Kwa mtindo huu kina Lugumi na Wazawa wengine watashindwa kuwekeza

Fabian the Jr

JF-Expert Member
Aug 4, 2012
756
743
Ni mara nyingi tumeona kamati za Bunge , zikiongozwa na PAC , zikiwahukumu Watanzania kwa namna ambayo inaonyesha wamekariri .
Wamekariri kwamba , ili kamati ionekane inafanya kazi ni lazima ionyeshe kwamba kuna Mtanzania ameiba mahali. Kukariri huko kumewafanya kushindwa kuwa makini na kuwazushia watu wengi kashfa za Ufisadi, ili mwisho wa siku waonekane wao ni wasafi.

Hasa baada ya Mzee Lowasa kushughulikiwa na ile kamati ya kina Mwakyembe enzi zile. Mpaka leo, hakuna ushahidi wa kueleweka wa nini kiliwafanya wamhukumu Edward Lowasasa, sana sana kinachoonekana ni kwamba jambo lile lilisukumwa na visasi vya kisiasa ndani ya Chama chao cha Mapinduzi.

Napata hofu kwamba somo hili la Kukariri litawaumiza Wazawa wengi. Mpaka sasa tumesikia watu wengi wameondolewa ktk nafasi zao za kazi lakini baadae hakuna ushahidi au inathibitika kwamba hawakufanya ubadhilifu .
Hivi karibuni lilisikika sakata la Bwana Said Lugumi, mfanyabiashara wa Kitanzania ambae alipata Tenda halali ya kusambaza mashine za kudect alama za vidole kwenye vituo vya polisi nchini.

Kwa mtindo ule ule wa kukaririshwa kwamba ni lazima kuwachafua Watanzania wengine ili wewe uwe msafi, ; Wanasiasa wetu walijaribu kulazimisha kwamba Lugumi hajatekeleza mkataba. Wengine walizusha kwamba amekimbia nchi.

Cha ajabu ni kwamba imeonekana Lugumi yupo nchini, na zaidi ya yote mashine zimefungwa kama Mkataba ulivyotaka. Lugumi hana makosa.

Hofu ninayopata kwa haya yanayoendelea : Watanzania watapata hofu na watashindwa kuomba Tenda katika nchi yao. Mamlaka ni kama "zimepanic" na zinaongozwa na hisia kwamba kila Mtanzania alipowekeza, au alipopata Tenda baasi ni lazima kuna rushwa.

Sasa jamani mnataka hizo Tenda ziende kwa kina nani?
Mtu kama Lugumi imethibitika alifuata sheria zote katika kupata mkataba, na ameutekeleza.

WANASIASA WAACHE TABIA YA KUPAKAZIA WATU NA WAACHE KUTOPOTOSHA KWA LENGO LA KUJIONGEZEA UMAARUFU.
WASIKARIRI; UNAWEZA KUCHAPA KAZI BILA KUCHAFUA WATU WENGINE.
 
Wezi ni haki kuhukumiwa!
Mbona Mengi na IPP yake anaendelea vema.
Stick to the business roadmap and follow the rules of the game.
 
Mkuu, hapa unataka ku pre empty kitu gani? Kama kampuni ya Lugumi ilifanya biashara halali kwani tatizo liko wapi, si itajulikana tu - kwa nini hatutaki kuvuta subira mpaka uchunguzi wa kina ukamilike kwanza - kama una uhakaki hukufanya lolote lenye walakini kwa nini uji feel jumpy jumpy muda wote??
 
Hizi kamati za bunge zimetawaliwa na visasi na njaa(wengi wamekopa) sasa ili wapate mwanya wa kuomba rushwa lazima waibue figisu figisu...
 
Mtoa mada, mie nikuhoji tu kama kweli unayo hakika kuwa Lugumi walitekeleza wajibu wao wa ufungaji wa mashine za finger print kama mkataba ulivyoelekeza tangu 2011 na kustahili malipo ya zaidi ya 90% ya pesa ya mkataba?
 
Back
Top Bottom