Kwa mtaji wa 25 million nifanye biashara gani?

Mandison

Senior Member
Mar 10, 2017
191
109
Sijawahi kufanya biashara ya aina yeyote isipokuwa nimefanikiwa kukusanya kiasi cha Tshs 25/- milioni ambazo nafikiria kujiajiri kwa kufanya biashara.

Naomba wazoefu wa Jiji la Dar mnipe ushauri juu ya biashara ya kufanya tafadhali.

Maoni ya wadau:
Kama utaona yakufaa fanya hivi:

1. Nunua pikipiki 5 jumla ni milioni 10. Wape vijana kwa mkataba wa kisheria wakupe elfu 10 kwa siku baada ya Mwaka unamwachia pikipiki. ( uwape mkataba wa kisheria akipoteza anakulipa) kwa siku ni 50000 sasa itakuwa 50000×365 = 18,250,000

Faida kwa mwaka ni 8,250,000. Kwa mwezi ni kama 687,500.

2. Fungua M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money & Halopesa mahali vibanda viwili pia usajili laini hapo hapo. Kibanda cha kwanza mtaji 2mil, makadirio ya commission 350,000 (mfanyakazi laki, kibanda 50,000, umebaki na 200,000)
Kwa hiyo vibanda viwili baada ya kodi na mishahara yao makadirio ya faida ni 200,000 × 2 = 400,000 Fanya 350,000 incase of anything.

Milioni 6 Iliyobaki: 3mil weka M-Pawa au fixed account ikulinde.

Milioni 3 nyingine fungua kaduka fulani kadogo lakini ka wadhifa weka vyakula au bidhaa za urembo (au yoyote isiyooza) Soma soko lakini 'ANZIA SOKONI' Hapo utapata hela ya kula daily, vocha, home kuacha elfu 5 kama una familia.

Kwa haraka haraka utakuwa umetengeneza mshahara 687,500 (pikipiki) + 350,000 (M-Pesa n.k) = 10337500 yaani milioni kila mwezi.

Kumbuka mtaji wako uko pale pale ndugu. Kila la heri na shetani asipite huko maana kazidi.
Nunua IST tatu used kwa mtu lakini zilizo katika hali nzuri kuanzia namba C au D kwa bei ya 7m kila moja. Jumla 21m. Milioni 2 kushughulikia uhamisho wa umiliki na vibali. Jiunge na Uber tafuta vijana watatu mtaani waliomaliza chuo wenye driving licences na upajue kwao wanapoishi na wawe na wadhamini wa kueleweka. Kila siku kila mmoja akuletee Tshs 40k jumla ni 120k kwa siku kwa mwezi ni 3.6 m. Kwa mwaka ni 43,200,000.
Biashara za mazao zinalipa sana, na kwa mtaji huo naamin unatosha kabisa kuanza biashara hiyo lakini biashara zipo nyingi, cha msingi angalia wewe unapenda nini maana itakuwa rahisi kukifanya na kukisimamia ili upate faida zaidi
Mimi nashauri ufanye biashara ya kuimport vyakula jumla jumla hapo kama unatoa Mbeya viazi unaleta mjini au ndizi Bukoba unaleta mjini ni biashara nzuri ukipata dalali mwenye wateja wengi
Chukua mil.5 tafuta sehemu yenye muonekano mzuri na watu wengi fungua COSMETICS and mambo ya kutengeneza kucha wadada.
Kaka hizo hela nyingi sana tuliza akili utakuwa tajiri ndani ya mwaka tu usilete ushikaji wala kuhonga idea ziko nyingi sana za kukutoa kiufupi kila biashara INA faida nzuri tegemea na uwekezaji na jinsi ya kufanya hiashara kamwe usiruhusu mawazo ya MTU eti panda mbegu vuna mbegu au kubet
Mafanikio mema
 
Mtaji mkubwa sana huo na vilevile mtaji mdogo sana huo.
Cha msingi usiiweke ela yote kwenye kitu kimoja, igawanye hata mara 3.

Ili biashara yeyote iwe na mafanikio endelevu ni lazima kuangalia usalama wa mtaji kwanza kabla ya kuangalia faida.
Ni sawa, ila ni biashara gani sasa?
 
Kuna uwezekano mkubwa sana wa wewe kuzipoteza hizo hela kama utafata ushauri wa watu humu jukwaani
 
kuna uwezekano mkubwa sana wa wewe kuzipoteza hizo hela kama utafata ushauri wa watu humu jukwaani
Inategemea ni ushauri gani na pia wanasema akili za kuambiwa changanya na zako..
Baada ya hapo hutomlaumu aliyekupa ushauri kwani ulipata nafasi ya kuchuja huo ushauri na kuona faida na hasara zake.
Tusiwakatishe tamaa wale wenye moyo wa kujitolea kuwapa wenzao ushauri humu jukwaani.
 
Back
Top Bottom