Kwa mtaji wa 25 million nifanye biashara gani?

Salam sana wakubwa na wadogo.

Nahitaji idea nzuri ya biashara ambayo
Haina usimamizi mgumu kwasababu mimi ni mwanafunzi ambaye niko chuoni kwahio mda mwingi nakuwa darasani.

KWAHIYO NILIKUWA NAWAZA KUTUMIA HIZI FEDHA KUANZISHA BIASHARA WAKATI MIMI NIKIWA NASOMA..

Baadhi ya biashara nilizowaza ni Kuanzisha
1. Biashara ya daladala au bajaji au hata toyo
2. Biashara ya nguo (kama nikipata msimamizi)
3. Biashara ya bondo za samaki(lakin hii sina research juu yake) labda kwa watu mnayoijua mnawezaa mkanipa ushauri.
 
Matokeo ya ushauri huu Ni haya
Asante sana Bloodstone, ushauri wako nimeona kuwa ni kati ya ushauri bora sana. Nitaendelea kuwasiliana nawe zaidi mkuu.
IMG-20191201-WA0082.jpeg
IMG-20191201-WA0083.jpeg
IMG-20191201-WA0080.jpeg
 
Ingiza kwenye forex ila zingatia haya:

1. Wekeza kwenye elimu ya forex for minimum of 2.5 years join reputable forex academy kama utaanza mwezi huu target ya kuanza kutrade live iwe July 2021

Ila kama huna au hujui biashara ya kufanya hujui unapoelekea mkuu
 
Darmajeks,
mkuu biashara ya daladala sikushauri kabisa maana mm ninayo ila inasumbua sana .sio ubovu wa gari wala matrafki ila roho zetu tuu wanadamu na mambo ya kitamaduni mkuu
Mi naona daladala Ni Kati ya biashara nzuri.
Funguka ni Mambo gani hayo.
Nina mpango wa kununua TATA niingize huko.
 
Mi naona daladala Ni Kati ya biashara nzuri.
Funguka ni Mambo gani hayo.
Nina mpango wa kununua TATA niingize huko.
Mkuu, biashara ya daladala inafaa na pia haifai mimi nimefanya miaka mitano hiyo biashara niliona mengi sasa ngoja nikuambie wapi inafaa na wapi haifai;

Inafaa ikiwa utakuwa na bahati ya kupitia yafuatyo- ukampata dereva mzuri anaejua nini anafanya, ukanunua gari mpya, nunua gari ambayo ukiataka kuiuza haitakusumbua kupata mteja na ukinunua gari mpya angalau ifanye kazi kwa miaka 4 utakuwa umerudisha hela na umepata faida ya kununua gari nyiningine pia.Hapa pia ni kama gari haitasababisha ajali za mara kwa mara na kubwa maana ajali ndogo hazikwepeki.

Kinyume cha hayo nilioandika hapo juu hii biashara haitakufaa kwani ukinunua gari ya mkononi ni pasua kichwa sana na kwa sababu huna uzoefu matengenezo yatakusumbua mnoo, madereva ndio tatizo kubwa kwenye biashara hii na pia usihadaike na faida za mezani kuna siku gari itaharibika itakaa garage hata zaidi ya wiki na pia dereva anaweza kuumwa akalala ndani hata wiki na pia mvua zikinyesha nyingi sku kazaa pia inaaffect hii biashara.

Kama umedhamiria kuingia kwenye hii biashara basi kwanza nakushauri ufuate ushauri wangu hapo kwenye ''inafaa'' na kama ujuavyo biashara inahitaji ''mentorship'' tafuta mtu anaefanya hiyo biashara akuelimishe kuhusu aina ya gari ya kununua na elimu namna ya kuoperate kabla ya kununua gari na endapo utaaply inafaa option basi baada ya miaka minne unaweza kuuza gari na ukanunua nyingine ukaanza moja.
 
Kua wakala wa mabenki na huduma za pesa kwa njia za simu, kata chumba hicho kama ni kikubwa weka vyerehani kama vitano na washonaji..wape hesabu ya buku tano tu per day kwa kila cherehani au buku 7.

Over
Nina frame dodoma one way mjini barabara ya tisa karibu na mskiti nina Mtaji wa millioni 25 mnanishauri ni biashara gani nzuri naweza kufungua
 
Kua wakala wa mabenki na huduma za pesa kwa njia za simu, kata chumba hicho kama ni kikubwa weka vyerehani kama vitano na washonaji..wape hesabu ya buku tano tu per day kwa kula cherehani au buku 7.

Over
Huu ushauri wako wa vyerehani nimeupenda kweli ngoja niufanyie utafiti
 
Huu ushauri wako wa vyerehani nimeupenda kweli ngoja niufanyie utafiti
Na usiwaze kuweka pesa yako yote kwenye biashara..anza kidogo kidogo,mapato madogo madogo ndo hukuza akili na mtaji
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom