijakuomba radhi
   
 8. B

  BWAXY Member

  #8
  Sep 9, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  unamaanisha nini?
   
 9. B

  BWAXY Member

  #9
  Sep 9, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kwa hawa wote wanaotoa maoni mazuri humu ndani ni wangapi watapiga kura kumchagua huyo kiongozi bora?
   
Loading...