Kwa mtindo huu Jairo hakupaswa kudhalilishwa na Watunga Sheria Namna ile

Avanti

JF-Expert Member
Aug 24, 2010
1,209
239
Nchi hii bana! kuna mtu nimemsoma akisema: "Nikigeuka huku nasikia wabunge hawajadili mambo ya msingi isipokuwa posho zimebunywa, na mbunge fulani kwamwambia 'hawara yake' afupishe safari". Ukweli tena hamna mtetezi wa wanyonge aliyekuwa akitegemewa kama Bunge hapa nchini kwetu. Hata sheria nyingi zinapojadiliwa kutungwa huwa mijadala inaelekea kulipa nguvu bunge katika utekelezaji wa sheria hizo. Mfano, kumekuwa na mijadala sana kwamba Bunge liwe linahusika katika uteuzi wa viongozi mbalimbali hapa nchini ikimaanisha kuwa Rais ana mamlaka makubwa sana katika nchi hii katika kuamua mambo mbalimbali na hasa uteuzi wa viongozi wa juu.

Leo nimekaa na kufikiri sana na kugundua kuwa ni afadhali ya Watendaji (Executive) kuliko Bunge. Miaka ya nyuma Bunge lilimkamia Jairo, yule Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini kwa ajili ya mambo haya haya yanayofanywa na wabunge (ambapo imedhihirika ni siku zote). Wabunge hawa hawa walikomaa na Jairo hadi akasimamishwa kazi. Leo hii natammbua kumbe wabunge wenyewe wananuka, tena wananuka kuliko hata Jairo, mtoto wa watu (ukumbuke Jairo alikuwa akipendwa kazini kwake). Leo hii wabunge hawa watajisafisha vipi kwa uchafu wao huu? Kelele wanazopiga nawaona ni kama waigizaji tu. Juzi mbunge mwingine anakiri kuwa wabunge wote wana wapenzi wao humo bungeni (labda ukiondoa mbabe Anne Makinda). Hii inamaanisha kuwa kumbe Dodoma ni sehemu ya kwenda kuhalalisha mapenzi na uozo wa kila aina kwa wabunge wetu.

Wabunge wetu wamechafuka, tena wamechafuka sana, tukimbile wapi sasa nchi hii? Nikigeuka huku wote wachafu, sio vyama vya kisiasa, vingozi wa kidini, nk, wote wachafu tu! Najiuliza leo hii hivi JK akiamua kumrudisha Jairo, kuna mbunge ambaye atasimama na kumrushia jiwe Jairo ama JK mwenyewe kwamba kwa nini kamrudisha fisadi mwenzao? Labda mbunge huyo awe mwehu! Kwa sababu sioni mbunge aliye msafi kiutashi na kimatendo, kuna wala rushwa, wabunya pesa, wasaliti, wazinzi, vigeugeu, wanafiki, n.k.

Nimechoka mimi na sina pa kukimbilia nchi hii.....
 
Back
Top Bottom