Kwa Mtazamo wa Kiroho: Kwanini mheshimiwa anaishi?

1954tanu

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
1,038
487
Kwa wale wanaoamini Mungu, Mungu aliyeziumba mbingu na nchi, kwa uweza wake hawashangai kwa nini mheshimiwa amekuwa akinusurika katika hila na udhalimu wote unaofanywa gizani hadi hadharani dhidi yake; bali kwao huwa ni kumshukuru Mungu na kumrejeshea sifa, heshima na adhama. Kwa mujibu wa maandiko, kila shauri ambalo waovu wanakaa na kulipanga dhidi ya mwenye haki; Mungu hulibatilisha. Isaya 8:10 '' Fanyeni shauri pamoja, nalo litabatilika; Semeni neno, lakini halitasimama..."

Shauri na mipango ya maadui ambayo waliipanga gizani kuhakikisha wanamwangamiza mheshimiwa; kwa kuwa ulikuwa ni mpango ovu BWANA amelibatilisha shauri la hao waovu. Kifo kupitia mauaji kimebatilishwa. Takribani, risasi za moto 30 hazikuweza kusababisha kifo. Matabibu wanaomganga majeruhi pia wamebaki kushangaa huyu amewezaje kuishi. Muda wote tunajulishwa alikuwa na fahamu zake pamoja na kuwa na majeraha lukuki mwilini mwake.

Tena maandiko yanatwambia, adui zako watakukabili kwa njia moja lakini hao wote watakimbia mbele zako kwa njia saba. Kumb 28: 7 “Yehova atawafanya adui zako wanaoinuka juu yako washindwe mbele yako.+ Kwa njia moja watakuja juu yako, lakini kwa njia saba watakimbia kutoka mbele yako. Adui walimkabiri mheshimiwa kwa njia moja lakini wakakimbia mbele zake kwa njia saba zisizojulikana kwenda kusikojulikana.

Aidha, maandiko yanasema watu waoga hukimbia pasipo na kukimbizwa. Tukio hili limejenga hofu na uoga usio na sababu, wamekuwa waoga hata kwa kadamnasi ndogo tu; hawataki kuiona hususan, linapoonekana kutajwa jina la mheshimiwa. Limewekwa na kubandikwa agizo, eti abadani, walinzi wasiruhusu ibada yoyote iwayo. Hakika waoga hukimbia pasipo na kukimbizwa.

BWANA anasema, adui zako watakushambulia kama nyuki lakini tazama watazimika kama moto wa miibani. Zaburi 118:12 Walinizunguka kama nyuki, Walizimika kama moto wa miibani.
Mheshimiwa alishambuliwa na adui kama nyuki washambuliavyo. Bali watazimika kama moto wa miibani.

Kuna msemo kwamba unapotaka kumwuua mbwa mpe majina yote mabaya, mathalan, mbwa huyu habweki, mbwa huyu hawezi kulinda, mbwa huyu kawa mwizi, mbwa huyu hula vifanga na kukamata kuku, mbwa huyu hashindi nyumbani, mbwa huyu hang'ati, mbwa huyu amegeuka jibwa koko na mengine mengi. Majina hayo yote hupewa mbwa ili kujenga mazingira ya kumuuwa. Mheshimiwa amepewa majina yote mabaya ili watesi wake wawe na sababu ya kumwangamiza.

Kinyume kabisa na hekima ya kibinadamu, maandiko yanasema kwenye kitabu cha Mithali/ Methali. Mtu anayesema mtu mwovu ana haki jamii humchukia huyo asemaye mtu mwovu ana haki. Bali yeye amkemeaye mwovu kwa kumkalipia yeye huyo taifa na jamii humpenda na hubarikiwa. Tangu tukio la kutaka kumwondoa mheshimiwa duniani litendwe taifa limeinuka na kumpenda mheshimiwa. Mithali 24: 24 - 25 Amwambiaye mtu mwovu, Wewe una haki; Kabila za watu watamlaani, taifa watamchukia. 25 Bali kwao wakemeao furaha itakuwako; Na baraka ya kufanikiwa itawajilia.

Kwa mujibu wa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni kwamba michango ya kumchangia majeruhi kwa ajili ya matibabu; imechangwa na watu wenye vipato vya kawaida ukiondoa michango ya wabunge. Mh. Mbowe amesoma taarifa za kibenki zikionesha kwamba wachangiaji wengi ni wale waliochanga kati ya Tsh. 500 hadi 1,000. Kwa kiasi kilichochangwa na watu wenye kipato cha kawaida hadi kufikisha Tsh. 22 milioni ni dhahili kwamba ni watu wengi sana (taifa) waliounganisha fedha zao kidogo ili waweze kwa kipato chao kidogo kutetea maisha ya majeruhi.

Hali hiyo ya watu wenye hali ya kawaida na wa hali ya chini kuweza kufanya hilo walilofanya linaweza linganishwa na kile maandiko yanayokisema kwenye kitabu cha Mithali sura ya 24: 24 hadi 25.

Mheshimiwa hakika Mungu amedhihirisha ni kwa kiasi gani anakupigania kwa kuwa huna hila ndani ya moyo wako. Bwana na azidi kukupigania. Usiwe na kisasi nao maana maandiko yanasema vita hiyo sio yako bali vita hiyo ni ya BWANA. Aidha, kisasi usilipe wewe bali kisasi ni cha BWANA. Warumi 12: 19 Wapenzi wangu, msilipize kisasi, bali mwachieni Mungu jambo hilo; maana Maandiko Matakatifu yasema: "Kulipiza kisasi ni shauri langu; mimi nitalipiza asema Bwana."
 
Ujumbe fasaha umefika.nadhani mkubwa atasoma au ataishia katikati kwa kua matamanio yake ya kumpoteza Lisu hakuyapata mbaya zaidi kila mwananchi ameishaelewa kwamba mkubwa ni muuaji
 
Mipango ya mungu si ya mwanadamu nao walipaswa wapeleke ombi kwa mungu kama shetani alivyo omba kumdhuru ayubu wangefanikiwa wao wametumia fahamu zao aibu imewapata
 
Maneno Kuntu..
Salute sana Mkuu.
 
Ila mkuu heading yako mi ilinihamisha before sijatulia kusoma maana najua waheshimiwa wapo ccm huku kwingine wanaoneka siyo waheshimiwa including lisu
 
Bwana ametenda muujiza mkuu! na hao maagent wa Joka liitwalo shetani, Muongo mkuu, muharibu na muuaji wamechimba shimo na watatumbukia wenyewe!
 
"Zab 104:30, wapeleka roho yako wanaumbwa nawe waufanya upya uso wa nchi" Eh Jehovah fanya upya mifupa, mishipa na kila kitu kilichoharibiwa na risasi katika mwili wa Hon TAL. katika Jina la Yeshua. Amen"
 
Kwa wale wanaoamini Mungu, Mungu aliyeziumba mbingu na nchi, kwa uweza wake hawashangai kwa nini mheshimiwa amekuwa akinusurika katika hila na udhalimu wote unaofanywa gizani hadi hadharani dhidi yake; bali kwao huwa ni kumshukuru Mungu na kumrejeshea sifa, heshima na adhama. Kwa mujibu wa maandiko, kila shauri ambalo waovu wanakaa na kulipanga dhidi ya mwenye haki; Mungu hulibatilisha. Isaya 8:10 '' Fanyeni shauri pamoja, nalo litabatilika; Semeni neno, lakini halitasimama..."

Shauri na mipango ya maadui ambayo waliipanga gizani kuhakikisha wanamwangamiza mheshimiwa; kwa kuwa ulikuwa ni mpango ovu BWANA amelibatilisha shauri la hao waovu. Kifo kupitia mauaji kimebatilishwa. Takribani, risasi za moto 30 hazikuweza kusababisha kifo. Matabibu wanaomganga majeruhi pia wamebaki kushangaa huyu amewezaje kuishi. Muda wote tunajulishwa alikuwa na fahamu zake pamoja na kuwa na majeraha lukuki mwilini mwake.

Tena maandiko yanatwambia, adui zako watakukabili kwa njia moja lakini hao wote watakimbia mbele zako kwa njia saba. Kumb 28: 7 “Yehova atawafanya adui zako wanaoinuka juu yako washindwe mbele yako.+ Kwa njia moja watakuja juu yako, lakini kwa njia saba watakimbia kutoka mbele yako. Adui walimkabiri mheshimiwa kwa njia moja lakini wakakimbia mbele zake kwa njia saba zisizojulikana kwenda kusikojulikana.

Aidha, maandiko yanasema watu waoga hukimbia pasipo na kukimbizwa. Tukio hili limejenga hofu na uoga usio na sababu, wamekuwa waoga hata kwa kadamnasi ndogo tu; hawataki kuiona hususan, linapoonekana kutajwa jina la mheshimiwa. Limewekwa na kubandikwa agizo, eti abadani, walinzi wasiruhusu ibada yoyote iwayo. Hakika waoga hukimbia pasipo na kukimbizwa.

BWANA anasema, adui zako watakushambulia kama nyuki lakini tazama watazimika kama moto wa miibani. Zaburi 118:12 Walinizunguka kama nyuki, Walizimika kama moto wa miibani.
Mheshimiwa alishambuliwa na adui kama nyuki washambuliavyo. Bali watazimika kama moto wa miibani.

Kuna msemo kwamba unapotaka kumwuua mbwa mpe majina yote mabaya, mathalan, mbwa huyu habweki, mbwa huyu hawezi kulinda, mbwa huyu kawa mwizi, mbwa huyu hula vifanga na kukamata kuku, mbwa huyu hashindi nyumbani, mbwa huyu hang'ati, mbwa huyu amegeuka jibwa koko na mengine mengi. Majina hayo yote hupewa mbwa ili kujenga mazingira ya kumuuwa. Mheshimiwa amepewa majina yote mabaya ili watesi wake wawe na sababu ya kumwangamiza.

Kinyume kabisa na hekima ya kibinadamu, maandiko yanasema kwenye kitabu cha Mithali/ Methali. Mtu anayesema mtu mwovu ana haki jamii humchukia huyo asemaye mtu mwovu ana haki. Bali yeye amkemeaye mwovu kwa kumkalipia yeye huyo taifa na jamii humpenda na hubarikiwa. Tangu tukio la kutaka kumwondoa mheshimiwa duniani litendwe taifa limeinuka na kumpenda mheshimiwa. Mithali 24: 24 - 25 Amwambiaye mtu mwovu, Wewe una haki; Kabila za watu watamlaani, taifa watamchukia. 25 Bali kwao wakemeao furaha itakuwako; Na baraka ya kufanikiwa itawajilia.

Kwa mujibu wa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni kwamba michango ya kumchangia majeruhi kwa ajili ya matibabu; imechangwa na watu wenye vipato vya kawaida ukiondoa michango ya wabunge. Mh. Mbowe amesoma taarifa za kibenki zikionesha kwamba wachangiaji wengi ni wale waliochanga kati ya Tsh. 500 hadi 1,000. Kwa kiasi kilichochangwa na watu wenye kipato cha kawaida hadi kufikisha Tsh. 22 milioni ni dhahili kwamba ni watu wengi sana (taifa) waliounganisha fedha zao kidogo ili waweze kwa kipato chao kidogo kutetea maisha ya majeruhi.
Amina.

Back
Top Bottom