Kwa Mtindo huu Tanzania ni ya Mafisadi na Maskini

Is Tanzania still Tanzania??

  • Total voters
    14

Expedito Mduda

JF-Expert Member
Sep 22, 2009
381
225
Tazameni ndugu zangu,
Huko CCM palikuwa na watu wachache waliokuwa ni watetezi wa watu. Mmojawapo niliyemwona akifanya hiyo kazi pamoja alikuwa bado kwenye chama cha mafisadi alikuwa mheshimiwa Sitta.
Mheshimiwa Sitta alikuwa anasimamia maslahi ya ya watu. Mwisho wa bunge lililopita kila mtu alitamani bunge linalofuata liwe kama lililopita na hata kulishinda kwa umahiri wa kusimamia maslahi ya taifa.
Katika kusimamia maslahi ya taifa kuna mambo kadhaa wa kadhaa ambayo mtu lazima ujitoe sadaka. Mmojawapo ni kuhakikisha unakuwa na msimamao wako binafsi na hasa nguvu ya kuwapinga mafisadi. Sitta aliweza kufanya hivyo na kwa maana hiyo alikuwa kwenye kundi la wapiganaji.
Kwa msimamo huu, bunge lilichangamka sana na lilifanya kazi kubwa kiasi kwamba liliwafunua mafisadi wengi mpaka wengine katika serikali wakatakiwa kujihudhuru na serikali kuvunjwa na nyingine kuundwa upya.
Bunge jipya limeundwa na spika mpya madam Anna Makinda yule aliyesema hakuna kupunguza posho za wabunge na pengine atahakikisha inaongezwa.
Kwa sasa Sitta alikuwa anahitajika kuwa spika wa bunge. Kwa kuwa alikuwa mwiba kwa mafisadi, wamefanya njama na kuhakikisha hapiti tena katika nafasi hiyo ili mafisadi waendelea kula nchi kwa uma na mrija.
Leo hii wanakuja na kisingizio cha jinsia. Kwani hiyo jinsia ni kwenye uspika tu? Kwa nini jinsia leo na siyo juzi au kesho? Jamani Kwa Tanzania ukiwa mtetezi wa wanyonge mafisadi wanakutoa kafara: Sitta ametolewa kafara.
Walipoona kumpeleka bungeni ili wabunge wasema kama bado wanamhitaji atapita, basi wakaona waje na ujinsia! Lakini hivi nyie Watanzania mmella usingizi wa mtindo gani?
Lakini pia watu kama Sitta mnasubiri nini huko mliko? Kwani huko mliko ndo mama yenu na baba yenu? Ondokeni!!
Ndugu zanguni mafisadi tunaomba mtuhurumie, Watanzania wenzenu tunakufa. Mwache hao watetezi wetu waendelee kututetea.
Anna Makinda umefurahi sana kuchaguliwa sijui kama unamjua aliyekuweka hapo! Ni juu yako kuamua kumtumikia na kuwatosa Watanzania wenzako au kumtosa huyo na kuwatumikia Watanzania wenzako.
Ni jukumu letu sote kuwa macho na mtindo huu mchafu na kuhakikisha tunakemea haya tusije tukaporwa nchi yetu kweupe mchana. Tuwe waangalifu sana na madaraka tunayowapa watu maana itategemea na uwezo wao wa kufikiri. Hayo nayo wanaweza wakawa hawayajui. Wanauza nchi bila kujua.
Mimi nasema kwa sasa Watanzania tuamke tuilinde nchi yetu.
 
CYPRIAN MKALI

Senior Member
Nov 12, 2010
176
225
mimi nakerwa sana na suala la kuzungumzia jinsia tukaacha uwezo wa mtu kulitumikia taifa. simpondi kwa jinsia yake lkn kigezo kikubwa kisiwe jinsia, tuangalie je anaweza. kweli mkono wa mafisadi ni mrefu.
 
Kashaijabutege

JF-Expert Member
Oct 20, 2010
2,696
1,195
mimi nakerwa sana na suala la kuzungumzia jinsia tukaacha uwezo wa mtu kulitumikia taifa. simpondi kwa jinsia yake lkn kigezo kikubwa kisiwe jinsia, tuangalie je anaweza. kweli mkono wa mafisadi ni mrefu.

Dr. Stock 10,000,000
Cr. Cash 10,000,000

Being recording of stock purchased by cash.

JV prepared by................................Checked by..............................Approved by..............................Date......................

Hii fani mama huyu angeiweza sana.
 
