Kwa mtindo huu kuikomesha rushwa ni ndoto

BONGOLALA

JF-Expert Member
Sep 14, 2009
16,507
11,883
Tumeshuhudia leo RC dsm akisema bila woga kuwa alipewa sh 147m na marehemu Mengi eti akalipe deni,Jee sheria zetu za rushwa zinaruhusu mtu mwenye mamlaka fulani kupokea pesa bila utaratibu wowote wa kiserikali au jamii kama fund raising.

Jee ni wafanyabiashara wangapi wanaliliwa shida na huyu RC na kumoa pesa kwa jambo hilo hilo?kila kukicha anabadilisha magari ya kifahari safari za dubai na afrika kusini hapo hapo anawanyima raha wafanyabiashara kwa kuwaomba pesa.

Kwa kweli kama tuna nia ya dhati kukomesha rushwa basi sheria ikataze haya mambo, hivi vijizawadi hata Mwalimu alivikemea sana ila kwa sasa ni too much kwa huyu RC na anaidhalilisha serikali ya awamu ya 5.
Jee marehemu angeenda kesho yake ofisini kwa RC na kumueleza shida yake huyu RC angekua na uwezo kupima jambo au angetolea maamuzi ya kumfurahisha huyu aliyempa pesa jana?

Haya ni matumizi mabaya ya ofisi kutumika kujinufaisha binafsi
 
Hivi ukiwa kiongozi hata private issues zako na mtu yeyote lazima ofisi yako iusike...?
 
Back
Top Bottom