Kwa mtaji wa Shilingi 1,200,000 unaweza kufanya biashara gani Dar es Salaam?

Abdul Mganyizi

JF-Expert Member
Oct 28, 2019
1,044
1,996
Habari zenu wana jamvi,

Nimepata mtaji kiasi cha sh 1,200,000/= lengo langu nifanye biashara ya kupata sh 20,000-30,000/= kwa siku. Je inawezekana kupata biashara ya kuingiza kiasi hicho?

Kuna mmoja kanishauri biashara ya kuuza juisi ya miwa kwa kumuweka mtu anifanyie maana yake mimi nipo mkoani, lakini bado sijaifikiria na kupata majawabu.

Nishaurini wadau biashara gani nifanye?

====

Pia, soma:
--Mtaji wa Tsh. Milioni 1 hadi 5: Naweza kufanya Biashara gani Tanzania?
-- Mtaji wa milioni 1 na laki 2 naweza fanya biashara gani Dar es Salaam?
 
Watakuja watu flani wanaitwa Forex. Usiwasikilize.

Me nashauri hivi:

(1) Tembeza maofisini mashuka, viatu au mashati. Wanaume tunapeana sana support.

(2) Anzisha "goli" la nguo, unaweza kuanza na za kiume tu au mashati tu au suruali tu.

(3) Kama upo vizuri kwenye "social media" fanya biashara za nguo na viatu online.

(4) Kama una eneo la wazi fuga basi (Kuku).

(5) Usidharau biashara ya chips, na juice. Mtaji mdogo ila unaweza fungua "magoli" kibao mjini hapa.

Ebu ngoja na wadau wengine waje.
 
Mkuu, chukua laki moja (100,000) fanya betting kwenye mechi ya Simba na Yanga. Usiweke kwamba Simba anashinda au Yanga lazima ashinde, hapana, bali chagua ile option kuwa mechi lazima iishe kwa ushindi na hakuna draw.

Pesa inayobaki 1,100,000/= ndio ufanyie mambo mengine sasa. Kufanya betting ya namna hii mara moja kwa mwezi sio jambo baya.
 
Watakuja watu flani wanaitwa Forex. Usiwasikilize.

Me nashauri hivi:

(1) Tembeza maofisini mashuka, viatu au mashati. Wanaume tunapeana sana support.

(2) Anzisha "goli" la nguo, unaweza kuanza na za kiume tu au mashati tu au suruali tu.

(3) Kama upo vizuri kwenye "social media" fanya biashara za nguo na viatu online.

(4) Kama una eneo la wazi fuga basi (Kuku).

(5) Usidharau biashara ya chips, na juice. Mtaji mdogo ila unaweza fungua "magoli" kibao mjini hapa.

Ebu ngoja na wadau wengine waje.
Jamaa kasema yupo mkoani 😳😳 hustles Dar
 
Mkuu kama unaweza ufugaji wekeza kwenye kuku wa kienyeji chuku 500K inatosha kwa kuanzia
 
Back
Top Bottom