Kwa mtu aliye nitukana kwa sms!

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,247
2,000
Naomba kuuliza mimi ninamtu namjua amenitukana na kunikashifu kwa kunitumia sms lakini yeye anaishi shinyanga mimi ninaishi tanga je nini naweza kufanya ili hatua za kisheria nizifate??Tafadhali nisaidieni!!
 

Slave

JF-Expert Member
Dec 6, 2010
5,314
2,000
Nenda katoe taarifa polisi. Wakitaka ushahidi utaupata kupita oprt wako kama zain,voda ,ttcl, etc.
 

Gsana

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
4,383
1,500
Mpotezee tu! Au unataka kumkomoa? Usijipe muda wa kumfikiria na ataumia sana kwa nini hukumjibu,kwake utakuwa umemtusi sana kwa kutomjibu!
 

Mokoyo

JF-Expert Member
Mar 2, 2010
15,150
2,000
kama unamfahamu mwambie asante, halafu kaa kimya, atakuja kukuomba msamaha one day
 

Kisanduku

JF-Expert Member
Jul 9, 2009
247
500
Una haki ya kumshaki kwa kutumia sheria ya mawasiliano. Nenda polisi chukua RB. Baada ya hapo nenda kwenye mtandao wa namba yake waifunge.

Kisha namba mwenye namba hiyo atakaporipoti kufungiwa simu yake basi palepale anakamatwa na gharama za kesi toa alipo hadi ulipo zilipwe na yeye.

Ikiwezekana kesi hii ikashuhudiwa na wanahabari na ikaandikwa magazetini basi itakuwa fundisho kwa wote wennye mchezo huu.
 

Quinty

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
463
225
Kutoa lugha ya matusi ni kosa kisheria. Kuna sheria aina Mbili moja iko ile ya kanuni za adhabu na nyingine sheria ya madhara...kwa sheria ya madhara lazima uonyeshe umedhurika na hayo matusi na pia kuna mtu mwngine zaidi ya ww amesoma huo ujumbe...kuhusu madhara haimaanishi uumie ila onyesha umedhurika kibiashara au kijamii inayokuzunguka...hapo utadai fidia na kupata pesa ya kutosha. Ukienda na sheria ya kanuni za adhabu hutapata fidia interms of cash ila uliyemtuhumu atafungwa. Naomba nikupe angalizo kwamba kudhibitisha hili itakuwa bila shaka yeyote ambayo ni ngumu so kama mtoa ushauri nakushauri uende kushtaki kwa sheria ya madhara ambayo ni rahisi kuthibitisha na mwisho wa siku utapata fidia.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom