Kwa mtaji wa 25 million nifanye biashara gani?

Nunua I.S.T tatu used kwa mtu lakini zilizo katika hali nzuri kuanzia namba C au D kwa bei ya 7m kila moja. Jumla 21m. Milioni 2 kushughulikia uhamisho wa umiliki na vibali. Jiunge na Uber tafuta vijana watatu mtaani waliomaliza chuo wenye driving licences na upajue kwao wanapoishi na wawe na wadhamini wa kueleweka. Kila siku kila mmoja akuletee Tshs 40k jumla ni 120k kwa siku kwa mwezi ni 3.6 m. Kwa mwaka ni 43,200,000.
Mkuu unauhakika uber anaweza kulaza 40 per day?
 
Sijawahi kufanya biashara ya aina yeyote isipokuwa nimefanikiwa kukusanya kiasi cha Tshs 25/-m ambazo nafikiria kujiajiri kwa kufanya biashara.

Naomba wazoefu wa Jiji la Dar mnipe ushauri juu ya biashara ya kufanya tafadhali.
Biashara ya kutoa mbao Iringa kupeleka sehemu zenye upungufu ni deal, jaribu!!
 
Fungua duka la jumla lenye bidhaa mchanganyoko na vinywaji vyote
Tagufuta vijana 2 salesmen wa kutafuta order madukani na kusambaza mitaani kwa kitumia baskeli na mkokoteni mshahara wao no 80x2 = 160.000
Uwe wakala wa vinywaji vya Mo , Azam, Maji Afya na Pespsi

Ambapo unakua na uhakika wa kuuzia wenye maduka madogo kwa eneo kubwa
Kwa mil 25 faida kwa mwezi ni 3m
Biashara ya jumla haina hasara
 
Sijawahi kufanya biashara ya aina yeyote isipokuwa nimefanikiwa kukusanya kiasi cha Tshs 25/-m ambazo nafikiria kujiajiri kwa kufanya biashara.

Naomba wazoefu wa Jiji la Dar mnipe ushauri juu ya biashara ya kufanya tafadhali.
Mkuu lete mrejesho Basi, biashara ipi unayoona inakutoa? Au bado upo kwenye research?
 
watu kila Siku lazima wale chakula na kila Siku watu wanasafiri angalia kati ya hizo zinafaa
Na watu wanaumwa deile, so wazo la mdau hapo juu la kifungua duka la dawa baridi almaarufu famasi ni wazo zuri kama unahitaji biashara stable
 
Kawaida kwenye hali ya namna hii ambako hakuna mzunguko wa pesa huwa tuna angalia biashara zinazogusa mahitaji ya lazima kama vile makazi, magadhi na chakula tunaweza kusubiri hali hii ipite labda 2025 kwa kupunguza manunuzi ya mvavazi na kuachana na ujenzi lakini hatuwezi kuacha kula kwani tuta dead. hivyo ushauri wangu wekeza mzigo kwenye kilimo focus kwenye nafaka especially mpunga ukiweza kupata maeneo ambayo utaweza kununua mashine ukamwagilia hivyo kulima mwaka mzima itakuwa bora zaidi to me ndio naona njia pekee ya kutunza na kukuza mtaji wako mpaka tuvuke hapa tulipo.
 
Wazo tu sijui kama pesa yako itatosha: nunua Gari aina ya Noah alafu utafute wazazi ambao watoto wao wanasoma shule za mbali kidogo kuwapunguzia gharama za usafiri mtoto mmoja alipie elf 30 kwa mwezi, ukipata watoto 8 ina maana utapata 240000× siku 30 utapata 7200000 toa gharama za mafuta kila siku 20000 ×30=600000 utabakiwa na 6600000, service ya Gari laki 200,000 emergency 200,000 utabakiwa na 6200000, dereva ww mwenyewe. Hy ni rough calculation kukosoa ruksa
Mtoto mmoja akilipia 30,000*8=240,000 hayo ndo mauzo yako ya mwezi usizidishe 30 maana inalipwa mara moja kwa mwezi kifupi biashara hiyo hailipi
 
Jamaa yangu ameomba ushauri,nimeona nilete jamvini:

Nimejifunza mengi kwa muda mrefu,...ninafanya shughuli nyingine ambayo inanihitaji niwepo muda mwingi....lakini nina mtaji kama 20m ambayo ninataka kuwekeza sehemu nyingine ili niongeze wigo wa kipato lakini napata changamoto ya kuwekeza ukizingatia sintokuwepo full time sababu

1. Asilimia 95% ya fursa zinazotangazwa ni za kitapeli kama vile Namaingo,BitClub,Forex nk kote huko nimepigwa vya kutosha

2. Nikifungua biashara na kumuweka kijana ...ni maumivu matupu kwani sasa nimeamini hakuna kijana wa kumpa kazi akafanya na ukatengeneza hela

3. Biashara za mtandaoni 99% ni za kitapeli

Sasa nimekwama kabisa. Natafuta mawazo mapya kama yapo.
Duh hata mimi nakuna kichwa, mwenye wazo jipya anakaribishwa.
 
Back
Top Bottom