Kwa mtini tujivunje! Yatokeapo haya wewe waona nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa mtini tujivunje! Yatokeapo haya wewe waona nini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Calnde, Nov 21, 2008.

 1. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #1
  Nov 21, 2008
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Uonapo viongozi wanaonesha dhahiri ni wavivu wakufikiri na wepesi wa kusahau,uonapo migongano ya wenyewe kwa wenyewe ndani ya chama chao 'tukufu',uonapo wananchi wanamdhihirishia mkuu wao kuwa wamemchoka hata kufikia hatua ya kutaka kumbonda mawe,uonapo wezi wanabembelezwa kurudisha fedha ili wasifikishwe mahakamani ili hali walioongoza migomo vyuoni kudai wanachoamini ni haki yao wanapandishwa kizimbani hata kabla ya uchunguzi kuanza,uonapo kila kundi katika jamii limechoka na diplomasia na kuona migomo ni njia sahihi,uonapo nchi imefikia mahali swala la kitaifa linakabidhiwa kwa chama tawala kwa ajili ya utekelezaji na kila mtu hata katibu mwenezi wa chama anaouwezo wa kutoa tamko la kitaifa,unonapo vyuo vinafungwa na watawala wanaimba tunaboresha elimu kufuta ujinga,uonapo maisha yanakuwa magumu na wakuu wanaimba uchumi unapaa,uonapo yote yanatukia na mkuu wa kaya yupo kama vile hayupo......

  Kisha uonapo kauli tamu kama vile MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA zinatoweka......

  Binafsi naona mwisho mbaya wa chama tukufu kuparanganyika,kuanguka,kuvunjika na kuteketea hata kama si leo basi ni kesho.Sioni matumanini yaliyoujaza uso wa JK mwaka 2005,sioni ujasiri wa Kina Lowassa walioanza nao,naona mwisho mbovu uliojaa aibu na fedheha kwa wakuu hawa...
  wewe waona nini?
   
  Last edited: Nov 21, 2008
 2. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #2
  Nov 21, 2008
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kijana umeandika ukweli mtupu, lakini kuna kipengere kimoja tafadhali naomba kutokubaliana na wewe, pale uliposema CCM CHAMA TUKUFU. CCM si chama tukufu kwani kimejaa wezi, majambazi, wauza unga, majangili, mafirauni na uchafu wote wa shetani.
   
 3. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #3
  Nov 21, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kidatu,

  Nafikiri Calnde hakumaanisha kukitikuza CCM.

  Ona "chama chao" halafu ona "tukufu" ilivyowekwa katika quotes.

  Amebonda sawia, highlighting what we are fighting for and waht we are fighting against to the point.
   
  Last edited: Nov 21, 2008
 4. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #4
  Nov 22, 2008
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0


  Wanataka tuamini hivyo,wauaminishe umma wa watanzania kwamba wao ni safi,huwa hawakosei na kwasababu wao ni wakongwe basi yote wayafanyao ni sahihi! Laiti wangekubali kuwa hata mzee pia aweza kukosea na wakakubali kujirekebisha aibu itakayowakumba muda si mrefu yumkini ingewapitia.
  lakini kwa kiburi chao na uvivu wa kufikiri lazima wataaibika.Naam hata sasa wamekwisha aibika!
   
Loading...