NKINKI

Member
Nov 1, 2010
8
0
Watanzania tumelala na tumeridhika sana na shida zetu. Tunasadiki hata kuuza haki zetu za kidemokrasia kwa maslahi ya vyama vyetu vya kisiasa badala ya maslahi ya nchi. Mimi naimani huyu mmama hataweza kuendeleza vita dhidi ya wala nchi (mafisadi)

Lakini siku watanzania wakizinduka usingizini mafisadi wote mtasaga meno
 
Expedito Mduda

JF-Expert Member
Sep 22, 2009
381
225
Kwa kweli tumelala ki kweli na usingizi unatumaliza kwisha kabisa!! Nchi ndo inaondoka hiyooooooooooooo!!
 
Mtumishi Wetu

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
5,703
2,000
Hapana mkuu nchi bado ipo tu! Wao wanazo fedha za ufisadi lakini sisi tunaye Mungu wetu anayechukia uovo. Wataporomoka kama mnara wa Babeli, subiri uone Mungu wetu alivyo na maajabu mengi tu. Mpambano ndio yameanza.

Our lives begin to end the day we become silent about things that matter. Martin Luther King Jr.
 
Fishyfish

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
231
0
CCM has been killing Tanzania for a while now.

The good news is, the new generation of Tanzanians are not oblivious to this fact. Expect significant things to unfold over the course of the next 5 years.
 
Kaa la Moto

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
7,694
2,000
Tazameni ndugu zangu,
Huko CCM palikuwa na watu wachache waliokuwa ni watetezi wa watu. Mmojawapo niliyemwona akifanya hiyo kazi pamoja alikuwa bado kwenye chama cha mafisadi alikuwa mheshimiwa Sitta.
Mheshimiwa Sitta alikuwa anasimamia maslahi ya ya watu. Mwisho wa bunge lililopita kila mtu alitamani bunge linalofuata liwe kama lililopita na hata kulishinda kwa umahiri wa kusimamia maslahi ya taifa.
Katika kusimamia maslahi ya taifa kuna mambo kadhaa wa kadhaa ambayo mtu lazima ujitoe sadaka. Mmojawapo ni kuhakikisha unakuwa na msimamao wako binafsi na hasa nguvu ya kuwapinga mafisadi. Sitta aliweza kufanya hivyo na kwa maana hiyo alikuwa kwenye kundi la wapiganaji.
Kwa msimamo huu, bunge lilichangamka sana na lilifanya kazi kubwa kiasi kwamba liliwafunua mafisadi wengi mpaka wengine katika serikali wakatakiwa kujihudhuru na serikali kuvunjwa na nyingine kuundwa upya.
Bunge jipya limeundwa na spika mpya madam Anna Makinda yule aliyesema hakuna kupunguza posho za wabunge na pengine atahakikisha inaongezwa.
Kwa sasa Sitta alikuwa anahitajika kuwa spika wa bunge. Kwa kuwa alikuwa mwiba kwa mafisadi, wamefanya njama na kuhakikisha hapiti tena katika nafasi hiyo ili mafisadi waendelea kula nchi kwa uma na mrija.
Leo hii wanakuja na kisingizio cha jinsia. Kwani hiyo jinsia ni kwenye uspika tu? Kwa nini jinsia leo na siyo juzi au kesho? Jamani Kwa Tanzania ukiwa mtetezi wa wanyonge mafisadi wanakutoa kafara: Sitta ametolewa kafara.
Walipoona kumpeleka bungeni ili wabunge wasema kama bado wanamhitaji atapita, basi wakaona waje na ujinsia! Lakini hivi nyie Watanzania mmella usingizi wa mtindo gani?
Lakini pia watu kama Sitta mnasubiri nini huko mliko? Kwani huko mliko ndo mama yenu na baba yenu? Ondokeni!!
Ndugu zanguni mafisadi tunaomba mtuhurumie, Watanzania wenzenu tunakufa. Mwache hao watetezi wetu waendelee kututetea.
Anna Makinda umefurahi sana kuchaguliwa sijui kama unamjua aliyekuweka hapo! Ni juu yako kuamua kumtumikia na kuwatosa Watanzania wenzako au kumtosa huyo na kuwatumikia Watanzania wenzako.
Ni jukumu letu sote kuwa macho na mtindo huu mchafu na kuhakikisha tunakemea haya tusije tukaporwa nchi yetu kweupe mchana. Tuwe waangalifu sana na madaraka tunayowapa watu maana itategemea na uwezo wao wa kufikiri. Hayo nayo wanaweza wakawa hawayajui. Wanauza nchi bila kujua.
Mimi nasema kwa sasa Watanzania tuamke tuilinde nchi yetu.
Yaani unawaomba mafisadi wakuhurumie? Why? Tunatakiwa kuwanyang'anya kwa nguvu. Hili linawezekana! Siwezi mbembeleza mwizi kurudisha mali yangu aliyoiba.
Ombea watanzania majuha ambayo yanatoa kura kwa kupewa kanga na kofia! Mimi mpaka sihitaji mtu aje kwamgu kuomba msaada. Hata kama yuko karibu na kufa, basi kila mtu abebe own cross.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom