Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Kama ndio biashara unayoipenda ifanye, ila usitumbukize mtaji wako wote, karibu kuweka kidogo kidogo huku ukisoma tabia za wateja wako, baadae utakuja kugundua nini wanataka na utafurahia biashara yako.

Usisahau pia kuangalia sehemu ambapo kunashughuli shunguli za kiuchumi na mahali ambapo mzunguko wa watu ni mkubwa.

Nakutakia kila la heri mkuu, maisha ni kupambana, vikwazo vipo ila usiviogope vitakuimarisha pia.
 
hiyo hela ni nyingi sana kama utakuwa makini nayo jaribu biashara ya paspot express inalipa sana printer ya canon kama laki3 camera kama ya laki na nusu inatosha sio lazima uwe na frem waeza kwenda frem ya mtu ukamwomba space ukamtoa kias kwa siku kama sehemu ni potential hasa stand, vyuoni, mahakamani au masokoni, kwenye benk nyingi nyingi au wanapokutana saccos au vicoba hzo sehemu ukipata ukaweka pazia lako waeza pata daily buku 20atleast na ukasahau ajira kadri siku zinasonga unaweza jiongeza ukapata kibanda chako ukawa huru kuongeza hata vitu vingine kama kuuza frem vocha flAsh, memory card,usb cables, etc ukichakalika hyo hela itakukomboa
 
Ujasiriamali ni moja kati ya mambo niliyokuwa nafikiria kwa upana toka nipo O-level hadi sasa nimefika chuo kikuu UDSM. Wakuu mimi nipo mwaka wa kwanza nimefanikiwa kupata mkopo wa elimu ya juu. Boom langu la kwanza nilifanyia biashara ya kupeleka viatu vya kike mkoani na imenipa faida kiasi na sasa naishi kwa kujitegemea yani nimepanga.

Wiki ijayo natarajia kuchukua boom la pili laki 5. Nina kama laki moja nimeitunza, sasa nilikuwa naomba mnipe wazo zuri la biashara kwa mtaji wa laki 6 ili niweze kuendesha maisha yangu ya kila siku na niweze kusaidia ndugu zangu.

NB: Biashara ya chipsi ndio wazo langu namba moja, kama mnaweza kunipa mwanga kuhusu hii biashara kama vile changamoto, faida, vifaa na mawazo mengine nitashukuru sana.
 
OK. Ni wazo zuri ukizingatia umeamua mwenyewe (commitment). Mtaji huo si mbaya kwa kuanzia ila nakupa changamoto baadhi.

1. Chagua location nzuri ambayo itafanya biashara yako iuzike haraka( increase turnover). Kuwe na watu wengi watakaohitaji service yako. Ikibidi itaifanya kuwa more valuable (Price discrimination).

2. Kuwa na usimamizi nzuri katika biashara, coz ukiwa mbali ni rahisi kupoteza mapato.

3. Pata mfanyakazi anaeijua kazi, anaeipenda, zaidi kwenye uelewa na biashara. Hii itakusaidia kuwa na relations nzuri kati wateja wako na biashara yako (B2C). Ni muhimu sana kuwa na relations nzuri kati ya wateja wako na biashara yako, kuanzia mapokezi yako mpaka service yenyewe au product watu wanayoifuata kwako.
Kumbuka hapa ndio mahali unapoonesha utofauti kati ya biashara yako na ya watu wengine.( kwa nini waje kwako na waache sehemu nyingine??)

4. Usisahau usafi, na kuweka hesabu zako vizuri ili kujua progress ya biashara yako. Ikiwezekana kwa kuanzia usichukue/ kutegemea pesa kutoka katika biashara hiyo( Expansion/growing strategy). You may find (if possible) another alternative source for your daily survival for a certain time.

Remember, real success won't come overnight.

Thanks.
 
mchango wako umenipa mwanga wa biashara..ubarikiwe mkuu
 
Mkuu unaweza fafanua kidogo hapo ulimaanisha kitu gani?
"Price discrimination " nitatoa mfano, bei ya bia katika Eneo au baa Fulani ni tofauti na na baa au Eneo Fulani. Lakini bia ni ile ile iliyotengenezwa na kiwanda kilekile. Utofauti huu Wa bei unaweza kusababishwa na aina ya tukio lenyewe ( event), mtu ( rickross) au umaarufu wa sehemu ile. Kwa hiyo umaarufu wa event hiyo, mtu huyo, au sehemu hiyo inaweza kuongeza bei ya services au products zile zile.

Mfano mwingine, mechi utofauti utofauti zinazochezwa uwanja Wa taifa huwa na viingilio utofauti utofauti.
 
Mi nakushauri kwanza wewe mwenyewe uwe na wazo la biashara unayotaka kuifanya kwa mtaji wako huo halafu ndo wadau wakushauri kwa kukufanyia analyisis, biashara ni kama imani, biashara unayoipenda utaipigania mpaka itafika pale unapotaka ifike, lakini ukifanya kitu kwa sababu umeshuriwa tu na sio kutoka moyoni unaweza kupata shida kutaka kuiendeleza vyema. Lakini wazo la mtu laweza kukufaa pia kama ni sehemu ya mapendekezo yako.

Huo ni mtazamo wangu tu katika kuchangia wazo la mdau.
Ushauri murua
 
hiyo hela ni nyingi sana kama utakuwa makini nayo jaribu biashara ya paspot express inalipa sana printer ya canon kama laki3 camera kama ya laki na nusu inatosha sio lazima uwe na frem waeza kwenda frem ya mtu ukamwomba space ukamtoa kias kwa siku kama sehemu ni potential hasa stand, vyuoni, mahakamani au masokoni, kwenye benk nyingi nyingi au wanapokutana saccos au vicoba hzo sehemu ukipata ukaweka pazia lako waeza pata daily buku 20atleast na ukasahau ajira kadri siku zinasonga unaweza jiongeza ukapata kibanda chako ukawa huru kuongeza hata vitu vingine kama kuuza frem vocha flAsh, memory card,usb cables, etc ukichakalika hyo hela itakukomboa
Umesema jambo jema sana!
 
Habari zenu wapendwa

Bila shaka muwazima wa afya. Kama kichwa cha habari kinavyo jieleza hapo juu.

Nimejibana bana mpaka nikapata laki tano kutokana na maisha yalivyo magumu nkaona niombe ushauri kwenu wadau.

Je, hii pesa naweza kuifanyia biashara gani ambayo haitachukua muda wangu sana manake kuna shughuli nyingine nafanya.

Nipo Dar Mbezi Makonde. Naombeni ushauri wadau angalau niweze kuingia risk huku na kule maisha yaende.

Asanteni..
Soko naweza uza wapi hapa dar ?
 
Na kwa wazoefu wa mafinga mjini mtaji huo wa laki 5 shughuli gan inaweza kifanyika?
 
Masanja mkandamizaji alitoa mchanganuo mzuri kuhusu laki tano.......Ukimtafuta atakusaidia.
 
Back
Top Bottom