Kwa mtazamo was naibu waziri wa afya sijui Kama tutafika

pakamwam

JF-Expert Member
May 28, 2013
516
651
Nimeshangaa Sana kuona mahojiano ya naibu waziri waa afya akiwasema wataalamu wa maabara kuwa wanatoa majibu ya uongo pia na madaktari alikosoa prescription ya dawa zao. Huu mtazamo Ni potofu na unarudisha nyuma juhudi zinafanywa kushawishi wananchi kwenda hospitali
Haingii akilini waziri mwenye dhamana anapoanza kulalamika alafu inaonyesha hajui uhalisia uliopo kwenye hospitali zake. Kama anaona tatizo na a haja ya media ni kurekebisha kwa sera na utendaji na kuwasimamia vizuri waliochini yake

Labda nianze kwa kuelezea kipimo Cha typhoid
Typhoid inaweza kupimwa kwa vipimo vingi lakini vifuatavyo ndio rahisi vinatumika hapa nchini kwetu

Mgonjwa au daktari akiomba uchunguzi wa typhoid maabara hufanya hivi

Kwa watamfanyia widal test
Hii widal iko makundi mawili
1.slide agutinagion
2. Titration ambayo huchukua reagent nyingi
Kwa uelewa wa kawaida huwa wanaanza slide agutinagion kama screening test alafu ukipata positive unaendelea n titration ambayo unatakiwa kusubiri hadi masaa 24. Kama kwenye slide agglutinagion ni negative mgonjwa hana haja ya kusubiri kesho majibu

Kipimo cha pili ni kwa baadhi ya hospitali hasa za rufaa
kuwaotesha wadudu kama wapo kwenye damu (blood culture) na kuangalia uwepo wao kwenye kinyesi kama agglutinagion imekuwa positive. Kuotesha wadudu kwa kutumia kinyesi inaweza kufanyika baadhi ya hospitali pia
Uotaji wa wadudu hawa kwenye vyakula tulivyopandikiza hutegemea kama mgonjwa hajatumia dawa. wagonjwa wetu wengi huja wakiwa wametumia dawa.
Waziri anaposema maabara wanakuja na majibu yasiyo ya kweli awe na ushahidi wa tafiti na sio hisia tu.
Alizungumzia mambo ya homa za virusi. hakutakiwa kutuhumu ili kumake point yake
Lakini pia akumbuke yeye ni mtu wa sera. Ni hekima angewasilina na katibu ili kurekebisha shida iliyopo kama utafiti umefanyika

Pia alizungumzia mambo ya UTI. Mimi sipendi kuongea vitu visivyo na uhakika.wewe ni waziri fanya utafiti na njoo na majibu.
Kuingiza siasa kwenye afya ni kuua afya.
Pia zipo taratibu za kurekebisha mambo na sio njia ya kutafuta populality
Nakubali kuwa yeye ni miongoni microbiologist lakini pia najua hajui kila kitu na mbaya zaidi ameacha taaluma na kwenda kwenye siasa. Inawezekana ukabaki na jina la taaluma alafu usi practice taaluma hiyo.

Tunahitaji viongozi wanaotoa uongozi yakinifu na kutatua matatizo ya kijamii.

Leo unasema maabara wanatoa majibu ya uongo kwenye media unategemea wananchi waende hospitali kupima?.
Ni vyema kujua nafasi yako na madhara ya maneno yako kwa wananchi na mfuumo mzima

Kama tatizo lipo waziri tumia wataalam wako kuyatatua. Lugha kama hizo sio afya kwa jamii
Asanteni
 

Attachments

  • VID-20180921-WA0000.mp4
    5.6 MB · Views: 14
Hongera sana, Pamoja na Kwamba umetoa Claim safi kabisa takatifu Nimejifunza Kidogo Kuhusu upimaji wa Homa ya Matumbo hasa hiyo ya Blood Culture, Nilikuwa Naisomaga tu!
 
Acha wanainchi wasiende hospital na sisi tupumua maana unafika saa mbili unakutana na msururu kama wakipungua kwenda hospitali hiyo ni fursa sasa.

Ata Ummy Mwalimu naye kuna mamb anaborongaga sana. Ukichanganya na siasa kuna mambo yanakuwa ya hovyo
 
Pale mwenye mamlaka anapofika na kuanza kubashiri baadala ya kuja na majibu
Hongera sana, Pamoja na Kwamba umetoa Claim safi kabisa takatifu Nimejifunza Kidogo Kuhusu upimaji wa Homa ya Matumbo hasa hiyo ya Blood Culture, Nilikuwa Naisomaga tu!
 
Nimekuelewa mleta uzi. Nakosa cha kucomment kwenye maelezo ya mheshimiwa
 
Magogoni wanataka makelele kama beberu linasalandia!
Huyu naibu kajikoki mzima mzima bmheeeeee! Mbheeeeee!

Heri yako mleta uzi kwa kuiomba jamii ikiamini kitengo cha maabara.

Sisi tunampuuza n/w
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom